Ndoa imenishinda wana Jf, nipeni mwongozo tafadhali.......!

NGOSWE.120

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
219
233
Wana Jf,

Nina mke ambaye sasa ni mjamzito wa miezi 8 sasa. Kiukweli tabia yake imenishinda. Ni mtu wa kununa nuna muda wote, sijisikii furaha kuwa nae though ni mke wangu na niliapa kuwa ni yeye tu basi hadi kifo kitutenganishe.

Nimemsomesha na sasa ana kazi yake, mshahara wake siujui na wala sihoji anachofanyia, ndani kuna kila kitu, kazini nampeleka kwa usafiri hadi kituo cha basi (km 5 toka home hadi kituo cha basi).

Mimi nakunywa bia but 1 au2 tu, saa 12 au 1 jioni nipo home.

KISA: juzi jioni nimemuona ana mawazo mengi sana, nikamuuliza kwa upole nini tatizo bibie kasema mhmh maisha magumu. Hakutaka kuendelea kuongea na mimi. Jana nimempeleka kazini namsemesha lakini anaongea kama namlazimisha tu, kifupi hakupenda kuongea nami.

Jioni nimetoka kazini namfuata, ameshukia daladala kituo kingine tofauti na ameamua kutembea kwa mguu hadi home. Hajaongea nami hadi anaamka asubuhi.

Leo nimemuacha atembee kwa mguu kwenda huko kituoni (km 5 hadi kituoni). Nimechukia sana na namuona kero. Najuta kumuoa na nataka nimuache coz sioni kama nina tija naye.

Naombeni ushauri wenu wandugu.
 
Ingia google, soma tabia za wajawazito.
Ukiamuacha mie namuona na mimba yake napata faida
 
kaka, usijali kaka ni hormone fluctuation, labda kakuchukia wewe. Huwa inatokea wala usimuadhibu, hamaanishi chochote. Be patient
 
Kuwa mvumilivu kaka. Hiyo ni kawaida sana kwa wajawazito. Jitahidi kumuelewa
 
Chukua ushauri wa Gaijin hapo juu,wajawazito ndivyo walivyo,halafu we ulifikiri ndoa ni nyepesiee!Tulia na mke wako!
 
Acha kabisa mkuu kuogopa au kukereka tulia, hiyo ni home work yako usitake kuikimbia. Jitahidi kumuonyesha uko naye wakati wote huu wa uja uzito! miezi 8, bado mwezi tu utapumzika.
 
Wana Jf,

Nina mke ambaye sasa ni mjamzito wa miezi 8 sasa. Kiukweli tabia yake imenishinda. Ni mtu wa kununa nuna muda wote, sijisikii furaha kuwa nae though ni mke wangu na niliapa kuwa ni yeye tu basi hadi kifo kitutenganishe.

Nimemsomesha na sasa ana kazi yake, mshahara wake siujui na wala sihoji anachofanyia, ndani kuna kila kitu, kazini nampeleka kwa usafiri hadi kituo cha basi (km 5 toka home hadi kituo cha basi).

Mimi nakunywa bia but 1 au2 tu, saa 12 au 1 jioni nipo home.

KISA: juzi jioni nimemuona ana mawazo mengi sana, nikamuuliza kwa upole nini tatizo bibie kasema mhmh maisha magumu. Hakutaka kuendelea kuongea na mimi. Jana nimempeleka kazini namsemesha lakini anaongea kama namlazimisha tu, kifupi hakupenda kuongea nami.

Jioni nimetoka kazini namfuata, ameshukia daladala kituo kingine tofauti na ameamua kutembea kwa mguu hadi home. Hajaongea nami hadi anaamka asubuhi.

Leo nimemuacha atembee kwa mguu kwenda huko kituoni (km 5 hadi kituoni). Nimechukia sana na namuona kero. Najuta kumuoa na nataka nimuache coz sioni kama nina tija naye.

Naombeni ushauri wenu wandugu.

Ni ujauzito unamsumbua huyo bibie usimuache, angekuwa hakupendi asingekubebea ujauzito who are You?
 
Yaani kakesi ka ovyo hv tena na mjamzito ndo unakaleta hapa? Hujakuwa wewe! Halafu huna huruma! Unamwacha mkeo anawalk 5 km tena mjamzito? Shame on u! Umeoa unatakiwa umeze madhila yote na sio kulia lia ka mtoto hapa! 2mbavu![/QUOTE
Asante kwa maoni yako. Wewe ni mwalimu so unapofundisha darasani na mwanafunzi wako hayupo kupokea unachofundisha je unaweza kuendelea kufundisha darasani au utafanya nini?

Usiwe na hasira, ndio mja mzito sasa kwanini anune? nini amechukizwa? home nipo ful time au nianze kulala bar ndio atajua nampenda????
 
pole kaka ni visa vya muda tu hivyo vya kununa nuna. Akijaaliwa mwana itatulia.
Hapo kwenye kusomesha, kazi na mshahara mbona kama unasimanga?

Sio kuwa namsimanga ila kifupi nilikuwa najaribu kueleza ni jinsi gani namthamini na namjali ili kusiwe na mkakanganyiko kana kwamba hana kazi au namnyanyasa. Ni upendo niliokuwa nao kwake lakini naona inafikia hatua sasa kama najiumiza, I can't feel proud of her any more! yaani dah ! kifupi sioni faida ya ndoa hadi dk hii.
 
binadamu bwana.... Wakati anakupa raha, hukuja kuulizia tumpe zawadi gani sasa changes za pregnancy, tayari unakata rufaa
 
Wana Jf,

Nina mke ambaye sasa ni mjamzito wa miezi 8 sasa. Kiukweli tabia yake imenishinda. Ni mtu wa kununa nuna muda wote, sijisikii furaha kuwa nae though ni mke wangu na niliapa kuwa ni yeye tu basi hadi kifo kitutenganishe.

Nimemsomesha na sasa ana kazi yake, mshahara wake siujui na wala sihoji anachofanyia, ndani kuna kila kitu, kazini nampeleka kwa usafiri hadi kituo cha basi (km 5 toka home hadi kituo cha basi).

Mimi nakunywa bia but 1 au2 tu, saa 12 au 1 jioni nipo home.

KISA: juzi jioni nimemuona ana mawazo mengi sana, nikamuuliza kwa upole nini tatizo bibie kasema mhmh maisha magumu. Hakutaka kuendelea kuongea na mimi. Jana nimempeleka kazini namsemesha lakini anaongea kama namlazimisha tu, kifupi hakupenda kuongea nami.

Jioni nimetoka kazini namfuata, ameshukia daladala kituo kingine tofauti na ameamua kutembea kwa mguu hadi home. Hajaongea nami hadi anaamka asubuhi.

Leo nimemuacha atembee kwa mguu kwenda huko kituoni (km 5 hadi kituoni). Nimechukia sana na namuona kero. Najuta kumuoa na nataka nimuache coz sioni kama nina tija naye.

Naombeni ushauri wenu wandugu.

Welcome to the MEN club. Kwa ufupi hayo ni mambo ya kawaida kwa akina mama wenye hali kama hiyo. We vumilia kidogo kwani umebaki mwezi mmoja tu mambo yote hayo yatakuwa historia na mtaishia kukumbushana kwa vicheko. Kama bado mna mpango wa kuujaza ulimwengu basi "next time" anaweza kuja kivingine mpaka ukashangaa - huwa hawatabiriki. At least you know what to expect. Kuhusu yeye kudai maisha magumu mimi naona sawa tu - kutembea na mzigo alionao kwa miezi nane sasa sio mchezo ndugu yangu. Wataalam wanashauri wakina mama wafanye mazoezi wanapokuwa kwenye hali kama hii hivyo kutembea kusikupe pressure sana.
 
Ni wivu tu akijifungua atacha tu..Ndo kawaida ya akina mama wakiwa na mimba.Wanakuwa ta tabia tofauti tofauti lakini ataacha tu.Msamehe
 
Sio kuwa namsimanga ila kifupi nilikuwa najaribu kueleza ni jinsi gani namthamini na namjali ili kusiwe na mkakanganyiko kana kwamba hana kazi au namnyanyasa. Ni upendo niliokuwa nao kwake lakini naona inafikia hatua sasa kama najiumiza, I can't feel proud of her any more! yaani dah ! kifupi sioni faida ya ndoa hadi dk hii.

Wakati tunakula kiapo cha ndoa huwa tuna tamka maneno fulani halafu tunasema "Kwa Raha na Shida Mpaka Kifo Kitutenganishe". Wewe ulishapata ile raha ya kutafuta mtoto sasa ni wakati wa shida ya kumsubiri huyo mtoto halafu bado kuna shida nyingine kidogo ya kukesha mpaka huyo mtoto atakapojifunza kulala. Baada ya hapo raha as usual. Ila huwa kuna vishida vya hapa na pale along the way be prepared.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom