Ndoa imenizawadia kiharusi

Upo sahihi.
Lakini sio wewe muhuni huna hofu ya mungu utafute mke mwenye hofu ya Mungu, ni kwenda kumtesa tu dada wa watu. Hofu ya Mungu muwe nayo wote wawili ndo mambo yataenda vizuri.
Ndege wenye rangi moja huruka pamoja, kwa maana huwezi ukawa unatafuta kitu wewe usiekiishi, ukitafuta anae mcha Mungu ni lazima utakua na hizo chembechembe ,wahuni hawatakagi mambo mengi wao hawanaga vigezo vingi
 
Hayajakukuta! Sio kila changamoto inavumilika vema kuinuasuru afya yako,hao wanao wataishi hata usipokuwepo. Tena wanaweza kuishi vzr zaidi ya ulivyokuwepo wewe! Wanaume tujifunze kujijali kibinafsi Kwa sababu Dunia haiko upande wetu
 
Type hizi dunia hii wapo wachache sana, kizazi cha wavumilivu hakipo. Wenyewe wamekalili kwamba mwanaume akipata hela anaenda kuoa mwengine kwa nilio washuhudia wengi huamua kuoa wanawake walio wavumilia. Nakumbuka wakati mimi na pigwa kibuti nina mwanangu alikuwa kwenye msoto kuliko mimi, ila still demu wake alikuwa anasimamia show,sasa hivi yule demu anakula mazuri ya nchi.
 
Pole sana Bro.

Ni makosa makubwa ulifanya kuwa humble kisa ndoa au Mwanamke mpumbavu. Au kisa watoto.

Wengi wanaotumia mbinu hii walipata matatizo na majanga makubwa kufikia kufa vifo visivyo vyao.

Hii itakuwa Case study Kwa vijana wajifunze. Kwa mwanaume heshima Yako ni muhimu kuliko Familia. Kwa sababu heshima yako ndio ulinzi wako na familia Yako.

Mungu akupe uponyaji urudi katika hali ya kawaida. Yale mambo ya demokrasia tunayoyapigania kwenye siasa huku Ndoani au kwenye familia hayatumiki. Ndoa au Familia Ili ikae sawa inapaswa kutumia mfumo wa Kifalme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…