Ndoa imenishinda wana Jf, nipeni mwongozo tafadhali.......!

Nashukuru sana wana JF kwa ushauri wenu.

Kwa kweli nimefarijika sana kupata maoni yenu na kwa kweli nimejiona nipo na ndugu zangu ambao kwa kweli wanajua namna gani ya kujenga mahusiano na kuimarisha ndoa za watu kwa michango mbali mbali.

Narudia tena ndugu zangu asanteni sana tena sana.

Nimeyapokea yote na nimehaidi kurudisha moyo nyuma na kumpenda mke wangu kama mwanzo na kumpa stahili zote ili naye hata kama atakuwa amegundua kosa alilofanya basi ajirekebishe.

Jioni amerejea tayari yupo hapa home na nimemuomba tutoke amekubali so baadayeee nitamuuliza kiustarabu tu kuona kama kuna kitu amekwazika basi awe muwazi kwangu ili tumalize tofauti iliyojitokeza ili tuweze kumpokea vema huyo mtoto wetu kama mungu akitusaidia na hatimaye kujifungua salama.

ASANTENI SANA,

JF IDUMU MILELE!
 
Kaka umesomeka ngoja niwe mpole for time being ila zoezi la ku-shutle kwenda kazini atafanya hadi ajifungue ..... hilo nimesema sirudishi moyo nyuma. Nafanya hivyo ili at the end aweze ku-value thamani ya kumpeleka na kumrudisha ili asirudie tena upuuzi wake.

Jamani Ngoswe mbona unakasirika namna hiyo..,. kwanza pole kwa yanayokusibu. I wish kama ungeomba ushauri mapema wakati mimba ndo changa, sasa hivi umebakiza mkia tu (mwezi mmoja) ndo unachoka. Ndio maana wanaume huwa wanashauriwa sasa waende na wake zao clinic ili angalao wajue yanayowasibu wake zao pindi wanapokuwa wajawazito. Ni muhimu sana kujua mabadiliko mbalimbali yanayomtokea mama wakati wa ujauzito, wakati mwingine ni vema kujiunga na site kama Baby centre wote wawili ili kuwa familiar na maendeleo ya mtoto na mabadiliko ya mwili wa mama. Hii inasaidia sana, ingawa sasa sio kwamba wengine watumie ujauzito kama kigezo cha kudeka sana na kuumiza wenza wao, na isitoshe kila ujauzito una tabia zake.
 
kweli wewe ngoswe,uwe unapata muda wa kujisomea vitabu,hasa vya wajawazito kwa kesi yako na sio kukimbilia jf tu!mke haachwi ovyo namna hiyo!una miaka mingapi?
 
Ucwe mwepec kias hcho..mwanamke yoyote akiwa na mimba kuna mabadiliko yanatokea bla yeye kutaka...mchukulie kawaida sasa utaacha wangap?mana ukiacha c utakuja kuoa tena na utae muoa c atabeba naye mimba...ndoa ni uvumiliv kaka
 
Nashukuru sana wana JF kwa ushauri wenu.

Kwa kweli nimefarijika sana kupata maoni yenu na kwa kweli nimejiona nipo na ndugu zangu ambao kwa kweli wanajua namna gani ya kujenga mahusiano na kuimarisha ndoa za watu kwa michango mbali mbali.

Narudia tena ndugu zangu asanteni sana tena sana.

Nimeyapokea yote na nimehaidi kurudisha moyo nyuma na kumpenda mke wangu kama mwanzo na kumpa stahili zote ili naye hata kama atakuwa amegundua kosa alilofanya basi ajirekebishe.

Jioni amerejea tayari yupo hapa home na nimemuomba tutoke amekubali so baadayeee nitamuuliza kiustarabu tu kuona kama kuna kitu amekwazika basi awe muwazi kwangu ili tumalize tofauti iliyojitokeza ili tuweze kumpokea vema huyo mtoto wetu kama mungu akitusaidia na hatimaye kujifungua salama.

ASANTENI SANA,

JF IDUMU MILELE!


Nice one bro, kila la heri kwa ndoa na watoto wenye heri na nyie...
 
Usijali mkuu, akizaa ataacha hicho kisirani chake. Mimi wakati mamsapu wangu ana mimba kila ikifika wakati wa kulala nilikuwa sina raha maana nlikuwa naambiwa nanuka kikwapa, basi usiku nlikuwa nakesha kujipulizia pafyumu. Ajabu baada ya kujifungua tu, eti kile kikwapa chote kikapotea na sasa hivi hata nikaa siku tatu bila kuoga, wala hana shida ndo kwanza 'ananivutia' kwake.

Nikikumbushia vile vituko badala ya kucheka, eti ananuna------wanawake kwa kudeka!
 
Hili la kutembea kwa mguu inabidi tupate 'ushauri wa wataalamu'
isije kuwa ni mazoezi yanayofaa kwa mjamzito..
 
Mbu,

unajua kuna kitu kinaitwa kupokea, sasa mimi nimejitahidi kwa kila kitu ili yeye a-feel comfortable kuwa nami home muda wote.

Imagine-- mpango wa kando sina na wala sitegemei kufanya hivyo. Nikitoka job nipo home ful time, bia nakunywa home, Jamii Forum na-surf nikiwa home but inafikia hatua mtu unachokaa mkuu.

yaani haoni uwepo wangu karibu naye kama una manufaa au ku-value upendo wangu kwake, so hapo mimi nifanye nini sasa.

Kama kubeba mimba ndio kigezo mbona hata kichaa huwa anabeba na huwa anazaa au yeye ndio wa kwanza kubeba mimba? be realistic mkuu sio kupendelea upande mmoja kisa eti kabeba mimba!

hapa nahisi umeongopa! Soma Pm nloku2mia.
 
tafadhali tafadhali tafadhali! mnaoingia kwenye ndoa hizi jamani mnatakiwa mjue ndoa ni nini! Sasa wewe issue kidogo tu unafikiria kumwacha mkeo!! Jitahidi kujua kila stage ya maisha ya ndoa kama mkiwa bila mtoto mnakuwaje, mkiwa wajawazito mnakuwaje na mkiwa na watoto mnakuwaje na hatimaye uzeeni. Angalia hapo baadae akishajifungua usije ukasema namwacha kwani hanipi tena attention, yeye muda wote na mtoto tu! Jitahidi kuwa mvumilivu na kumwelewa mkeo mkuu hasa kipindi hiki cha matarajio.
 
Guys, its hard to understand men sometimes.
Hali hii ina muda gani? mana kutokana na thread yako naona kama ni siku moja tu sasa utaweza kweli kama ulivyoapa kwa shida na raha hadi kifo kitutenganishe?
Kitu kingine nahisi kama unafichaa kitu maana hadi anune pamoja na ujauzito ghafla kiasi hicho lazima kuna kitu nyuma ya pazia.
Nakushauri uvumilie na usibadili tabia coz ya attitude yake itacoz more problems, maana kwa miezi aliyonayo ni ya hatari sana. Pia uwe unatembea naye nyakati za jioni mkisharudi home ili mtoto ashuke na itampa urahisi wakati wakujifungua.
Huwezi kumchoka kwani ndoa ina miaka 50?nahisi huyo ndio fisrt born basi hamna mwaka au miaka2,ndoa inahitaji akili na wewwe ndio baba.
ONYO: haya mambo yakupost wake zenu humu ohooo isije ikawa kama ya Theone na wife ila kama ulichoandika ni kweli haya maana akigundua atapost humu halaf yatakua yaleyale
 
Mheshimiwa una watoto wangapi na shemeji yetu nathani hapo ndo uanze kupata mauzoefu mkuu hapo ndio ulezi unapo anza muhim sana jaribu kumuangalia sana sio umuache atembee KM5 nawewe umseme unamkomesha sioo kabisa ukiona hivyo nibora uwe unamfata ili uhakikishe hapati tatizo njiani muenzi sana niwakati mgum sana kwake mkuu hizo ndio tabia za mimba anaweza akwambia nipishe hapa unanuka na akawa hanahaja yakukuona lakini haipo ndani ya uwezo wake siku akijifungua tu yote yanaisha mkuu vumilia walasio swala la kushangaza nikawaida
 
Dear Daughter,

Plse tambua kuwa mimi sio tatizo, imagine mtu unampeleka na gari hadi kituoni. Then baadae unaenda tena na gari hadi kituoni unakaaa unaona muda umepita na sio kawaida yake kuchelewa hivyo, unampigia simu anasema anakaribia kufika home na yupo kwa mguu. Simu anayo na ina vocha, je kwanini asingesema kama nisimfuate kituoni leo kuwa ana mishemishe zake? mimi kosa langu hapo ni nini daughter?

Ndio maana nimeumia na kuamua nimuache since leo asubuhi aende ka kurudi home hadi hapo atakapojifungua huenda later ataweza ku-value kupelekwa na gari.

still nasubiri ushauri wako, ila mhmhm huyu bibie naona habebeki kabisaa!

Kama umeamua kuzira basi kuwa tayari kwa possibilities za mkeo kuzaa premature au kupoteza mtoto.km 10 kwa siku si mchezo
Google behaviour changes za mimba ili uwe imformed zaidi na pia inaweza akawa kapata pregnancy depression.
Au tafuta hata siku uende nae clinic umuulize gynae maswali kuliko kulalama tu
 
Huyu mwanamke anataka uwe una mpeleka kazini na kumchukua kila siku. kugombania daladala na mimba kubwa hivyo lazima maisha yawe magumu. so either tafuta dereva awe anampeleka na kumchukua kazini, halafu wewe panda daladala kwenye mishe zako. sishauri aendeshe gari mwenyewe akiwa na hali hiyo
 
Bwa'shee safari ya maisha ya ndoa ndo kwanza iko ubungo terminal.., acha kulalama lalama.ujauzito unakuja na mabadiliko ya tabia kwa kinamama,so don panik wala uskasirike zikumbuke zile siku alizokuwa 'yeye yeye kweli! Suala la mshahara wake,kaeni(baada ya kujifungua) mkubaliane kias gan kbak kwenye maendeleo ya familia. Nahis kpato chak kmeyumba mkuu ndo maana hata bia hazizd 2,tehe teh teh...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom