Ndoa si Upendo?... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa si Upendo?...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by PakaJimmy, Jul 19, 2009.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Leo nasoma gazeti fulani, nikashangaa kuona kichwa cha habari:
  NDOA SI UPENDO!
  Nimeshangaa sana... Je wanaJF, NI KWELI NDOA SI UPENDO?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,905
  Trophy Points: 280
  Ndoa ni upendo. Huwezi kuamua kumuoa mtu au kuolewa na mtu ambaye kuna uwezekano wa kuwa naye hapa duniani kwa kipindi cha maisha yako yote yaliyobaki bila kumpenda. Lakini kwa kusoma hapa majadiliano mbali mbali kuhusiana na manyanyaso ambayo dada zetu wanapata toka kwa wanaume wao naweza kusema labda kwa wenzetu wanawake labda ndoa si upendo. Maana wanavumilia manyanyaso mengi sana ndani ya ndoa nyingi ikiwemo vipigo, tuhuma za kutembea nje hata pasipo na ushahidi wa kutosha, matusi na karaha mbali mbali. Wengine ambao ni waajiriwa huwakilisha mishahara yao yote kila mwezi kwa waume zao pamoja na manyanyaso hayo eti mwanaume "ndiye apange matumizi ya pesa hizo". Wengine wanaume wao hawarudi majumbani mwao na kulala nje kwa siku moja au hata zaidi lakini bado wamo tu kwenye ndoa hizo.

  Manyanyaso wanayoyapata na kuendelea kuyavumilia yamenishangaza sana hasa ukitilia maanani wengi wanaonekana ni waajiriwa ambao wanaweza kujisupport wenye ingawaje katika hali ya kujibana sana. Lakini naamini kabisa wanawake wote wanapoamua kuolewa hufanya hivyo kwa mapendo makubwa ya hao wenzi wao, lakini cha kushangaza ni kuendelea kuwemo kwao katika ndoa hizo hata kama kuna ushahidi tosha kwamba mapenzi ya wenzao kwao yamepotea kabisa na kila siku wanaishi maisha yasiyokuwa na furaha yoyote na wakati mwingine kuishi maisha yaliyojaa woga dhidi ya wenzao kutokana na vipigo na manyanyaso wanayoyapata.
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nafikiri aliyesema "Ndoa si upendo" alitaka kuweka mkazo wa wazo lake mahali fulani, na si kuukataa kabisa upendo katika ndoa. Vinginevo ni kwenda mbali mno.

  Ni hivi: Upendo tu kati ya mwanaume na mwanamke haufanyi watu hao kuwa mume na mke kwa kuwa tu wanapendana. Ndiyo maana kuna mahawara, wapenzi, nk. Kupendana kwao hakuzai ndoa. Hakuna ndoa hapo

  Na watu wa ndoa waliokuwa wanapendana, upendo unapoisha haina maana kwa tendo hilo tu ndoa imevunjika au imekufa. Ndoa bado ipo hata kama upendo umekwisha.

  Sasa kinachofanya ndoa iwepo ni nini? Ni MAKUBALIANO ya HIARI ya watu wawili (consent) yaliyoidhinishwa mbele ya DC, mchungaji au shehe na mashahidi. Baada ya idhinisho hilo ndoa inazaliwa hata kama kilichowasukuma kufunga ndoa haukuwa upendo bali malengo mengine, mf. nia ya kutaka kuzaa watoto, au kupata heshima ktk jamii.

  Kinachofanya ndoa ivunjike ni nini? Ni uvunjaji rasmi wa makubaliano ya ndoa (mkataba) yaliyowekwa huko nyuma. Kuisha kwa upendo tu peke yake hakutoshi. Lazima wahusika wavunje rasmi mahusiano hayo. Ndoa inavunjwa rasmi pale inapotolewa talaka mahakamani. Hapo hao wawili si mume na mke tena.

  Kumbe ndoa kama "pingu za maisha" inazaliwa pale wawili wanapoweka makubaliano yao kwa hiari mbele ya wajumbe halali. Hicho ndiyo KIINI. Hata hivo, ili ndoa idumu na iweze kuwa ya furaha kwa watu wa ndoa, upendo ni kitu cha lazima. Ukikosekana upendo basi ndoa hiyo iliyofungwa haiwezi kudumu.

  Kwa kifupi ndoa si upendo bali ni makubaliano (mkataba). Lakini upendo ni wa lazima kwa kudumisha ndoa. Ukiisha upendo mkataba unakuwa hatarini kuvujwa na kuisitisha ndoa yenyewe.
   
 4. m

  mpangwa1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 5. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ndoa ni upendo, kama sio upendo hiyo sio ndoa bali ni ndoana.
   
 6. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 561
  Trophy Points: 280
  :confused:  Sielewi kabisa huu mjadala; kwanini huyo aliyetoa hiyo mada hakuweka vigezo vya kwanini ndoa sio upendo.

  Lakini gazeti la HabariLeo Jumapili lilitoa matokeo ya utafiti uliofanyika Australia. Moja ya matokeo ilikuwa hili: 13% ya ndoa zilizovunjika zilitokea baada ya mwanaume kuishiwa fedha ukilinganisha na 09% (tisa) zilizovunjika bila kigezo cha mshiko kuhusika. Aidha habari zingine zinadai huko Uingereza (England) mapenzi nje ya ndoa yameongezeka sana kipindi hiki cha mparaganyiko wa uchumi (economic crisis) kiasi kwamba ndoa nyingi zinavunjika.

  Sasa Pretty kwanini usiseme ndoa sio upendo. NDOA KUWA UPENDO ILIHAHUSU ZAIDI BIBI & BABU ZETU; sisi tunajali zaidi masilahi yetu binafsi basi.
   
 7. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Upendo ni muhimu but it aint everything u need kwenye ndoa... yataka uvumilivu, compromises kibao tu, maelewano, kusaidiana etc... its part of the package!
   
 8. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2009
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Inaweza kuwa ni upendo au siyo upendo, vyote vinawezekana. Still, hata inapokuwa ni upendo, haina guarantee sababu everything has got to expire! Kwa sisi bongo ambapo hatuna ndoa za mikataba, ndiyo maana kunakuwa na makaratasi yayanyotolewa na wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini yanayowabana wanandoa waendelee kuwa pamoja hata kama EXPIRY DATE ya penzi lao ikipita! I do not know kama ktu hiki hakina madhara, ila nadhani wana-Sosholojia na wana-Saikolojia inabidi walifanyie utafiti swala hili! Mi nakmbuka kama penzi la ndoa yangu na my wife wangu ilitaka-expire kipindi fulani yapata kama miaka 10 hivi imepita, ikabidi nichangamke sana. Nilifikria ni ktu gani anapenda sana halafu sku moja nikamsurprise nacho. Hiyo renewal ilikuwa ni ya milele, effect yake ni hadi leo!
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Jul 21, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nafikiri ndoa ni zaidi ya upendo... yaani si upendo peke yake unaowafanya watu wakaishi katika ndoa kuna chachu kibao ambazo lazima ziwepo ili ndoa idumu na iwe na amani na katu chachu hizo hazihusiani na upendo. Unaweza ukawa unampenda mtu kufa but kuna vitu anavyo ambavyo utajikuta unashindwa vumilia unaamua kubwaga manyanga.

  Ndio maana huwa tunashuhudia kuna mtu anamwacha mwenzi wake ikingali bado anampenda.
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hee,
  Hii ni mpya tena! Kumwacha mtu wakati bado unampenda?
  Ni shida gani ewe MwanajamiiOne zitakazokupelekea umwache mtu ungali bado unampenda?
   
 11. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Maana ya ndoa ni muungano wa watu wawili wa jinsi tofauti kwa makubaliano ya kuishi pamoja kama mke na mme.Labda mtoa mada anamaanisha Ndoa ya jinsi moja(mashoga).
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145

  Kweli tena PakaJimmy hujawahisikia?

  Unampenda kiukweli lakini mwenzio heshi vituko! Unakuta unampenda lakini yeye anakuwa ndivyo sivyo na pengine anatumia mapendo yako kukunyanyasa maana si anajua unampenda sana. Itafika siku unachoka inabidi tu umwache hata kama bado unampenda moyoni mwako, utaenda sikilizia maumivu mbele ya safari but unakuwa umeondokana na lile kero la kuudhiwa kila siku
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu BAK,
  Inatia moyo kuona kuwa wewe ni mwanaume unayeshangaa wanaume wenzio kufanya vitendo visivyokuwa na kiashiria chochote cha upendo.Nadhani tunapozungumzia suala la upendo tuliangalie kwenye ngazi zifuatazo:
  1. Upendo kabla ya kuwa na commitment yoyote - huu huwa mtamu, wenye kujenga matumaini kila siku, wenye kujenga matarajio ya furaha siku za usoni.Ni upendo huu unaofanya mwanamme na mwanamke kuombana na kuliliana wakubaliane kuishi pamoja milele! Hapo ndipo wapendanao huingia hatua nyingine - NDOA.Dr Remmy Ongala aliwahi kuimba " mwanzo wa penzi ni tamu kama chungwa, katikati kama ndimu na mwisho ni chungu kama shubiri!"
  2. Upendo baada ya commitment ya ndoa - hapa napo kuna stages
  • - wanandoa wameingia kwenye ndoa wakidhani ni raha mustarehe kumbe kuna majukumu na uwajibikaji;hii huanza kutia dosari kwenye ndoa na upendo huathirika.
   kuna struggle for power maana ndoa ina hierachy kama taasis nyingine yoyote; ndoa siyo ya mke na mume tu - inashirikisha watu wengine -ndugu na jamaa.Mapambano yaliyomo humo huweza kuwa makali au mepesi kutegemeana na influence ya mwenye kutaka kutawala mwenzie kuanza kujenga taratibu zake na sheria ( zisizo rasmi) kumwezesha kutawala nyumba yake.Taratibu/sheria hizi hazipokelewi kwa urahisi na yule anayetakiwa kuzipokea - hapo ndipo hutokea magomvi, chuki nakadhalika.
  Wakati haya yanatokea, polepole upendo huanza kuyeyuka kwa wote japo hautoweki wote.Kuna vipindi vya highs - upendo hurudi, kuna vya lows - hupungua n.k.Hii hujirudiarudia.

  Kuhusu kwanini wanawake hushindwa kuondoka hata kama wana uwezo wa kujimudu kimaisha - hili ni suala gumu sana kulitolea majibu.Nadhani inatokana na hizo highs and lows - kwamba wakati wa lows ndipo mtu ungetegemea mwanamke aondoke lakini hapo hapo hawezi kutoa uamuzi bila kushirikisha wengine na hata huyo mwanaume mnyanyasaji anashiriki kutafuta kumzuia mkewe asiondoke.Wakati wa highs basi watu hujikuta wakiendelea na maisha yao tena kama kawaida.Ni kama mchezo wa watoto wa Seesaw!

  Tusisahau pia wapo wanaume wanateseka kwenye ndoa zao.Na bado hawako tayari kuachana na wake zao.Labda tusikie kutoka kwa wachangiaji inakuwaje?
   
 14. H

  Haika JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani alimaanisha kuwa ndoa ni zaidi ya upendo.
  sio ndoa haiihitaji upendo, wala wanandoa hawatakiwi wawe na upendo.

  lakini kwanza kabla ya kuenda mbali, je upendo maana yake nini?

  kila mtu anaujua upendo kutokana na malezi yake, ndo maana hatuwezi kukubaliana na mwandishi huyo bila kujua upendo anaouzungumzia una maana gani.

  mimi kwa mawazo yangu, upendo ambao ni msingi wa ndoa ni ule wa kuingia kwa hiari kwenya maisha ambayo una mtu pembeni yake ambaye umekubali akugande kwa siku zote, yani umakubali kuwa bosi wake, mfanyakazi wake, mama yake, baba yake, banker wake, mwanasheria wake, daktari wake, mzazi mwenzake, shareholder mwenzake, mhubiri wake muumini wake etc kwa siku zako zote zilizobakia.

  mimi kwangu huu ndio upendo unaotakiwa, ila si hivyo tu kuna mambo mengine muhimu kama kutokujiachia sana huru kutaka kupata kila unachotaka.

  mapenzi ambayo yakitangulizwa mbele ya ndoa lazima uvunjike ni hisia za matamanio ili ukiwa nampenzi unajisikia vizuri, unaona raha ukijisikia vibaya unavunja ndoa (ukishatanguliza hayo lazima utakuwa na ndoa moja kila mwaka)
   
 15. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Ndoa ni upendo na Ndoa inaweza isiwe upendo. Inategemea ni upendo gani unazungumziwa. Kwani upendo umegawanyika katika nyanja mbalimbali. Kwahiyo ndio ni upendo au sio upendo vilevile

  Je hujawahi kuona upendo ukipungua?
   
 16. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Ndoa ni utaratibu wa kuweka bayana kuwa hawa watu wanaishi pamoja lakini sio necessarily kuwa ni upendo. Mnaweza mkapendana na mkaishi bila kuoana lakini pamoja kwa upendo zaidi kuliko wanandoa. Wanandoa wengi hawana upendo wa kweli.
   
 17. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kuna ndoa zinafungwa baada ya wazazi kumchagulia mtoto wao mchumba. Je hapo kuna upendo kati ya hao wawili? Kama hakuna upendo, je, hiyo ni ndoa au si ndoa? Naamini ni ndoa lakini haikufungwa kutokana na upendo wa wanandoa hata kama utashi wa kupokeana kati yao umekuwepo baada ya kuwa-influenced na wazazi. Kumbe ndoa hasa ni makubaliano/mkataba na si upendo, hata kama kimsingi kunahitajika upendo ili ndoa idumu.
   
 18. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nadhani ingekuwa vyema kama ungetuwekea content za hiyo makala humu. Inawezekana alikuwa ana point zake ambazo zinge justfy hicho kichwa cha habari, lakini kujadili kichwa cha habari tu tutakuwa tunadandia treni kwa mbele....LOL

  Lkini hata hivyo aina ya uandishi wetu nao unatia mashaka hasa magazeti ya udaku, mara nyingi vichwa vya habari haviendani na habari yenyewe.....
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  it si very true siku hizi kuna ndoa nyingi tu amabzao zimefungwa not because of love but because of something else..Wengine wanaona kwasababu ya vigezo bila kujali mapenzi ya dhati yaani bila kujali falling in love.
   
 20. Sydney

  Sydney Senior Member

  #20
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndoa ni upendo jamani, nani kasema sio upendo? sijui hicho kichwa cha habari ulichosoma wameadika wakiwa na maana gani, au mwandishi alifikiria nini. Lakini kwa mtazamo wangu naona ndoa ni upendo, labda kama mlilazimishwa kuoana!
   
Loading...