Ndoa ya mama PHD na baba standard seven

Ndoa ya mama PHD na baba standard seven

kwa maisha yetu ya kibongobongo mwanaume kumuoa mwanamke aliyemzidi elimu mmmm...hapo ndo mwanaume atakuwa kaolewa na kichwa cha familia atakuwa mwanamke PHD ninayoijua mimi c mchezo jaman,mtu wa STD 7 kumuongoza educated woman ni ngumu hata kama utakua ukitoa mawazo sahihi utakua hujiamin na utajishusha thaman hutaweza kuwa na kauli ya kumkontrol wife by the way awe STD7 na awe na mkwanja wa maana kumzidi wife hapo ataheshimika bt else hiyo ni tungo tata 4me
 
Hapo ni sawa na kuagiza bangi kwa eBay.

HAKUNA NDOA HAPO.
 
Mimi sioni tatizo,kikubwa ni kupendana na kuheshimiana!Elimu ni muhimu lakini haiwezi kuzuia wapendanao washindwe kuishi pamoja!mwanamke atakuwa anatoa theories alizosoma darasani ili mwanaume ajifunze kutoka kwake.On the other hand mwanaume atakuwa anampa mke wake real life context principles,mwisho wa siku kila mtu atakuwa ana cha kujifunza kutoka kwa mwezake na ndoa inaweza kudumu!

Inawezekana kabisa mradi kuwe na mapenzi ya kweli. Pia wapo wanaume wana Ph.d na wameoa wa darasa la saba/shule ya msingi
 
Habari zenu wakuu. Naombeni mawazo yenu nimsaidie dada yangu maana yuko katika wakati mgumu wa kuamua.

Ni dada mwenye miaka 32, mtoto mmoja, elimu ya PHD. Amekutana na mwanaume, mfanya biashara wa kawaida tu, elimu std 7, anaemzidi kama miaka mitatu. Wanapendana na mwanaume amepropose anataka wafunge ndoa haraka iwezekanavyo. kinachomtatiza ndugu yangu ni kwamba anawasiwasi kuwa understanding capacity yao inaweza kuja kuwaletea shida huko baadae as wanaume wakioa wanawake wa aina hii kunakuwaga na inferiority complex fulani na mara nyingi hawachukulii vitu vingi kwa namna sawa. Kuna ambae ana uzoefu na jambo hili na wenye mawazo naomba tumsaidie ndugu yetu. natanguliza shukran
Msingi mkubwa wa ndoa ni upendo; ambao ndani yake kuna kuheshimiana, kuaminiana, kusaidiana nk. Hii inakuwa rahisi zaidi iwapo wahusika wanalingana au wanaendana kwa mambo mengi ya msingi kutokana na mila na desturi zao, kwa mfano umri, mila na desturi, kipato, elimu, dini, nk. Katika mila za kiaafrika inapotokea mwanamke (mke) amemzidi sana mwanamme(mume) kielimu, kimapato nk. Heshima ya mwanamke kwa mwanamme itapungua sana na ndoa hii ni rahisi kuvunjika. Mwanamke akiwa na kipato cha kutosha au elimu ya kumzidi mumewe basi anakuwa na NYODO nyingi. Mifano iko mingi tu. Ni afadhali mwanamme ajaliwe vitu hivyo. Siyo rahisi kwa mwanamme kuwa na NYODO kwa mkewe iwapo atakuwa na elimu au kipato cha kutosha dhidi ya mkewe. Wanaume wana HURUMA sana. Ndoa ambayo mwanamme amemzidi mkewe kipato au elimu, itadumu zaidi kuliko kinyume chake.(sitaki matusi)
 
Uislam kigezo cha ndoa ni DINI mengine ziada pakiwepo na dini hata kama elimu to mmezidiana walau mtakutana kwenye dini na hapo kila kitu kitarekebishwa maana kusoma ni rizk ni majaala wengi hawajasoma sio kwasababu hawakujua umuhimu wa elimu la! hawakubapata fursa,, lakini kwenye ndo elimu inasehemu ndogo sana maana mimi kama ni fundi baiskeli na mke wangu Daktari mambo yangu ya baisketi definetely haya muhusu na mimi yake ya udaktari haya hayanihusu mahaba tu ndo maa wasomi wengii wanaibiwa wake zao maana wao hata wakirudi home ni yes no yes no tu na matheory kibao mapenzi hakuna.... hata kwenye mambo ya faragha pia shida kubwa maana wako very tressed wenzangu na mimi kwa mahaba usipime mama atamkimbia msomi na kuolewa na masikini... DINI baaas
 
Tusiofika hata la saba sijui tusemeje kama ndo hivyo
 
Ushauri mkubwa hapo ni kwamba achukue tahadhali. Asithubutu kufanya papara ili tu aolewe. Chukua muda kujifunza tabia zenu na kufahamiana kwa undani zaidi ili kupima mambo yatakuwaje ktk siku za usoni.
 
How did you sort this? What happened? Je walioana?

Sorry kwa kutoleta feedback. yeah waliona hawa watu, ndoa yao ina mwaka na wana mtoto tayari, so far wako poa ingawa wao ndio wanajua ndani kwao kukoja, lakini from a curious eye, wako vizuri. Shukrani kwa wale walitoa mawazo yao
 
NDOA kama ndoa inawezekana ila MAISHA YA NDOA yanaweza yasiwezekane!.
 
Waoane tu ila ni baada ya kila mmoja wao kujiridhisha kama mwenza anaweza kukaa ktk nafasi yake kama "mume" au kama "mke" na sio kama "PHD" au "STD 7".Vigezo artificial watupe kuleee,waangalie vigezo asilia.Wakifanya hivyo im sure watainjoy sana ndoa yao mpaka watu wawaonee donge na huo ndio utakuwa mwanzo wa mapinduzi ya mitazamo hasi juu ishu kama hiyo!
 
Mimi sioni tatizo,kikubwa ni kupendana na kuheshimiana!Elimu ni muhimu lakini haiwezi kuzuia wapendanao washindwe kuishi pamoja!mwanamke atakuwa anatoa theories alizosoma darasani ili mwanaume ajifunze kutoka kwake.On the other hand mwanaume atakuwa anampa mke wake real life context principles,mwisho wa siku kila mtu atakuwa ana cha kujifunza kutoka kwa mwezake na ndoa inaweza kudumu!

Ni mpaka umkute huyu mwanamke mwelewa otherwise ni wanawake waliosoma mara nyingi hu behave u much know too much! Hawako tayari kusikia asiyesoma naye anatoa hoja, pia hawako tayari kujifunza kutoka kwa wasiosoma wakidhani kwa kusoma kwao basi wamebarikiwa kujua kila kitu.
 
Katika tofauti hii ya elimu ni kwa neema ya Mungu, maana mwanzoni mwa ndoa mambo uwa mazuri na masikilizano. Mapenzi yakipungua ndiyo tofauti ya elemu uanza kuonekana na shida ya ndoa uanzia hapo.

Wanatakiwa kujitafakali kwa undani kabla hawajaamua kujiweka kitanzi cha ndoa.
 
Kumbuka hakunaga formula katika swala kama hilo na kama PHD ndo anaona ina maana sana Basi abaki hapo hapo na PHD yake lakini kitu cha msingi ni kwamba ajaribu kufikiria kwa usahihi zaidi ili aweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Uliona wap + na + zikazlisha umeme lazima +- Ndo umeme unaweza patikana so kama anataka msomi mwenzie hapo itakuwa matatizoooooooo
 
Msingi mkubwa wa ndoa ni upendo; ambao ndani yake kuna kuheshimiana, kuaminiana, kusaidiana nk. Hii inakuwa rahisi zaidi iwapo wahusika wanalingana au wanaendana kwa mambo mengi ya msingi kutokana na mila na desturi zao, kwa mfano umri, mila na desturi, kipato, elimu, dini, nk. Katika mila za kiaafrika inapotokea mwanamke (mke) amemzidi sana mwanamme(mume) kielimu, kimapato nk. Heshima ya mwanamke kwa mwanamme itapungua sana na ndoa hii ni rahisi kuvunjika. Mwanamke akiwa na kipato cha kutosha au elimu ya kumzidi mumewe basi anakuwa na NYODO nyingi. Mifano iko mingi tu. Ni afadhali mwanamme ajaliwe vitu hivyo. Siyo rahisi kwa mwanamme kuwa na NYODO kwa mkewe iwapo atakuwa na elimu au kipato cha kutosha dhidi ya mkewe. Wanaume wana HURUMA sana. Ndoa ambayo mwanamme amemzidi mkewe kipato au elimu, itadumu zaidi kuliko kinyume chake.(sitaki matusi)

Mh;
naunga mkono hoja
 
miaka 32 ana PHD?sina uhakika,anybade to help!

nyie mko dunia gani jameni? mimi ni mmojawapo. Ukimaliza degree ya kwanza na miaka 24, ukaanza masters na miaka 25 ukamaliza na miaka 27 ukaanza phd na miaka 29 utamaliza ukiwa na umri huo.
 
Back
Top Bottom