Ndoa ni tamu sana

Ndoa ni tamu sana

Ndoa tamu mwanzoni tu baada ya kama 3-4 years MTU anakwambia anataman atoke ...kiukweli mm kama kuna mtihan nmebakiza n huu maana cjui utakuwaje....Hasa wanaume ndio wanaonekana kulia zaid sjui n kwann??
Miaka ya mwanzoni ndoa ni chungu maana mnakuwa bado hamjajuana vizuri..mkiweza kuvuka hiyo miaka mitatu au minne ndoa inakuwa nzuri. Kuna kipindi nilichukia ndoa maana vurugu zilikuwa nyingi mno, hata sasa sijui nilivukaje kile kipindi. Ila now am happy, mume wangu ni kila kitu kwangu...haondoki mtu hapa tutabanana hapa hapa!
 
Habari wanakijiji wenzangu, matumaini mko salama kabisa, bila kupoteza muda nielekee kwenye mada

Kumekuwa na wimbi la watu wengi hasa wanandoa kueleza negatives za ndoa kiasi kupelekea wengine kukata tamaa ama kuogopa lakini ngoja niwaelezeni kitu

Ndoa ni tamu sana hasa kama umepata mtu sahihi, kwanza mfanye mke au mume kuwa rafiki yao ambaye unaweza kushare mambo yote yawe ya Furaha au huzuni hii itamfanya mwenzako kuwa huru kushauri lolote kwa kauli nzuri, ikumbukwe hakuna binadamu mkamilifu hivyo mapungufu ya mwenzio chukulia kama kilema sio ndio fimbo ya kumchapia, unaweza kupata mwanamke mrembo lakn kitandani hajui chukulia hiyo ni changamoto na usimuumize kwa sababu ya udhaifu huo utafurahia ndoa yako.

Mwanamke akijua majukumu yake na akaweza kuyatimiza licha ya kuajiriwa, kuheshimiana licha ya kuwa na utofauti wa kipato, kuwe na mipaka mambo ya kazini yaishie kazini uwapo nyumbani lazima familia iwe imara na ndoa itafurahiwa na kila mmoja.

Makwazo hayakosekani, mkikaa pamoja na kuelezana kwa upendo mkiepuka maneno makali ya kuumiza lakini pia kuachilia kwa kusamehe yaliyopita, mtafurahia

Michepuko kwa wanaume husababishwa na mwanamke kutokaa kaa katika nafasi au tamaa tu, kama mwanamke atakaa katika nafasi yake, kupunguza gubu kuna nafasi kubwa kwa mwanaume kutulia au kupata mchepuko mstaarabu ambaye hatavuruga ndoa.

Mungu ni kiongozi mkuu wa ndoa ukiambatana naye katika kila hatua lazima ufurahie ndoa yako wengine watalalamika kuhusu ndoa zao wewe utakuwa unashangaa mambo ya naenda

Mwisho vijana msiogope ndoa, ni tamu sana kama utapata mtu sahihi kama nilivyoeleza hapo juu, usikubali kukatishwa tamaa kwa sababu et ndoa ya fulani inasumbua ukajua na yako itakuwa hivyo nooo, kila mtu amezaliwa kivyake ingekuwa hivyo tungeogopa kusoma eti kisa Fulani amefeli mtihani, Muwe na siku njema.
Mke Wangu alikuwa idara zingine zoote yuko vizuri lakini malaya ni hatari nilimshauri aache tabia hakuweza baadaye aliondoka mwenyewe kuendeleza fani yake nimemwona mahali juzi kanenepa mithili ya mbuyu.
 
Miaka ya mwanzoni ndoa ni chungu maana mnakuwa bado hamjajuana vizuri..mkiweza kuvuka hiyo miaka mitatu au minne ndoa inakuwa nzuri. Kuna kipindi nilichukia ndoa maana vurugu zilikuwa nyingi mno, hata sasa sijui nilivukaje kile kipindi. Ila now am happy, mume wangu ni kila kitu kwangu...haondoki mtu hapa tutabanana hapa hapa!
Uko sahihi msome Tuckman anasema kitu kama hiki
 
Mnao
Ukijitahid kumfanya mwenza wako rafiki yako michepuko watakaa mbali na mumeo maana muda wote atataka muongozane na muwe pamoja popote
Mnaongozana kwa njia ya simu hali mwenzio yupo kwenye kifua cha mkeo hata kuhema hawezi duh maisha haya
 
Mke Wangu alikuwa idara zingine zoote yuko vizuri lakini malaya ni hatari nilimshauri aache tabia hakuweza baadaye aliondoka mwenyewe kuendeleza fani yake nimemwona mahali juzi kanenepa mithili ya mbuyu.


nimecheka sana jman bas jua hakuwa akikufaa si umeona kachana mkuu!ukute hukuwa ukimridhisha
 
Back
Top Bottom