Ndoa ni tamu sana

Ndoa ni tamu sana

Waooh kwa mara ya kwanza sijui mara chache watu kusifia ndoa. Safi sana mi sijajuta na sitaki kujuta kuolewa am happy kuwa na familia. Sasa na ww mtoa mada umeharibu pale uliposema "mchepuko mstaarabu" hakuna mchepuko mstaarabu kama angekua mstaarabu asingeingilia ndoa ya mtu. Kwani wanaume hamuwezi kukaa bila mchepuko but nadhani wapo wastaarabu japo hawawezi kusema mbele ya watu kuwa hawachepuki.
Hongera sana, hilo la mchepuko mstaraabu inajulikana wazi kuwa mwanaume wa kiafrika asili yake wanawake wengi akiweza kuwa na mmoja tunapiga makofi, akiwa na mchepuko basi apatikane huyo mchepuko mstaraabu ambaye hatavuruga syatem ya familia
 
Kwa kweli ndoa tamu sana hasa ya kikristo ambayo haina uwezekano wa kuachana hivyo kusaidia kila mmoja kuiboresha maana hamna jinsi nyingine hasa kama wote wameokoka.
 
Asante kwa positive hii kuhusu ndoa...

Hapo kwenye kumpata mtu sahihi tumruhusu Mungu ahusike
 
Habari wanakijiji wenzangu, matumaini mko salama kabisa, bila kupoteza muda nielekee kwenye mada

Kumekuwa na wimbi la watu wengi hasa wanandoa kueleza negatives za ndoa kiasi kupelekea wengine kukata tamaa ama kuogopa lakini ngoja niwaelezeni kitu

Ndoa ni tamu sana hasa kama umepata mtu sahihi, kwanza mfanye mke au mume kuwa rafiki yao ambaye unaweza kushare mambo yote yawe ya Furaha au huzuni hii itamfanya mwenzako kuwa huru kushauri lolote kwa kauli nzuri, ikumbukwe hakuna binadamu mkamilifu hivyo mapungufu ya mwenzio chukulia kama kilema sio ndio fimbo ya kumchapia, unaweza kupata mwanamke mrembo lakn kitandani hajui chukulia hiyo ni changamoto na usimuumize kwa sababu ya udhaifu huo utafurahia ndoa yako.

Mwanamke akijua majukumu yake na akaweza kuyatimiza licha ya kuajiriwa, kuheshimiana licha ya kuwa na utofauti wa kipato, kuwe na mipaka mambo ya kazini yaishie kazini uwapo nyumbani lazima familia iwe imara na ndoa itafurahiwa na kila mmoja.

Makwazo hayakosekani, mkikaa pamoja na kuelezana kwa upendo mkiepuka maneno makali ya kuumiza lakini pia kuachilia kwa kusamehe yaliyopita, mtafurahia

Michepuko kwa wanaume husababishwa na mwanamke kutokaa kaa katika nafasi au tamaa tu, kama mwanamke atakaa katika nafasi yake, kupunguza gubu kuna nafasi kubwa kwa mwanaume kutulia au kupata mchepuko mstaarabu ambaye hatavuruga ndoa.

Mungu ni kiongozi mkuu wa ndoa ukiambatana naye katika kila hatua lazima ufurahie ndoa yako wengine watalalamika kuhusu ndoa zao wewe utakuwa unashangaa mambo ya naenda

Mwisho vijana msiogope ndoa, ni tamu sana kama utapata mtu sahihi kama nilivyoeleza hapo juu, usikubali kukatishwa tamaa kwa sababu et ndoa ya fulani inasumbua ukajua na yako itakuwa hivyo nooo, kila mtu amezaliwa kivyake ingekuwa hivyo tungeogopa kusoma eti kisa Fulani amefeli mtihani, Muwe na siku njema.
Well Said
 
Hao wanaosema wanatamani kutoka waongo tu wanaishia kusema ila hawatoki, lakini pia mkuu mtu akishindwa biashara ukaenda kumuomba ushauri unafikiri atakuambia kuwa biashara inafaida?
Sure waongo sana. Wanatamani kutoka si watoke tuone? Ndo ni kuvumiliana kuna ups and downs ila yote ni maisha. Huko nje napo hapakamatiki watu wana haha
 
Kwa kweli ndoa tamu sana hasa ya kikristo ambayo haina uwezekano wa kuachana hivyo kusaidia kila mmoja kuiboresha maana hamna jinsi nyingine hasa kama wote wameokoka.
Ni tamu Sana
 
Back
Top Bottom