Ndoa inaelekea kunishinda

Ndoa inaelekea kunishinda

Ushauri wenu jamani mimi nimeolewa nipo kwenye ndoa hatujamaliza hata mwaka Ila kinachoniumiza mme Wangu ananisaliti, nimemkuta anamiliki simu ya Siri pamoja na line alikuwa kaficha kabatini baada ya kugombana naye akakubali kuwa ana mchepuko akampigia akaweka loud nikawa nawasikia akamuomba samahani kwa kumchezea akamwambia Mimi nimeoa, nina mke nmeona siyo vizuri kumsaliti mke wangu dada akalalamika we badae akakubali kumblock kidogo nikapata amani.

Baada ya hapo hiyo simu ya Siri akaweka mezani akatoka zake Ila kilichoniumiza zaidi baada ya lisaa zilikuwa zinaingia text kutoka no. tofauti tofauti 2 baada ya kuchart nao kumbe nao ni michepuko yake tena jumla nimemfuma na wanawake 3 kwa wakati mmoja.

Msamaha kaniomba Ila nashindwa kumsamehe, naumia sana Bora ningemkamata hata na mmoja nisingeumia sana Ila wa 3 ukitegemea ndoa haina hata mwaka nawaza sijui kalogwa, natamani nimshirikishe hata mchungaji wetu Ila napata wakati mgumu naona ni vitu vya aibu hata kushirikisha watu wetu wa karibu. Natamani niondoke Ila kinachonipa wakati mgumu tayari Mimi ni mjamzito yaani nawaza ingekuwa siyo hii mimba ningeachana nae ananifanya Hadi nakata tamaa na mimba niliyonayo kitu ambacho ni dhambi, Naombeni mnishauri nifanyaje nahisi kuchanganyikiwa nakosa maamuzi presha imeshuka naona Kama dunia imeniangukia kweli ndoa ni ngumu sana duh! Mungu anitie tu nguvu.
Inaonekana umeolewa ukiwa bado mtoto..pole, ndoa ndoano. Ushanasa, vumilia maumivu.
 
Kiukweli ukipata mwanaume loyal kwako 100% nenda katoe sadaqa...

Ni ngumu sana kuwa faithful hasa kwa dunia hii ambapo kila angle ina vishawishi...tuna tabu sana vidume!
Hahaha!muhimu heshima kwa wenza wenu sio mpk mnakamatwa nasemaga sigusi simu ya mwanaume may be kama nshamchoka au aniruhusu!!!
 
Mbona sioni kosa la huyo ndugu yetu. Amekuheshimu mno. Ongea nae vizuri kwa utulivu na utii. Huyo ametubu na hawezi kurudia. Nakusihi Tena ongea nae kwa upendo hawezi kurudia. My take: Hajatenda kosa😀😀
 
Kama Mungu mwenyewe alisema ndoa na iheshimiwe na watu wote, bhasi rudi tena magotini pake umwombe aitete na kuijenga ndoa yako upya.
Kwani peke yako kwa akili za kibinadamu huwezi mwache Mungu achukue nafasi
My dear piga goti mwombe Mungu uone atakavyo kushangaza
Vita si vyetu bali ni vyake(Mungu) mpe Mungu nafasi nae atakushangaza kwa namna ya a ajabu
 
Mmeo mbona mtakatifu sana,michepuko 3 tu atakuwa na matatizo huyo huku wengine tunakaribia kuanzisha timu ya mpira.
 
Achana nae,hapo sasa jipende wewe mwenyewe na kiumbe ulichobeba,yeye fanya kama haumji Mpikie ale

Jilinde
Kula
Vaa Vizuri
Pendeza,jipendezeshe
Usimuulize
Usimfuatilie
Fanya mambo yako

Hiyo tabia ya kuchepuka hawezi kiacha,na yule mchepuko wa mwanzo aliyempogia simu mbele yako ni gelesha tu hawajaachana.
Kabisa! dada usijipe matumaini yasio kuwepo eti ameshaachana nae hakuna kitu kama hicho,chukua huu ushauri wala usijipe presha.wataachana endapo mmeo atachoka yeye mwenyewe lakini si kwa sababu wewe umesema.
 
Dada mvumilie tu mumeo sisi wanaume ndio tulivyo unaweza kuwa hata na michepuko kumi lakini mke wako ndio kila kitu, huyo mwamba kitendo cha kupiga simu mbele yako na kumchana live huyo mchepuko kuwa ana wife, ni kitendo cha kishujaa sana na huyo mwamba bila shaka anakunda sema tu jitahidi kumuelimosha madhara ya kuwa na michepuko ataacha na kubadilika
 
Kuna mambo mengine yanaweza yasizungumzike hapa.

Mimi ningetafuta kuprove beyond no doubt kuwa ana michepuko mitatu. Kuna watu wanaoweza kucheza mchezo wa maneno ili kuharibu maisha ya watu wengine.

Dada yetu usifanye maamuzi ya pupa. Unaweza kujikuta unapoteza mahali ambapo hukuwa na sababu ya kupoteza.


Uwe makini sana na ushauri tunaokupatia hapa. Upime vizuri.

Yaruhusu macho yatazame miaka kumi au ishirini mbele unapoelekea kufanya uamuzi wako.


Barikiwa na Bwana.
 
kabisaa au anamheshimu mkewee!maana wengine ndo kama hao michepuko mi3 yotee na mkewe anajua na hapo ndo hatajali ataonesha live live sasa hivi
Nimecheka kwa sababu mchana kuna uzi fulani umewakebehi wacha Mungu...umesema huwaamini WANAOJIFANYA wacha Mungu ila hapa naona rafiki yangu Relief Mirzska unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa
 
ndoa sio ngumu best, unavyoichukulia ndo utapata shida

ndoa ni nzr sana maana mko wawili mnashirikishana maisha na kusaidiana

omba na zungumza na mwenzako mambo yatakaa sawa
Ndugu sio rahisi hivyo usiombe yakukute ndoa yenyewe miezi 6 bado upo wamoto moto hata hina haijatoka mikononi wee anapitia wakati mgumu sana huyo mwenzetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: amu
Si ndo hapo??? Muwaambie ukweli jamani mnatu confuse huku.. af kumliza liza mkeo kisa wanawake wa nje ambao ungeweza kuwa control wala hupati baraka..
Uzuri mlishakubali kuwa kumiliki mgegedo weye peke hilo halipo so wacha na sie tujitaidi kuwadhibiti hawa warembo wa nje walilete sekeseke kwa wife
 
Ndugu sio rahisi hivyo usiombe yakukute ndoa yenyewe miezi 6 bado upo wamoto moto hata hina haijatoka mikononi wee anapitia wakati mgumu sana huyo mwenzetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Naelewa anapitia wakati mgumu..ila asiaminishe watu kuwa ndoa ni ngumu. Itakuwa ngumu vile umeichukulia.

Don't take life too serious, hutaenjoy
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom