Ndoa ya mama PHD na baba standard seven

Ndoa ya mama PHD na baba standard seven

Hiyo ndoa haitadumu maana mmoja wao lazima atajipaisha na kumdharau mwenzake
 
kwa maisha yetu ya kibongobongo mwanaume kumuoa mwanamke aliyemzidi elimu mmmm...hapo ndo mwanaume atakuwa kaolewa na kichwa cha familia atakuwa mwanamke PHD ninayoijua mimi c mchezo jaman,mtu wa STD 7 kumuongoza educated woman ni ngumu hata kama utakua ukitoa mawazo sahihi utakua hujiamin na utajishusha thaman hutaweza kuwa na kauli ya kumkontrol wife by the way awe STD7 na awe na mkwanja wa maana kumzidi wife hapo ataheshimika bt else hiyo ni tungo tata 4me

Kumbe kwako umeona Soln ni pexa km upendo wa dhat hakuna hta uwe na pexa kiac gan nisawa kaz bure mpnde vle alvyo ucmpende mtu kwa kuwa ana kit na pia kuwa na elmu sio kuelemika tuna ma Prof hapa Tz wanaishia kubaka tu
nguv ya elm ina umuhmu pale inapo tumika
 
Kimaumbile, mwanaume ameumbwa kumtimizia matakwa ya mke wake, kuanzia kumlisha kumvisha na mengineyo! ili family iwe stable lazima mwanaume amzidi mwanamke kipato/elimu au vyote!

Kwa situation hiyo the only way possible ni mwanaume awe Bilionea otherwise awe serengeti boy akubali kila anachoambiwa.
 
tz hii?hebu nipe mchanganuo niridhike!anzia toka vidudu

Mpwa Neylu:Kupata PhD katika umri huo inawezekana tu,wengi wanapata hata ndani ya 20's.Nikupe mchanganua,Kwa mfano mtu awe amezaliwa tarehe:1.1.1981. Na awe amesoma Tanzania tena shule zetu za kata.(achana na zile international school ambazo watoto wanasoma mda mfupi na wanajijunga vyuo)

MCHANGANUO:-
Januari 1981-Desemba 1986=Kuzaliwa + Chekechea

Januari 1987-Desemba 1993=Shule ya msingi

Januari 1994-Desemba 1997=O'level

Julai 1998-May 2000=A' level

Septemba 2001-Julai 2004=Bachelor

September 2005- Julai 2008=Master

Septemba 2008-Julai 2012=PhD


Huo mchanganuo ni kwa mfumo wa elimu ya Tanzania wa zamani wa kutegemea sponsorship ya serikali ktk kulipiwa vyuo,Ila kama aliamua kujilipia mwenyewe chuo (bachelor degree) angeunganisha tu na kumaliza mapema zaidi (2010)

Mambo yanawezekana na watu wengi wamesoma kwa staili hiyo,Ila wazazi wakikuchelewesha kukuanzisha shule ya msingi au ukawa kilaza kurudia mwaka/miaka au ukipatwa na magonjwa na kusitisha masomo kwa muda, ndo hapo mtu anamaliza au kupata PhD akiwa na umri mkubwa sana.
 
Habari zenu wakuu. Naombeni mawazo yenu nimsaidie dada yangu maana yuko katika wakati mgumu wa kuamua.

Ni dada mwenye miaka 32, mtoto mmoja, elimu ya PHD. Amekutana na mwanaume, mfanya biashara wa kawaida tu, elimu std 7, anaemzidi kama miaka mitatu. Wanapendana na mwanaume amepropose anataka wafunge ndoa haraka iwezekanavyo. kinachomtatiza ndugu yangu ni kwamba anawasiwasi kuwa understanding capacity yao inaweza kuja kuwaletea shida huko baadae as wanaume wakioa wanawake wa aina hii kunakuwaga na inferiority complex fulani na mara nyingi hawachukulii vitu vingi kwa namna sawa. Kuna ambae ana uzoefu na jambo hili na wenye mawazo naomba tumsaidie ndugu yetu. natanguliza shukran

Mbona Dada yako anaolewa akiwa na mtoto wa mwanamume mwingine??? huyo wa kwanza na aliye mzalisha walishindwana nini?? Kijana standard 7 soma alama za nyakati ila mapenzi ni uhuru wa waliopendana. na huyo dada yako akitaka afurahie hio ndoa arudishe mtoto wa watu kwa baba yake hapo atakuwa salama ndani ya ndoa hiyo otherwise ategemee ugomvi utakao sababishwa na wivu.
 
In love ,nothin is impossible. Hiyo ni michango yetu tu, lkn ukwel wa moyo upo nafsin mwa wahusika. Why negativity and not positivity? Arrg!
 
STD kama ana hela yaani mfanyabiashara maarufu hapo ndoa itawezekana lkn kama hana kitu hamna ndoa hapo!

Kamshinda mno kwa elimu na yy amshinde sana kwa pesa
 
Mmmh PHD..STD 7!!!
Siku mapenzi yakipungua mwanaume atajutaa huko ndani, labda aombe apendwe daima na milele na mwanamke awe na busara za kutosha!!!!
Kwasababu hii imesemwa na KE basi huu ndo utakuwa uhalisia.
 
Hii itawezekana tu kama mwanamke ataiacha Ph.D yake mlangoni kila aingiapo nyumbani. Tofauti na hapo, misuguano haitaisha na ndoa itakuwa vurugu kwani mitazamo itakuwa imeachana sana.
 
Kama walielewana tangu urafiki mpaka uchumba wataendelea kuelewana mpaka ndani ya ndoa. Ndoa ni zaidi ya kuwa na elimu na pesa
 
Kama anampenda kabisa huyo jamaa kutoka moyoni aolewe tu...tofauti na hapo asiolewe. Upendo ndo autumie kuamua maana kama anampenda ataweza kujishusha kama mama na kuvumilia siku wakiwa wametofautiana. Maana hata kama mwanaume anahela kiasi gani maisha huwa hayatabiriki kuna kupanda na kushuka. Kama anampenda kweli wataelewana tu. Cha muhimu wawe wanapendana kweli.
 
Habari zenu wakuu. Naombeni mawazo yenu nimsaidie dada yangu maana yuko katika wakati mgumu wa kuamua.

Ni dada mwenye miaka 32, mtoto mmoja, elimu ya PHD. Amekutana na mwanaume, mfanya biashara wa kawaida tu, elimu std 7, anaemzidi kama miaka mitatu. Wanapendana na mwanaume amepropose anataka wafunge ndoa haraka iwezekanavyo. kinachomtatiza ndugu yangu ni kwamba anawasiwasi kuwa understanding capacity yao inaweza kuja kuwaletea shida huko baadae as wanaume wakioa wanawake wa aina hii kunakuwaga na inferiority complex fulani na mara nyingi hawachukulii vitu vingi kwa namna sawa. Kuna ambae ana uzoefu na jambo hili na wenye mawazo naomba tumsaidie ndugu yetu. natanguliza shukran
watu wanasema pamenzi hayachagui... lakini tuwe wakweli, mapenzi yanachagua wa kufanana naye...

Hiyo relationship ni recipe for a disaster... DONT EVEN TRY IT
 
Kwa mwendo huu sisi wa STD 7....ndio basi tena...maana STD7 wenzetu wanataka wasomi
Na wasomi nao tukiwatongoza kutukubalia mpaka waje watutungie thread huku....Kazi ipo....
 
Hii itawezekana tu kama mwanamke ataiacha Ph.D yake mlangoni kila aingiapo nyumbani. Tofauti na hapo, misuguano haitaisha na ndoa itakuwa vurugu kwani mitazamo itakuwa imeachana sana.
ni bora mwanamke akuzidi umri ila sio kipato na elimu
 
Back
Top Bottom