Ndoa: Nimevipata vyote isipokuwa hiki tu

Ndoa: Nimevipata vyote isipokuwa hiki tu

QMajaribu2013

Pole sana. Ni vema kufunga na kuomba.

Endelea kufanya maombi makali zaidi yakiambatana na kufunga na muda ukifika Mungu atatenda mpaka utafurahi mwenyewe. Uvumilivu ni muhimu kwani hali inaweza isibadilike kwa kipindi fulani au hata ikawa mbaya zaidi, ila wewe silaha yako ni kusimama katika maombi kama baba wa familia na

muda mwafaka ukifika Mungu atakurudishia mara mbili au zaidi.
chukua biblia yako, soma, tafakari mwombe Mungu, funga, ombea familia yako.

Biblia takupa faraja unayoihotaji, jikumbushe ahadi za Mungu kwa wale wamtumainiao, hizo ndizo zitakuwa faraja yako wakati ukisubiri Bwana kutenda. Utakuja kuniambia humu humu
Wewe mwenzio ana miezi 9 haja do biblia ataisoma vipi mpe msaada wa shida yake.
 
Kiukweli Kuna Vitu Vya Kuvumilia Mungu Aniepushe Na Mke Wa Aina Hyo, , , Miez 9 Daaah
 
kuna kitu kimoja umekosea, ni kutojua vita. wewe unaonekana ni mtu wa kiroho, na unatakiwa kupigana vita vya kiroho. nitakusaiia kitu kimoja ambacho ukikifuata, utapata furaha ya milele.

kwanza kabisa, kila kabila lina pepo lake, na pepo mojawapo la wanawake wa kinyakyusa ni kiburi na kutosikiliza waume zao na uzinzi. naona hilo la uzinzi mkeo kapona lakini la kiburi lipo. nina experience na wanyakyusa, na nimeolea huko pia. usishindane nao, sio wao ni roho iliyoko ndani yao. ni kama roho ya wahehe tu kuwa na hasira, au ya wamachame kupenda hela kupita chochote. its a spirit ambayo unatakiwa kudeal nayo kiroho na si kimwili.

kuna kipindi ndoa yangu ilishawahi kuwa hivyo, kiburi sana na kununiana sana hivyohivyo, na ilitokea hivyo kwasababu alijua mimi ni mlokole siwezi kufanya chochote. ilitupelekea hata matumizi ya kutumia nguvu kidogo jambo lililonifanya nijute sana. ila nikapata suluhisho kwenye bible.

zipo roho zilizowekwa kabisa na shetani kazi yake ni kuvuruga ndoa, kukosesha ndoa amani na kuwagonganisha vichwa mtaumizana mioyo wee na shetani yupo pembeni anawacheka tu. dawa yake, unatakiwa kushambulia mashetani hayo kwa maombi, usifunge tu, tumia neno la Mungu kushambulia kuchinjachinja kwa Jina la Yesu na Damu ya Yesu, fanya hivyo kwa kutumia mistari ya kwenye Bible, mfano: imeandikwa tumepewa mamlaka kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui shetani wala hakuna kitakachotudhuru,....wewe sasa tamka kwa Jina la Yesu na kwa Damu ya Yesu ninakanyaga nguvu zote za giza, roho za kuvuruga ndoa kati yangu na mke wangu, roho ya kiburi kwa mke wangu etc...chinjachinja kwa mwezi mmoja hivi, hali hiyo itapotea na mkeo utafikiri amefufuka hutamwona tena na hali ile na yeye atajisikia mwepesi. ilinitokea hivyo, na kila ikitaka kurudia hata akinijibu vibaya huwa najua ni shetani tu anatafuta mimi nami nireact ili apate nafasi ya kuingilia, na akiingia huwa anavuruga kwa maangamizi makuba utakapokuja kuomba atakimbia lakini ameshasababisha madhara makuuubwa. hii ndio siri pekee ya vita vya rohoni.

zaidi ya yote, wamwabuduo Mungu imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. lazima Roho mtakatifu ahusike katika maisha yako, katika kuabudu kwako, katika kuomba kwako everything you do, Roho Mtakatifu atakuwepo kwako kama utashuka mbele za Mungu, kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na mwombe Mungu akujaze Roho wake, utabubujina na ukipata neema hiyo, chochote utakachoongea, utakachotamka, utakachofanya huwa kina upako wa nguvu za Mungu na kinatendeka. Roho mtakatifu ni moto ulao ambao mapepo ndani yako au kwa mkeo/ubavu wako yatayeyuka yenyewe. Yesu anabatiza kwa Roho mtakatifu hata leo hii, Yohana aliwaambia ,mimi nabatiza kwa maji lakini ajaye atawabatiza kwa Roho mtakatifu na kwa moto. Roho Mtakatifu ambaye ndiye Mungu mwenyewe ni moto ulao. ukivumilia, ukashuka mbele za Mungu, ukamtafuta Mungu kwa moyo wako wote ukawa na kiu ya maji yake ya uzima/Roho, utapata neema na vita vyako vyote vitakuwa vizuri sana na ndoa yako itakuwa bora.

Roho mtakatifu ni wa muhimu sana katika maombi, kwasababu yeye analia 'aba" na anaomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa ndani yetu ndio maana uombapo kwa Roho moyo wako huwa unapondeka to the maximum. Mungu akusaidie.
What if he married without asking God...? Alipenda tu na akajitwalia mke ambaye Hakua chaguo LA Bwana
 
Mkuu pole sanaa! Kiumbe kinachoitwa mwanamke kiogope sanaa, Mwanamke akisema hapana utaomba mpaka Bwana Yesu atashuka lakini hawezi kubadilika. Ushauri wangu mzuri jitahidi kuachana na huyo mwanamke miezi tisa hamjafanya tendo la ndoa kuna ndoa kweli hapo. Na katika maisha kumbuka Mungu hakupi vyote atakupa pesa lakini akakunyima furaha. Akakupa umasikini lakini akakupa furaha hakuna budi kumshukuru. Ila ndugu yangu pole sanaa mimi yalinikuta miaka mitatu nyuma ila nashukuru kwasasa niko poa.
 
Ni ngumu kumeza lakini ni kweli, huyu ana X wake alikua anampenda lakini ikashindikana kuolewa, hivyo hana hisia na wewe, hata umpe au umfanyie nini hatoridhika, na atamfuata huyo x wake wakati uko naye, na atafanya hapo kwako kama kambi ila akitaka kufurahia maisha anamfuata x wake, mwambie ukweli hana, hana sababu ya kusononesha moyo wake amfuate x wake akuache na maisha yako, kama una watoto chukua na lea watoto wako.
 
ulikurupuka.kama unakosa miezi 9 bila nae haoni shida. Na kama alishaolewa ilitakiwa ujiulize sababu ya kuachana na mumewa awali. Fuatilia ujue ndoa ndoan Better be alone than bad company. Hata kama umeokaka ulioaje mwanamke alieachika one mistake one goal.chamsingi kama utashindwa mpe talaka .anza taratibu kutafuta mke mwingine Kwa uangalifu. Maisha mafupi uendelee kupata stress kwaajili yake upunguze siku za kushi .wanawake wengi oa mwingine uyo hakupendi.
 
mateso huwa furaha,furaha huwa mateso so usikate tamaa subili fungu lako li njiani.
 
Tujifunze kujitune...kuishi kadiri mazingira yanavuokuja...to live outside our expectations....
Mm binafsi kutaka furaha yangu ipatikane kupitia mtu niliekutana nae ukubwani hapana kwa kweli...niliushakataa milele...
Naheshima, napenda lkn sipendi kihisiahisia tu....INFATUATIONS.....
Furaha naipata kwenye kutimiza malengo yangu......kutimiza wajibu wangu kama baba kwa familia yangu na mke wangu...Nikijitahidi kusambaza furaha na upendo na mke asijali..its none of my business....and im cool kabisa yani..always happy..
Kuna vitu nimegundua ktk maisha..kuna baadhi ya mambo mtu awaye yote hawezi kukupa hata kama ni mke.....wewe unabaki wewe tu.....
We jamaa embu mind your own business....fanyakazi, timiza wajibu wako kula maisha...acha kulialia
Uko vizuri
 
  • Thanks
Reactions: Lob
Ndo walivyo wanyakyusa tululiopo mbeya tunawajua ila kuna namna yao ya kuwadhibiti muhimu usiwe mwoga
 
Ndg pole sana.
Funga siku tatu mwambie Mungu aamue kati yako na huyo mwanamke. Unapoingia mfungoni uhakikishe una furaha. Anza kwa kushukuru kisha hitaji. Mwambie Mungu atende si kama upendavyo bali yeye lipo jambo utaliona mapema. Usiiache imani yako.
 
Wanasema ukiona unafanya jambo lile lile na unapata matokeo yale yale
basi jaribu kufanya kinyume chake

Kuna aina ya watu 'ukiwadekeza tu umewaharibu'
watazidi kukuletea utoto hadi ushangae

dawa yake ni wewe ku sit back and do nothing..

akinuna usimuulize kitu...shika remote control and ignore her...
kweli kabisa
You said it all, na haya maisha ya Magu ni vyema mtu kutafuta amani ya moyo wako kwanza
unajikuta unachanganywa na maisha huku kuna mpenzi bado anakuchanganya?
Kwa hapo mimi hapana kabisa
 
Wanasema ukiona unafanya jambo lile lile na unapata matokeo yale yale
basi jaribu kufanya kinyume chake

Kuna aina ya watu 'ukiwadekeza tu umewaharibu'
watazidi kukuletea utoto hadi ushangae

dawa yake ni wewe ku sit back and do nothing..

akinuna usimuulize kitu...shika remote control and ignore her...
Very effective,,,nampaga wife mara moja moja anaishika adabu..vice versa also ..lol
 
Ulipaswa kujiuliza why aliachika ndio umuoe!!
Ulikurupuka kuoa mwanamke aliyeachwa mkuu na kamwe usirudie.
Huyo mkeo ni kisirani na haponi kwa maombi bali psychologist pekee kama kweli ndoa ilimuathiri lakini kama ni kisirani kaka hata kama aolewa na malaika atanuna tuu.
Fuata maandika kuwa Ishini na wanawake kwa akili sanaaa, so kaka mpuuze tuu wala usimuombe unyumba au jambo lolote huenda akajirudi Ila ukimjali sana atakusumbua huyo.
Sometimes tunapaswa kuwafunza kwa vitendo hawa watu.
Mwanamke halisi anyimi unyumba mume maana ndio kilichomleta hapo so unafikiri unakaa nae hapo kwa lipi? Vunja ndoa kaka maana haina haja kama mwaka mzima anakubania show.
Sio kila mnyama anafugika kaka wengine hawafugiki mrudishe kwao huyo.
 
Back
Top Bottom