Ndoa ni tamu sana

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
8,758
8,631
Habari wanakijiji wenzangu, matumaini mko salama kabisa, bila kupoteza muda nielekee kwenye mada

Kumekuwa na wimbi la watu wengi hasa wanandoa kueleza negatives za ndoa kiasi kupelekea wengine kukata tamaa ama kuogopa lakini ngoja niwaelezeni kitu

Ndoa ni tamu sana hasa kama umepata mtu sahihi, kwanza mfanye mke au mume kuwa rafiki yao ambaye unaweza kushare mambo yote yawe ya Furaha au huzuni hii itamfanya mwenzako kuwa huru kushauri lolote kwa kauli nzuri, ikumbukwe hakuna binadamu mkamilifu hivyo mapungufu ya mwenzio chukulia kama kilema sio ndio fimbo ya kumchapia, unaweza kupata mwanamke mrembo lakn kitandani hajui chukulia hiyo ni changamoto na usimuumize kwa sababu ya udhaifu huo utafurahia ndoa yako.

Mwanamke akijua majukumu yake na akaweza kuyatimiza licha ya kuajiriwa, kuheshimiana licha ya kuwa na utofauti wa kipato, kuwe na mipaka mambo ya kazini yaishie kazini uwapo nyumbani lazima familia iwe imara na ndoa itafurahiwa na kila mmoja.

Makwazo hayakosekani, mkikaa pamoja na kuelezana kwa upendo mkiepuka maneno makali ya kuumiza lakini pia kuachilia kwa kusamehe yaliyopita, mtafurahia

Michepuko kwa wanaume husababishwa na mwanamke kutokaa kaa katika nafasi au tamaa tu, kama mwanamke atakaa katika nafasi yake, kupunguza gubu kuna nafasi kubwa kwa mwanaume kutulia au kupata mchepuko mstaarabu ambaye hatavuruga ndoa.

Mungu ni kiongozi mkuu wa ndoa ukiambatana naye katika kila hatua lazima ufurahie ndoa yako wengine watalalamika kuhusu ndoa zao wewe utakuwa unashangaa mambo ya naenda

Mwisho vijana msiogope ndoa, ni tamu sana kama utapata mtu sahihi kama nilivyoeleza hapo juu, usikubali kukatishwa tamaa kwa sababu et ndoa ya fulani inasumbua ukajua na yako itakuwa hivyo nooo, kila mtu amezaliwa kivyake ingekuwa hivyo tungeogopa kusoma eti kisa Fulani amefeli mtihani, Muwe na siku njema.
 
Sante kwa kututia moyo..! Ingekuwa ni possibly kuingia mwenyewe ningeoa leo ila sasa namuoa nani hapo sasa duuh bora nikae tuu kwanza.
 
Wanawake mbona wako wengi? Takwimu zinaonyesha wanawake ni wengi kuliko wanaume unakosaje hapo? Tafuta wa vigezo vyako kulingana na uwezo wako
 
Unaposhauri mtu achukulie udhaifu wa mwenzie kama ni kilema unapotosha. Mfano kutokuwa mjuz kitandan utachukuliaje kama n kilema?
 
Sio priority yake kuna vitu vinampa Furaha zaidi ya hiyo kitandani hivyo kama unataka ajue hayo muelekeze don't acuse her
 
Mchepuko ni gharama na kama mwanaume hayuko makini anakupumbuka kujenga kwa hela ya pensheni au asijenge nyumba kabisa.
Ukijitahid kumfanya mwenza wako rafiki yako michepuko watakaa mbali na mumeo maana muda wote atataka muongozane na muwe pamoja popote
 
Asante ndoa ina raha jamani haswa kama kuna upendo na kuvumilia. Hata kama ikitokea mmepishana sio kukalipiana au kotoleana maneno machafu.
Kabisa maneno makali yanauma sana, kwa mfano mumeo anamaumbile madogo ukamsema kwa kutumia udhaifu huo unatengeneza ufa ndani ya moyo wake tujitahidi kutumia Lugha nyepesi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom