Ndoa ni tamu sana

Aiseee mkuuu ukweli utabaki KUA pale ,,Ndoa nitamuuuu sanaaaaa yaaaan nitamu mnooooooi.


Wanaolalamikia ndoa ,ujue kuna mambo wanayafanya ambayo hata Minh hayapendi....

Ndoa aliianzisha Mungu ...Mungu haanzishigi kitu kibaya ktk maisha yetu maana ANATUPENDA KUPITILIZAAA.
Hakika ni watu wachache wasioelewa wanajaribu kupotosha ila kiukweli ndoa ni tamu hasa ile ambayo unaishi maisha yako si ya kushindana na wengine, wala si ndoa ya maonyesho ina utamu wake
 
Hakika ni watu wachache wasioelewa wanajaribu kupotosha ila kiukweli ndoa ni tamu hasa ile ambayo unaishi maisha yako si ya kushindana na wengine, wala si ndoa ya maonyesho ina utamu wake
Kabisaaa....ukiona MTU anakuambia "" Ndoa mbaya ,,nataman nitoke ,,oohhh ndoa nikama chooo ,ukiwa nje unataman uingie ukiwa NDANI unataman utoke ***

MTU wanamna hiyo msikilize alafuuu moyoni mfananishe na MTU aliyeshimdwa ....sio kitu Bali mpotezaji ,,alafu ukija kuangalia utagundua Anamatatizo chungu nzima ...


Ila ninachokiamin Mimi nakamwe hakitobadilika ,,Ndoa nitamu ,,Nitampenda mke Wangu , nitamheshimu ,,nitamjali ,nitamlea km mtoto kama ambavyo maandiko yameniitaji nimfanyie .
 
Ukijitahid kumfanya mwenza wako rafiki yako michepuko watakaa mbali na mumeo maana muda wote atataka muongozane na muwe pamoja popote
Matatizo yetu haya ya kiuchumi bakuli la nyama mnashare watu sita ugali mlima, baada ya watoto wawili una kukuta tumbo kule, unatupia madera, mkitoka mume anakwambia tangulia ninakuja. Kama ni restaurant atahakikisha umekula umemaliza wewe na wanao akija analipa bill mnarudi nyumbani.

Huwezi kulalamika hunitoi
 
Mwanaume ni mbaya sana katika ndoa hasa kila ikifika mwisho wa mwezi,atakamuliwa njee zikiisha ndo anarudi ndani anakuita baby, ovyooooooo,wanaume mungu anawaona,yaani mwanaume akishapata hela anawaza kuchepuka tu!!!!
 
Sante kwa kututia moyo..! Ingekuwa ni possibly kuingia mwenyewe ningeoa leo ila sasa namuoa nani hapo sasa duuh bora nikae tuu kwanza.
Mtoa hoja Mungu wetu si wa michanganyo. Kama mtu amekuwa mwaminifu kwa Mungu hilo suala la mchepuko mstarabu halipo, huo ni uzinzi tu kama ilivyo kahaba/mzinzi yeyote hakuna cha ustarabu, atendaye dhambi ni wa ibilisi
Habari wanakijiji wenzangu, matumaini mko salama kabisa, bila kupoteza muda nielekee kwenye mada

Kumekuwa na wimbi la watu wengi hasa wanandoa kueleza negatives za ndoa kiasi kupelekea wengine kukata tamaa ama kuogopa lakini ngoja niwaelezeni kitu

Ndoa ni tamu sana hasa kama umepata mtu sahihi, kwanza mfanye mke au mume kuwa rafiki yao ambaye unaweza kushare mambo yote yawe ya Furaha au huzuni hii itamfanya mwenzako kuwa huru kushauri lolote kwa kauli nzuri, ikumbukwe hakuna binadamu mkamilifu hivyo mapungufu ya mwenzio chukulia kama kilema sio ndio fimbo ya kumchapia, unaweza kupata mwanamke mrembo lakn kitandani hajui chukulia hiyo ni changamoto na usimuumize kwa sababu ya udhaifu huo utafurahia ndoa yako.

Mwanamke akijua majukumu yake na akaweza kuyatimiza licha ya kuajiriwa, kuheshimiana licha ya kuwa na utofauti wa kipato, kuwe na mipaka mambo ya kazini yaishie kazini uwapo nyumbani lazima familia iwe imara na ndoa itafurahiwa na kila mmoja.

Makwazo hayakosekani, mkikaa pamoja na kuelezana kwa upendo mkiepuka maneno makali ya kuumiza lakini pia kuachilia kwa kusamehe yaliyopita, mtafurahia

Michepuko kwa wanaume husababishwa na mwanamke kutokaa kaa katika nafasi au tamaa tu, kama mwanamke atakaa katika nafasi yake, kupunguza gubu kuna nafasi kubwa kwa mwanaume kutulia au kupata mchepuko mstaarabu ambaye hatavuruga ndoa.

Mungu ni kiongozi mkuu wa ndoa ukiambatana naye katika kila hatua lazima ufurahie ndoa yako wengine watalalamika kuhusu ndoa zao wewe utakuwa unashangaa mambo ya naenda

Mwisho vijana msiogope ndoa, ni tamu sana kama utapata mtu sahihi kama nilivyoeleza hapo juu, usikubali kukatishwa tamaa kwa sababu et ndoa ya fulani inasumbua ukajua na yako itakuwa hivyo nooo, kila mtu amezaliwa kivyake ingekuwa hivyo tungeogopa kusoma eti kisa Fulani amefeli mtihani, Muwe na siku njema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom