Ndoa imenishinda wana Jf, nipeni mwongozo tafadhali.......!

Dah! Kamanda wewe bado sana hapo shukuru mungu, mimi wa kwangu ilikuwa unatoka huko umejipinda na hela umekopa umeenda kumnunulia yeye vijimayai na sheesh kebab ukifika unalembewa nazo za uso, halaf anakwambia "umeskia mie mturuki hata unaniletea mashish kebab"?. Ni kawaida sana mkuu.

Na kama uko huku shekoslovakia kikawaida wanakuruhusu kumsindikiza waifu wako labour kama unapenda, sasa Part 2 ni huko labour, ile akimaliza kujifungua tu mara unaweza ukamuona analembea matusi kwako bila sababu na kama pana ma pampers pembeni unalembwa nayo ya uso, unaambiwa ukayavae mwenyewe, halaf unaambiwa unagomewa kupewa kiduku. Lakini baada ya mwezi na nusu tu raha zinarudi pale pale.

Tuliza munkar kamanda ni kawaida sana na wewe bado una afazali sana, mpeleke waifu kazini bana na zingatia kwamba teso lolote la sasa hivi ujue haumtesi mama tu bali pia linampata na mwanao tumboni. Tafakari, chukua hatua.

Nimemaliza
 
Mwanasheria kloro,unafaa kwa ushauri nasaha pale martenity ward. Kuna vacancy, vipi utachangamkia?

wanalipa dolari? kama wanalipa kwa dollar niachane na haka ka duka ka vinyago, kamenikosesha wachumba kweli haka ka duka aisee
 
Naskia uporoto wamemuibia wallet mitaa ya ohio. hehehe halaf ankal uschakachue sredi jamaa ana hasira za mke wake atajeruhi yoyote anaemkalia mbele
Hahaha! Ankal nilimwabia Uporoto aache kununua wale watu pale Ohio sijui kama ameacha hiyo tabia.
 
pole cna rafiki ila tambua kwmb hizo ni pregnancy problems na kila mwanamke huwa na visa vyake tena ww unaafadhali mshukuru mungu kwa hilo
 
pole sana,mie mwenyewe niko njiani kumtaliki mke wangu lakini sio wkasababu hiyo yako wewe.Nalog off
 
ikiwa utaendelea na tabia kama hiyo,
tabia ya kununanuna wife wangu ooh tutatengana,
mimi utanishinda,kwa kweli utanishinda,
Fadhila utanishinda,kwa kweli utanishinda,
itakuwaje tulale pamoja tusiongee,
itakuwaje tujifunike shuka moja unanichunia,
Source:Wanyamwezi Family chini ya uongozi wa (Hayati)Baba J.
Nalog off
 
Dah! Kamanda wewe bado sana hapo shukuru mungu, mimi wa kwangu ilikuwa unatoka huko umejipinda na hela umekopa umeenda kumnunulia yeye vijimayai na sheesh kebab ukifika unalembewa nazo za uso, halaf anakwambia "umeskia mie mturuki hata unaniletea mashish kebab"?. Ni kawaida sana mkuu.

Na kama uko huku shekoslovakia kikawaida wanakuruhusu kumsindikiza waifu wako labour kama unapenda, sasa Part 2 ni huko labour, ile akimaliza kujifungua tu mara unaweza ukamuona analembea matusi kwako bila sababu na kama pana ma pampers pembeni unalembwa nayo ya uso, unaambiwa ukayavae mwenyewe, halaf unaambiwa unagomewa kupewa kiduku. Lakini baada ya mwezi na nusu tu raha zinarudi pale pale.

Tuliza munkar kamanda ni kawaida sana na wewe bado una afazali sana, mpeleke waifu kazini bana na zingatia kwamba teso lolote la sasa hivi ujue haumtesi mama tu bali pia linampata na mwanao tumboni. Tafakari, chukua hatua.

Nimemaliza
Asante sana kiongozi, umesomeka vema. Nitazingatia maoni yako na ya wadau wote hapo juu. Mungu awabariki sana tena sana.
 
ndo mambo ya ujauzito hayo! alafu kama anapenda kutembea na miguu ndo vizuri maana ni lazima akiwa ivyo afanye mazoezi sana! ila pia kuna ulakini hapo kwenye mshahara! kama vp kama ataendeleza iyo tabia yakununa bila 7bu tafuta nyumba ndogo uwe unapita jioni usuuze nafsi kabla ujarudi hm! alah! hajui mwanaume 1 anatakiwa aoe wanawake 5 ili wapungue uko mtaan, au cku moja mpeleke waliko machangudoa akajione mademu wakali zaidi yake lakini hawajaolewa!
 
Mimba noma, wakati waifu wangu ana mimba tulikuwa tunatoka wote Posta kwenda home (Kunduchi) mkifika njia panda ya Kawe anakwambia nataka chipsi za Namanga. Usiporudi kasheshe lake ni soo.
Take note: Unampeleka mpaka kituoni na unamwacha anagombania daladala, unaijua kweli adha ya daladala tena kwa mja mzito? Halafu unajisifu eti nimempeleka kituoni na nimemfata. We unaijua thamani ya kilichoko tumboni mwake? Shame on you! Hilo gari umemnunulia nani kama sio mkeo na mwanao?
Nakupa homework kwa hizi siku zilizobaki jipe muda wa kumpeleka mpaka ofisini na umfate jioni, pia mpe muda
wa kuongea naye kwa sababu unamkera na harufu ya pombe hata kama ni bia 1, na punguza kuwa net kama JF mida ambayo yeye yupo.
Wakati mwingine hasira zinawajia kwa sababu hatuonekani kuifeel ile torture wanayoipata wao, kwa hiyo ili akupende inabidi ujishughulishe hasa.
Last: kumbuka kumfanyia massage ya miguu daily, ili kupunguza miguu kuvimba, hii inasaidia hata kupunguza presha na anajifungua salama.
Jumapili njema.
 
Pole sana, Nimdagani tangu mfunge ndoa? kumbuka mwanamke anapokua na mimba anakua na mabadiliko mengi sana jaribu kumstahmilia mpaka ajifungue, usimchukulie na unajua mwanamke ni mtu wa kudekezwa sio mda mwingi uliobaki kwa yeye kujifungua na usimfanyie yeye fanya kwa ajili ya huyo kiumbe anaekuja azaliwe wakati wazazi wake wote wako pamoja mengine utajua baadae... jikaze mwanamme kustahmili hasa kwenye kipindi kigumu kama hiko usimuache atembee mbali sana kiasi hicho...
 
pole sana mkuu, hiyo nikawaida sana kwa mwanamke mwenye mimba nidalili tu zamimba na wala usichukie kabsa wala kufanya maamzi ya haraka, kuwa mvumilivu mwezi 1 simwingi hiyo khali itakuwa mwisho wake
 
Naona kuna watu wanasema mazoezi ni mazuri kwa wajawazito. Naomba niwaonye kuwa si kila zoezi ni sahihi. Kutembea 10 km per day naona kama ni too much kwa mimba ya miezi nane. Muwe waangalifu na msifanye mazoezi kiolela; tafuta ushauri wa doctor msije bebesha wake zenu vyuma eti wajifungue salama. Mimba zitaja toka ooh.

Maana najua hata kama mja mzito anafanya walking exercise kwa umri wa hiyo mimba the husband should be by her side (in case of anything?).

Kuna mmoja amesema kwa umri wa hiyo mimba hakuna cha mood swing; mood swing ni tofauti na kichefuchefu. Kichefu chefu ndo kinaisha baada ya miezi ya kwanza. Mood swing mpaka ujifungue. Na muhusila wala hajuhi analotenda.
 
Kiongozi si ulipiga bao mwenyewe? hizo ndo tabia za ujauzito. tena anakuheshimu sana maana hakuambii kuna wengine wanatimuliwa na wake zao vyumbani mwao kisa utasikia unanuka sitaki kusikia harufu yako! wengine hata sauti yako hataki kusikia unakaa mbali na yeye! vumilia akishajifungua tu utaona mabadiliko makubwa sana tuu
 
Kuna jamaa baada ya kuona hali kama hiyo iliyojitokeza kwa mkeo, alikuwa akisha mtwisha zigo la mimba anasepa kusoma, anarudi akishajifungua, unaonaje hiyo? Anatafuta hata kozi ya mwaka mmoja.
 
We ulidhani ndoa ni mchezo? Wazazi wako wamepitia hayo; wamepitia shida na raha hata ukapatikana wewe! Hacha kulia lia Mwanaume! Wewe ukilia na mke wako alie, uanaume wako uko wapiiii? Acha hizo bana!
 
Naona kuna watu wanasema mazoezi ni mazuri kwa wajawazito. Naomba niwaonye kuwa si kila zoezi ni sahihi. Kutembea 10 km per day naona kama ni too much kwa mimba ya miezi nane. Muwe waangalifu na msifanye mazoezi kiolela; tafuta ushauri wa doctor msije bebesha wake zenu vyuma eti wajifungue salama. Mimba zitaja toka ooh.

Maana najua hata kama mja mzito anafanya walking exercise kwa umri wa hiyo mimba the husband should be by her side (in case of anything?).

Kuna mmoja amesema kwa umri wa hiyo mimba hakuna cha mood swing; mood swing ni tofauti na kichefuchefu. Kichefu chefu ndo kinaisha baada ya miezi ya kwanza. Mood swing mpaka ujifungue. Na muhusila wala hajuhi analotenda.

Napenda kuongezea pia kwa wengine wachache kichefuchefu na kutapika kinaweza kuendelea hadi wakati wa kujifungua.
Pia kuna mood swings pia kuna mbaya zaidi ambayo ni pregnancy depression ,so wanaume jamani wapelekeni clinic wake zenu iki mjue mabadiliko yote na pia kusaidia kuelezea mambo mengine ambayo umeona kwa mwenzio na yeye hajayaeleza kwa doctor
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom