Ndoa VS Usioe grand finale!

Girland

JF-Expert Member
Jan 24, 2016
1,826
2,843
TEAM NDOA VS TEAM USIOE
Mjadala huu mkali umeshika kasi huku kila upande ukitoa sababu zake! Kabla hujaamua uunge mkono upande upi ni vyema ukajitafakari na kuona Kama uamuzi wako binafsi una mantiki na manufaa kwako.

NDOA NI KWA AJILI YA NANI?
 U
kipata majibu ya swali hili utaelewa maana halisi ya ndoa. Ndoa ni kwa ajili ya mke na Mume. Watu wengi hufikiri ndoa ni kwaajili ya mwanamke na mwanaume!! Ni "mume " tu ndiye anayeweza kuishi na "mke "katika ndoa.

Hata katika maandiko imeandikwa apataye mke apata kitu chema,...
Hawajaandika apataye "mwanamke "maana wanajua kabisa kuwa Siyo kila mwanamke anafaa kuwa "mke "!!

Kosa kubwa ni Mume anapooa "mwanamke "akifikiri ni "mke "au "mke "anapoolewa na "mwanaume " akidhani kwamba ni "mume ".Ndoa ya aina hii itakuwa ngumu Sana!

JE NIOE /NISIOE?
hili litategemea Kama wewe ni "mume " au mwanaume, wa kwanza (mume) anapaswa kutafuta mke amuoe. Lakini ukijijua wewe ni mwanaume na hauko tayari kuwa "mume " tafadhali usituhangaishe na michango! Tulia na uishi maisha yako maana ndoa ni kwa ajili ya Mume na mke!

JE TUWALAUMU WANAOKATAA NDOA?
HAPANA !Lazima tukubali tofauti zetu! Mfano hatutegemei kuwa na Padri "mume " tunategemea wawe wanaume vivyo hivyo kwa masista. Ukiacha hawa kuna wanawake ambao maisha yote hawawezi kuwa "wake " ,ila wanaweza kuwa wanawake wa shoka (super woman) Usishangae kuona Super woman wengi ndoa zao ziko chali ni sababu hiyo hapo juu! KUWA SUPER WOMAN HAKUKUFANYI KUWA SUPER WIFE 😀

NAKALA KWA Robert Heriel na Mshana Jr nawasilisha
 
Bora TU ukae Kama ukwaju kila mbegu na Ganda lake kuliko kuharakia kuoa.
1662144081333.jpg
 
Back
Top Bottom