Ndoa: Nimevipata vyote isipokuwa hiki tu

Ndoa: Nimevipata vyote isipokuwa hiki tu

Usiwe weak kiasi hicho bwana,mke wako ameshaijua wweakness yako na ndio anaitumia, huyo mwanamke huwezi mbadilisha tabia yake mpaka aamue mwenyewe, najua itakuwa ngumu kwa sababu ulishajiwekea picha ambayo unapenda ndoa yako iwe vipi,Ila jaribu kumu ignore ingawa kwako itakuwa ngumu au jaribu kuchukulia hiyo ni mojawapo ya changamoto ya ndoa yako.Au yakikushinda mpeleke kwao kwa muda
 
Nastahili pumziko la milele! Ee Mungu nisaidie!

Usiwaze hvyoo mkuu endeleaa kumuombaaa munguuu atakusaidiaa
hapo hajaongea sahihi. kujirestisha kwasababu tu hakusikilizi, je angemkuta kitandani na mwanaume mwingine si ndio angejimaliza kabisa.? kwanini umekata tamaa kiasi hicho, umesalenda kwa adui mzee, mkeo ni mzuri tu ila kilichopo ndani yake ndicho kibaya na hicho ndicho unachotakiwa kupamgana nacho. angalia usijiue aisee.
 
wewe mtumish usiwe hopelesss! hapa duniani hukuzaliwa na mtu jarbu kufikir faida alizokupa MUNGU badala ya kuanza kulaumu kwani uyo mwanamke ni MUNGU wako? acha ujinga songa mbele, ukipata ugumu vunja ndoa.maisha ni zaid ya mwanamke. wasio nao hawaish??? MOI ameongoza nch hana mke sembuse ww? mtt wako ana thaman sana mthamini usimkatil kwa sababu ya mama yake.UBARIKIWE SANA
 
mkuu GAZANINGA Upo very right BOSS nimekutana nao wengi sana. na dawa nawaambiaga tusiyeyushane hebu fanya yako vigubuuuu? unaulza nin tatzo amna jibu?
 
Dah mambo ya ndoa magumu sana. Hii kitu iliwahi kunikuta nikiwa katika ujana. Nilikutana na binti wa Kikenya kwenye mishemishe za Duniani, akili na matendo yake nadhani ilikuwa ni sawa na unachokihadithia kutoka kwa mkeo. Nakumbuka nilijitahidi sana kuwa mtulivu na kujitahidi kumsikiliza na kumtendea "accordingly", lakini siku akinuna wala hutojua sababu. Utadhani ana mapepo, sura inakuwa kavuu; hapo hata umuigize "Charlie Chaplin" ni bure tu, huambulii cha tabasamu wala nini.

Hapo hata uongee zuri gani atakujibu neno moja, yakizidi mawili, makavu na yenye kutia simanzi! Ilifikia wakati hata kumpigia simu, kumjulia hali tu, unahisi atakuharibia siku endapo ukimkuta katika wakati wake hovyo.Na haya mambo kama kuna upendo wa dhati huwa yanakwenda kuharibu "psychology"; unaweza kupoteza hamu ya kuwa naye karibu, na inapolazimika kuwa naye karibu unakosa/kupoteza mvuto wa kufanya naye chochote, hata tunda la roho.

Ndicho kilichofika kwangu; kipindi ambacho ilitokea anashida na mimi ilikuwa ni "case" kubwa, kwa kuwa sikuwa tena na ile hamu ya kuwa naye karibu (maana alikuwa hatabiriki tena). Sasa kwetu sisi ilikuwa rahisi kwa kuwa hatukuwa katika ndoa. Hali ilivyofika hapo, nilikaa naye kitako nikamueleza ukweli; kwamba kwa kuwa nilikuwa sina uwezo wa "kucope" na mahitaji yake ya faragha kutokana na kuhisi kukosa amani ni vyema kila mmoja akawa "free" na maisha yake. Uzuri hawa majirani zetu ni "Wabepari", na sometimes wanaishi kiHollywood haikuwa shida sana kuhitimisha. Lakini nilijifunza jambo.

Wewe huyo ni mkeo ndugu, una kila sababu ya kupambana na hali hiyo. Ni lazima utengeneze "Happiness" kwenye familia yako kwa gharama yeyote ile. Inapobidi kukaa na mkeo kulizungumza ukae nae; usikome, onesha dhahiri unavyopata tabu juu ya hili tatizo kwa mkeo. Ikiwezekana tafuta hata udhaifu wake uutumie. Mfano, kama yuko "cautious" sana na kuyumba kwa uchumi ndani ya nyumba, onesha unayumba kiuchumi kwa ajili tu ya kulishughulikia tatizo hili; labda kwa kuwa unampeleka kwa "psychologist". Fanya jambo hadi ataelewa tu, na hatimaye utashinda kwa "TKO".
POLE MCHUNGAJI
 
Mfupa uliomshinda fisi wewe utauweza?hizi tabia zinazojitokeza katika ndoa ndio zilipelekea wenzetu wazungu kuwa na ndoa za mikataba.
 
Ndio mambo ya ndoa hayo, wengine watamani kuingia na wengine wanatamani kutoka.
 
Duh aisee pole sana ndugu, huo msalaba komaa nao tu no way!

Kama utaamua kuoa tena jitahidi uoe fresh woman, hawa wenye watoto mara nyingi huwa majanga
 
Ndugu, ili uwe na furaha maishani hakikisha unajipa mwenyewe furaha na kufurahi kwako hakutegemei furaha za wengine. Huyo mwanamke amrkuzalia mtoto mzuri, hiyo ni sababu mojawapo ya kumpenda. Anasimamia nyumba yako interms of usafi, chakula na matumizi. Si ajabu anakuombea japo hajui kujiexpress. Hebu kaa chini uandike list ndefu ya mazuri yake (pata picha asingekuwepo leo ni mambo gani yangekwama ) na uandike mapungufu yake. Halafu pima, kisha panda mlimani kwa maombi.

Baada ya hapo andika weaknesses zako na ujiombee pia. Shetani anakuwinda mtumishi na utapigwa ngwara sasa hivi. The grass is greener on the other side, and you will never notice her presence until she leaves you.
 
Usiwe weak kiasi hicho bwana,mke wako ameshaijua wweakness yako na ndio anaitumia, huyo mwanamke huwezi mbadilisha tabia yake mpaka aamue mwenyewe, najua itakuwa ngumu kwa sababu ulishajiwekea picha ambayo unapenda ndoa yako iwe vipi,Ila jaribu kumu ignore ingawa kwako itakuwa ngumu au jaribu kuchukulia hiyo ni mojawapo ya changamoto ya ndoa yako.Au yakikushinda mpeleke kwao kwa muda

Hawezi kumpeleka kwao coz ni mke ni mfanyakazi. Sema achukue njia yake(asimwache...ila aishi maisha kana kwamba yuko peke yake....aone inakuwa vp.).
 
Ulisha ambiwa mwanaume mwenzako alikimbia na kwenda kuoa mwanamke mwingine, huku dodosa kujua why mpaka jamaa amwache?

Majibu unayapata sasa.
 
Tatizo la kutokua na talaka ktk ndoa ndio hili sasa.
Au kuruhusiwa kuongeza mke mwingine.
Pole mtumshi hana pepo ni tabia mbaya tu aliyonayo.
Ungechunguza nini kilimfanya aachwe na mumewe wa kwanza.

Mtumishi wa Mungu anafikiria mpaka kujiua
Nastahili pumziko la milele! Ee Mungu nisaidie!
 
Nastahili pumziko la milele! Ee Mungu nisaidie!

Mtu wa MUNGU wacha mawazo ya kijinga yaani unaomba kufa sababu ya Mwanamke? Nyinyi sindio mnatuhubiria kuwa majaribu ni mtaji wakuongeza Imani,,,,!!! Umesema umemkuta namtoto,,,

, Ingawa cdhambi kufikia mtoto lkn nivyema km nyote mngekuwa na watt au ungeoa asie na mtt Maana yangu nikwamba nyote mngeanza hatua pamoja Samaki anakunjwa akiwa mBICHI,

,,ss ww unaenda kuchukua Mwanamke alieachika ulitegemea nini? MTU yyt aliekuwa na Ndoa kisha ikavunjika uctegemee huko mbele km atakuwa na mahusiano Imara Ushauri wangu ww umesema ni mtu mkubwa kanisani kwamaana hiyo huwezi kumwacha Endelea kumsihi MUNGU ili jambo jipya lizaliwe kwenye Moyo wake
 
Tatizo la kutokua na talaka ktk ndoa ndio hili sasa.
Au kuruhusiwa kuongeza mke mwingine.
Pole mtumshi hana pepo ni tabia mbaya tu aliyonayo.
Ungechunguza nini kilimfanya aachwe na mumewe wa kwanza.

Mtumishi wa Mungu anafikiria mpaka kujiua

Mkuu unadhani kuongeza mke ni Suluhisho? Hata ndoa za Kanisani zinavunjika2 cha muhimu ufate taratibu ambazo ni ngumu
 
Mapenzi ukiyaendekeza yatakutia wazimu.
Ongea nae na ukiweza wahusishe ndugu wa karibu
Kama bado atanuna basi mpige chini na endelea na maisha yako
 
.mi pia ningekaa kimya nione me mwisho wake eti unalia ndo Atazidisha manjonjo na vurugu_ tena wengine anajisifia kwa mashostito kuwa anakukomesha
Onesa ujasiri eti mzuri kwan unamla nyama?
Huenda keshajua unamuona mzur ndo maana anakuletea ukichaaa...
Amani na upendo no jambo jema hata kama yupo na sura kama gar LA majitaka
 
Preta asante sana. Kwakweli naona maisha yangu si ktu. Juhudi zangu za maisha naonahazinasupport yoyote. Inaiuma mno mpaka muda huu natokwa na machozi mno. Nimefunga sana kumuombea, namhrumia sana sana làkini yote hayà bila furaha na amanini bure.

punguza wema utakuponza wewe akinuna mwambie" najua sijakufanyia lolote baya wew wenda ukiniona ndo unanuna sasa wewe nenda nyumbani hali hii ikiisha nyumba ni yako"
 
Last edited by a moderator:
Naomba nikuulize

1. Hivi miezi yote 9 ambayo ujalala na mkeo, yeye anapata hiyo huduma wapi?

2. Hivi unajua historia yake ya nyuma vizuri. Nina maana mume wake wa kwanza alikuwa mtu ya aina gani mchungaji kama wewe? Msela? Au mpole?

3. Ushawahi kumuonesha kuwa unaweza kuishi nila yeye wakati wowote.

Mi nanachoona we umezidi kuwa laini laini wakati mkeo anataka njia mbadala. Jaribu kupiga kazi vizuri kitandani style zote, (sio za kilokole) then utaona matunda siku chache.

Inaonekana umpe furaha ya ndoa na ndio maana ameweza kukaa muda mrefu na ajaomba hata penzi kwako.

Jamani tuache kuwa walokole kwenye mapenzi
 
Back
Top Bottom