Ndoa inaelekea kunishinda

Ndoa inaelekea kunishinda

Baada ya hapo hiyo simu ya Siri akaweka mezani akatoka zake Ila kilichoniumiza zaidi baada ya lisaa zilikuwa zinaingia text kutoka no. tofauti tofauti 2 baada ya kuchart nao kumbe nao ni michepuko yake tena jumla nimemfuma na wanawake 3 kwa wakati mmoja.
Kuna utata mkubwa ktk hii nukuu
 
Na Mimi nawaza kitu Kama hicho niwe tu bize na maisha yangu na mwanangu aliye tumboni nafikiria kwanzia Leo nisishike simu yake Wala nisimfatilie akiamua kuchepuka achepuke maana nshaona nikijua naumia alafu ameshanikatisha tamaa coz ndokwanza tuna miezi 6 kwenye ndoa alafu namfuma na wanawake 3 Bora hata angekuwa mmoja ningesema labda kwakuwa na mimba ameona anitafutie msaidizi nafikiria hata siku akitaka nishiriki nae niwe tu Mimi natumia nae condom maisha yote kujiepusha na maradhi maana nimewasiliana na wadada wawili kati ya hao wanasema walikuwa hawatumii condom mmoja ndoanasubiri kazi ya upolisi hivyo alimforce wakapime ukimwi kuhofia asijepata maambukizi akakosa kazi, yani hata hajali afya yangu na mtoto wake mpaka Kuna wakati inanijia roho ya kishetani nawaza sijui nimchomee hata ndani jamani naumia Basi tu mpaka naona tena Kama huu ujauzito nlobeba ni mzigo kwangu maana mimba tu nayo inanitesa naumwa badala ya yeye kuwa faraja kwangu ndokawa Moto ananichoma
Pole sana, tuliza akili na kumwomba Mungu akufariji. Usifanye maamuzi yatakayokuumiza kipindi hiki cha ujauzito.

Pia unaweza kuongea na wazazi wake wakusaidie kuzungumza nae.
 
Sawa tutaacha, ila muwe mnawaambia kabisa wasiwe wanawatumia message mkirudi nyumbani no calls or text.. nyie mnawapa uhuuuru kama nini sijui
Kwa kweli vijana wanakosea sana. Sema nini?? Sometimes za mwizi arobaini tu.

Ila sometimes ukipata mtu muelewa inakuwa sawa kabisa
 
Si ndo hapo??? Muwaambie ukweli jamani mnatu confuse huku.. af kumliza liza mkeo kisa wanawake wa nje ambao ungeweza kuwa control wala hupati baraka..
I agree with you.

Baraka za mke zinaweza fanya ukafanikiwa sana. Aisee namshkuru Mungu mimi ninebarikiwa sana
 
"Love is a game for fools to play
And I ain't fooling again (fooling)
What a cruel thing (cruel thing)
To self-inflict that pain"

Ngoja niimbe zangu tu sina ushauri wowote zaidi ya kukusaidia kuharibu zaidi. Kwani unafikiri ataacha hiyo tabia? hiyo ndio tabia yake na itazidi baadae. Huwa tabia na makucha yanajitokezaga mapemaaa, kwahiyo kazi kwako kuzika au kusafirisha.
Mmmhhhhh wewe dada wewe duh
 
Una hofu na Mungu ukimpata mwanaume mwenye hofu na Mungu maisha yanasonga Sana'a!!!
Yaani aminini tu kwamba we are trying really hard.

Hususan sasa wengine kama mimi, changamoto ni nyingi sana. Maofisini, majiani huko wadada wanajilengesha yaani nyie acheni tu.

Tunayoyapitia kwa kweli mtuombee tu jamani
 
Ushauri wenu jamani mimi nimeolewa nipo kwenye ndoa hatujamaliza hata mwaka Ila kinachoniumiza mme Wangu ananisaliti, nimemkuta anamiliki simu ya Siri pamoja na line alikuwa kaficha kabatini baada ya kugombana naye akakubali kuwa ana mchepuko akampigia akaweka loud nikawa nawasikia akamuomba samahani kwa kumchezea akamwambia Mimi nimeoa, nina mke nmeona siyo vizuri kumsaliti mke wangu dada akalalamika we badae akakubali kumblock kidogo nikapata amani.

Baada ya hapo hiyo simu ya Siri akaweka mezani akatoka zake Ila kilichoniumiza zaidi baada ya lisaa zilikuwa zinaingia text kutoka no. tofauti tofauti 2 baada ya kuchart nao kumbe nao ni michepuko yake tena jumla nimemfuma na wanawake 3 kwa wakati mmoja.

Msamaha kaniomba Ila nashindwa kumsamehe, naumia sana Bora ningemkamata hata na mmoja nisingeumia sana Ila wa 3 ukitegemea ndoa haina hata mwaka nawaza sijui kalogwa, natamani nimshirikishe hata mchungaji wetu Ila napata wakati mgumu naona ni vitu vya aibu hata kushirikisha watu wetu wa karibu. Natamani niondoke Ila kinachonipa wakati mgumu tayari Mimi ni mjamzito yaani nawaza ingekuwa siyo hii mimba ningeachana nae ananifanya Hadi nakata tamaa na mimba niliyonayo kitu ambacho ni dhambi, Naombeni mnishauri nifanyaje nahisi kuchanganyikiwa nakosa maamuzi presha imeshuka naona Kama dunia imeniangukia kweli ndoa ni ngumu sana duh! Mungu anitie tu nguvu.
Yatapita tu hayo, vumilia..
 
Mmh wewe ndio kivuruge. Mwisho wa siku wenzio wakianza kupata magonjwa nyemelezi kinga zipo chini wewe uko zako pembeni unawacheka. Kucheat ndan ya ndoa ya miezi 6 haimpi credibility mwanaume aliye serious na ndoa, NEVER.

Kwanini uoe na huwezi tulia na mwanamke mmoja. Kuna bahat mbaya sawa lakini ndoa bado changa una wanawake watatu nje tayari
If you don't know you don't know
 
Mmmhhhhh wewe dada wewe duh
Ni kumwambia ukweli tu hamna kumung'unyamung'unya na kumdanganya. Yeye aliziona hizo tabia na kufungua uzi kabisa kuwa jamaa anachiti mpaka analeta ndani. Sasa akaamua kuingia humo. Raha ya ngoma uingie ucheze!. Love is a game, kaamua kuingia kwenye game acheze tu mpaka dakika ya 90 "No retreat No Surrender" . Wasitese kiumbe cha watu tu kisicho na hatia. Man Ho huwa hawaachi, wanapumzikaga tu kitambo kisha wanaanza tena.
 
Tulia ndugu.
Acha hasira, acha papara.
Ndoa sasa hapo ndio imeanza rasmi, pale mwanzoni mlikuwa mnajidanganya kwenye kivuli cha unafiki tu.
Simama pamoja na muwe wako, linda ndoa yako, usimuache kamwe mumeo, mpende zaidi ya mwanzo. Pambana kadri unavyoweza kuitimua hiyo michepuko lakini kamwe usimuache mumeo.

Kama hujui tu, hiyo tabia ya kuchepuka mumeo hakuanza leo wala jana, wewe umeijua leo, lakini mumeo amekuwa nayo hata kabla hajafunga ndoa na wewe, katikati ya yote hayo bado alikuona wewe ndio best girl wa kuolewa naye, hivyo wewe ni mshindi kwa 100%.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom