Ndoa: Nimevipata vyote isipokuwa hiki tu

Ndoa: Nimevipata vyote isipokuwa hiki tu

Majaribu2013

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
952
Reaction score
1,050
Wakati mwingine kujieleza mwenyewe upande mmoja bila upande mwingine kuwepo huwa kama kuna mambo yanafichwa na upande unaojeleza. Nimejitahidi sana niandike bila hasira yoyote.Nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa mtu mwenye hisia kali sana zàkutengeneza picha ya familia yangu kuanzia mke mpaka watoto.

Kikubwa kilichokuwa kikijirudia ni picha ya familia yenye furaha sana. Hali hii ilijengea moyo wa upole na upendo sana ambao nimekua nao mpaka sasa.Mwaka 2013 nilifanikiwa kuoa mwanamke wa kinyakyusa aliekulia Dar, mmi nikiwa Mnyamwezi wa Ziba, Nzega Tabora. Wakati namuoa mke wangu alikuwa na mtoto mmoja.

Kwa maelezo yake ni mtoto aliezaa alipokuwa ameolewa huko Dar, ila ndoa ilivunjika baada ya mume kuoà ke mwingne na kumnyanyasa sana mke wangu huyu.Tulifahamiana Dar katia mishemishe ya maisha akiwa mwajiriwa wa shirika fulani. Kwakweli kwa uzuri wa binti huyu na vileàlivyoonekana mpole sikujishauri sana kuingia naye kwenye mahusiano hatimaye tukafunga ndoa.

Maisha yakaendelea na hali ilianza kubadilika àlionekàna kama mtu mwenyejupe na jeusi. Namaanisha anaweza kuamka amenuna bila sababu. Lakini pamoja na haya yote upendo wake kwangu ulionekana waziwazi mpaka kwa wazazi wake. Mwazoni mwa mwaka 2014 aliifungua mtoto wakike.

Tuliendelea na maisha ya ndoakwa hali hiyo hiyo.Ulifika wakati nikajaribu kuzungumza naye juu ya hali hiyo nakutaka kujua kulikoni anakuwa hivyo alisema kwa mateso alopata kwa mume wa kwanza yalimfanya kuwà na moyo katili. Nilimuanzishia huduma ya maombezi na kumpeleka kwa wachungaji walimwombea na hatimaye mapepo yalitoka. Kwa kiasi fulani alibadilika na kuwa mtu mzuri.

Pamoja na hali hiyo ya mabadiliko hali ya kununa iliendelea kuwepo na mbaya zaidi ukiuliza tatizo ninini anakuàmbia kawaida tu. Au mimi nina makosa? Anakuambia hamna.Wadau, nimejitahidi sana kumsaidia kwa kila jambo abadilke lakini hakuna mafanikio mpaka mudà naandika amekuwa na tabia za ajabu sana.

1. Hawezi kutii sauti ya mume kwa jambo lolote jema au baya. Unaweza kutoka naye out ukajidai kumçare wala hawezikusuuport hata. Unawezakmshauri asifanye jambo fulani vile linahatarish maisha yake wala hatakuelewa.

2. Kununa ni jambola kawaida kwake, hata siku3 amenuna tu bila sababu.

3. Hana muda wa kuchochea amani na upendo wenye ndoa, muda wote ni kutafuta namna ya kuingusha ndoa tu.

Kwakweli najisikia vibaya sana katika maisha yangu. Nilitamani sana kutimiza zile hisia za familiayangu yenye furaha na amani lakini imekuwa kinyume.Najisikia sina nafasi yoyote kwenye fàmilia kwa vile hawezi kunisikiliza na kukubaliana hoja zangu. Yàani kila jema unàlomfanyia yeye àtatakaufanya kinyume tu ilimradi mkorofishane.

Umefika wakati sasa hata hamu ya tendo landoa imekwisha kabisa, siwezi kusisimka kufanya naye chochote japo ni mzuri sana tu. Mfano mpaka sasa nina miezi 9 tangu nishiriki naye. Mimi ni mtumishi mkubwa tu kanisani kwetu nameshimu sana Mungu. Kwa muda wote huu sifanyi ngono, unafikawakati mwili unawaka tamaa mno lakini Mungu hunijalia uimara tena.

Nimemuombea sana huyu mwanamke lakinihakuna matund yoyote sasa. Nahisi hii hali ya kukosa hamu ya kushiriki nayehuenda ikaniathiri zaidkwani hata kwa wanawake wengi saasa naiona hàli hii.Wadau nimevumilia sana, nimepata vyote vizuri kwenye ndoa yangu lakinihiki kimoja amani na furaha nimevikosa. Naona bora nisingevipata vyote hivi ila nikakipata hicho kimoja.

Bora ningeoa maskni ambaye ningefurahinaye. Siwezi kutoka nje ya ndoa wala kuwa namçhepuko kwa vile imani yangu kwa Mungu ni imara. Lakini pia nahisi nawachukia sana wanawake sasa.Naona kama wote wànaweza kunifanyia hivihivi.Inaniuma sana bora Mungu aitwae roho yangu nikapumzike.

Maana mateso haya nimakali mno. Naandika nikiwa nabubujikwa na machozi mengi sana, je Mungu alinijalia upole na upendo ili niteseke namna hii? Naumia sana. Sijajua msaada mzuri zaidini upi, nimeamua kueleza jaambo langu hili la sirini kwenu huenda akapatikana hata mmoja akanipa ushauri.Mara nyingi nimekuwanikipost humu mambo ya utani lakiini leo nakuja kwenuna uchungu sana neno lako kwangu ni faraja tosha maishani mwangu.

Asante kwa ushauri wako
 
Dah.......pole sana mchungaji.......ki ukweli kukosa furaha na amani ni kitu kibaya sana........kuna watu wana experience humu subiri watakushauri ushauri mzuri.......
Mimi ushauri wangu kwa hili hautakufaa......
Pole sana........
 
Dah.......pole sana mchungaji.......ki ukweli kukosa furaha na amani ni kitu kibaya sana........kuna watu wana experience humu subiri watakushauri ushauri mzuri.......
Mimi ushauri wangu kwa hili hautakufaa......
Pole sana........

Preta asante sana. Kwakweli naona maisha yangu si ktu. Juhudi zangu za maisha naonahazinasupport yoyote. Inaiuma mno mpaka muda huu natokwa na machozi mno. Nimefunga sana kumuombea, namhrumia sana sana làkini yote hayà bila furaha na amanini bure.
 
Last edited by a moderator:
Jifanyie tathmini we we mwenyewe kwanza. Unaweza kuona namna unavyoyatizama maisha ni sawa na kwa MTU mwingine kumbe binadam tunatofautiana sana.
Kuna wengine hawapendi attention sana, wanapenda kuwa ignored sometime. Hebu jaribu huo mtazamo
 
Jifanyie tathmini we we mwenyewe kwanza. Unaweza kuona namna unavyoyatizama maisha ni sawa na kwa MTU mwingine kumbe binadam tunatofautiana sana.
Kuna wengine hawapendi attention sana, wanapenda kuwa ignored sometime. Hebu jaribu huo mtazamo

Mkuu nimefanya sana haya ndipomaisha yabfamilia yalipoharibika kabsa
 
Wanasema ukiona unafanya jambo lile lile na unapata matokeo yale yale
basi jaribu kufanya kinyume chake

Kuna aina ya watu 'ukiwadekeza tu umewaharibu'
watazidi kukuletea utoto hadi ushangae

dawa yake ni wewe ku sit back and do nothing..

akinuna usimuulize kitu...shika remote control and ignore her...
 
Majaribu2013

Daah pole sana mtumishi, suala lako limenigusa sanaaaa mtumishi,kwa uzoefu wangu mdogo nilionao kwenyendoa inaonekana suala lako ni la kisaikolojia zaidi,naamini litapata utatuzi humu ndani,hapana kulia,mkabidhi Mungu fedheha zako.
 
Last edited by a moderator:
QMajaribu2013

Pole sana. Ni vema kufunga na kuomba.

Endelea kufanya maombi makali zaidi yakiambatana na kufunga na muda ukifika Mungu atatenda mpaka utafurahi mwenyewe. Uvumilivu ni muhimu kwani hali inaweza isibadilike kwa kipindi fulani au hata ikawa mbaya zaidi, ila wewe silaha yako ni kusimama katika maombi kama baba wa familia na

muda mwafaka ukifika Mungu atakurudishia mara mbili au zaidi.
chukua biblia yako, soma, tafakari mwombe Mungu, funga, ombea familia yako.

Biblia takupa faraja unayoihotaji, jikumbushe ahadi za Mungu kwa wale wamtumainiao, hizo ndizo zitakuwa faraja yako wakati ukisubiri Bwana kutenda. Utakuja kuniambia humu humu
 
Huyo kinuni kaona unamjali sana anataka akupande kichwani.
Huenda kumuignore huwezi basi fanya kitu.
Siku akinuna mwambie huwezi kuishi na mtu kisirani. kwa sababu yeye ndio kanuna, aondoke aende kokote akakae hadi atakapokua sawa.
Kuna wanawake wanajiendekeza vya kununa
 
Dah.......pole sana mchungaji.......ki ukweli kukosa furaha na amani ni kitu kibaya sana........kuna watu wana experience humu subiri watakushauri ushauri mzuri.......
Mimi ushauri wangu kwa hili hautakufaa......
Pole sana........

Duh umenichekesha hapo

Ila na mimi leo maji marefu haya, ngoja labda nimsaidie kuita wazoefu pengine wanaweza kusaidia kitu hapa gfsonwin, King'asti, Da Asia, NANDERA, nifah, Watu8 n.k
 
Pole sana mkuu, nachokiona hapa tatizo kuu ni wewe kuendelea kuishi kwenye ndoto zako zilizotimilifu kama ulivyokuwa ukifikiri awali kabla hujampata mwenza wako.
Hapa sina maana ya kubeza makabila ya watu wa Mbeya, la hasha ila mostly wazaliwa wa kyera na mbozi mioyo yao ndivyo ilivyo... ni migumu kama ngozi ya kobe na si wepesi wa kusamehe. Yawezekana katika kuishi kwenu hapo mwanzo kuna siku ulimuudhi kwahiyo usishangae pengine mwenzio bado hajalitoa kifuani mwake.
Cha msingi using'ang'ane kuishi kwenye ndoto ruhusu msawazo katika ubongo wako make ni mkeo huyo hakuna jinsi ya kuubadili ukweli. Pia jitahidi uelekeze upendo wako kwa mwanenu make hilo ni tunda na zawadi toka kwa Mungu na ni moja ya hitaji lako uliloombwa Bwana akujalize na uelewe kuwa hapa Duniani hutapewa vyote katika utimilifu kuna wenzako wamepewa wake wema ndoa yenye upendo lkn hawajabarikiwa kupata watoto.
Piga moyo konde mkuu na mche sana Mungu wako atakufunulia makuu usiyoyajua.
 
Kuomba Mungu akutwae si sahihi, nakuomba utubu tu na usiwaze hayo mambo ya kufa.

Jaribu linapomjia mtu huwa halina sura, taarifa wala specific approach. Kuna wenzio wengi ambao Mungu anajivunia walokuwa na jaribu kama lako lakini walipasua. Think twice maana wewe peke yako ndio utaenda kutoa hesabu, na pia mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa.

Mungu ni mtetezi wetu na ni msaada wetu pale tunapohisi hatuna nguvu tena za kuendelea mbele yeye huja na kututia nguvu. Kama kweli wewe ni mtumishi wa Mungu, naomba ujipange na umuombe Mungu akupe soln ya hili tatizo lako.

Kutafta utetezi au msaada kwa wanadamu haitakusaidia. Yesu pekee ndio analojibu lako. Nakusihi mtafte bila kuchoka. Yesu akasema namna hii haiwezekani, isipokuwa kwa kufunga na kuomba.

Pole sana, Yesu akutie nguvu.
 
Pole sana mtumishi naweza hisi maumivi uliyonayo ila kwanini ulioa mwanamke aliyezaa na mwanaume mwingine hao mara nyingi ni majeruhi hawafai kwa matumizi ya ndoa sina kitu naweza kukushauri kufanya ila naomba tu uvumilie hiyo project uliyochagua payback period ni kubwa sana na pengine hakuna vumilia.
 
Preta asante sana. Kwakweli naona maisha yangu si ktu. Juhudi zangu za maisha naonahazinasupport yoyote. Inaiuma mno mpaka muda huu natokwa na machozi mno. Nimefunga sana kumuombea, namhrumia sana sana làkini yote hayà bila furaha na amanini bure.
kuna kitu kimoja umekosea, ni kutojua vita. wewe unaonekana ni mtu wa kiroho, na unatakiwa kupigana vita vya kiroho. nitakusaiia kitu kimoja ambacho ukikifuata, utapata furaha ya milele.

kwanza kabisa, kila kabila lina pepo lake, na pepo mojawapo la wanawake wa kinyakyusa ni kiburi na kutosikiliza waume zao na uzinzi. naona hilo la uzinzi mkeo kapona lakini la kiburi lipo. nina experience na wanyakyusa, na nimeolea huko pia. usishindane nao, sio wao ni roho iliyoko ndani yao. ni kama roho ya wahehe tu kuwa na hasira, au ya wamachame kupenda hela kupita chochote. its a spirit ambayo unatakiwa kudeal nayo kiroho na si kimwili.

kuna kipindi ndoa yangu ilishawahi kuwa hivyo, kiburi sana na kununiana sana hivyohivyo, na ilitokea hivyo kwasababu alijua mimi ni mlokole siwezi kufanya chochote. ilitupelekea hata matumizi ya kutumia nguvu kidogo jambo lililonifanya nijute sana. ila nikapata suluhisho kwenye bible.

zipo roho zilizowekwa kabisa na shetani kazi yake ni kuvuruga ndoa, kukosesha ndoa amani na kuwagonganisha vichwa mtaumizana mioyo wee na shetani yupo pembeni anawacheka tu. dawa yake, unatakiwa kushambulia mashetani hayo kwa maombi, usifunge tu, tumia neno la Mungu kushambulia kuchinjachinja kwa Jina la Yesu na Damu ya Yesu, fanya hivyo kwa kutumia mistari ya kwenye Bible, mfano: imeandikwa tumepewa mamlaka kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui shetani wala hakuna kitakachotudhuru,....wewe sasa tamka kwa Jina la Yesu na kwa Damu ya Yesu ninakanyaga nguvu zote za giza, roho za kuvuruga ndoa kati yangu na mke wangu, roho ya kiburi kwa mke wangu etc...chinjachinja kwa mwezi mmoja hivi, hali hiyo itapotea na mkeo utafikiri amefufuka hutamwona tena na hali ile na yeye atajisikia mwepesi. ilinitokea hivyo, na kila ikitaka kurudia hata akinijibu vibaya huwa najua ni shetani tu anatafuta mimi nami nireact ili apate nafasi ya kuingilia, na akiingia huwa anavuruga kwa maangamizi makuba utakapokuja kuomba atakimbia lakini ameshasababisha madhara makuuubwa. hii ndio siri pekee ya vita vya rohoni.

zaidi ya yote, wamwabuduo Mungu imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. lazima Roho mtakatifu ahusike katika maisha yako, katika kuabudu kwako, katika kuomba kwako everything you do, Roho Mtakatifu atakuwepo kwako kama utashuka mbele za Mungu, kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na mwombe Mungu akujaze Roho wake, utabubujina na ukipata neema hiyo, chochote utakachoongea, utakachotamka, utakachofanya huwa kina upako wa nguvu za Mungu na kinatendeka. Roho mtakatifu ni moto ulao ambao mapepo ndani yako au kwa mkeo/ubavu wako yatayeyuka yenyewe. Yesu anabatiza kwa Roho mtakatifu hata leo hii, Yohana aliwaambia ,mimi nabatiza kwa maji lakini ajaye atawabatiza kwa Roho mtakatifu na kwa moto. Roho Mtakatifu ambaye ndiye Mungu mwenyewe ni moto ulao. ukivumilia, ukashuka mbele za Mungu, ukamtafuta Mungu kwa moyo wako wote ukawa na kiu ya maji yake ya uzima/Roho, utapata neema na vita vyako vyote vitakuwa vizuri sana na ndoa yako itakuwa bora.

Roho mtakatifu ni wa muhimu sana katika maombi, kwasababu yeye analia 'aba" na anaomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa ndani yetu ndio maana uombapo kwa Roho moyo wako huwa unapondeka to the maximum. Mungu akusaidie.
 
hiyo ni nafasi yako Mungu amekupa upambane kumshinda shetani ii akupandishe kwenye viwango vingine, kwasababu kama utashindwa kuishinda vita ya mashetani yanayoshambulia ndoa yako tu, je, Mungu atakupatia kampuni kubwa au hata utawala? si hata wachawi tu watakushinda? vita vinatufanya tunolewe na kumtafuta Mungu zaidi hadi tumwone.
 
Duh kuna wanawake ambao usipowajali kidg wanalaumu,ukiwapenda na kuwajali wanakuona boya flan hivi
BTW mwomba Mungu hachoki,muombee nahisi kuna mapepo yalibaki bado.
 
Back
Top Bottom