Sijui unapozungumzia makelele unazungumzia nini, naamini kila ndoa ina changamoto lakini pia kuna namna ya kutatua changamoto kwa upendo na hekima padipo kumfanya mwenzi wako ajisikie kudharaulika au ajute kwa namna moja au nyingine
Wanaume wengi si wepesi kujishusha hata wanapokosea, changamoto inakuja pale mwanamke anaposhout au kutumia lugha ya dharau/ubabe anapoona mwezie amekosea au hata anapohitaji kitu kutoka kwa mwenzi badala ya kutumi kuuliza kwa unyeyekevu
Trust me, mwanaume ni mwepesi sana kwa mwanamke, ila kama tu ukijua lugha ya kuzungumza nae, vilevile kwa mwanamke, kuna lugha ambazo pia wanaume mnapaswa kuzitumia kwa wake zenu especially pale unapokua umefanya jambo ambalo unajua limemuudhi au kumkwaza kwa namna moja au nyingine,
Watu mnaolala kitanda kimoja na kishare miili yenu hampaswi kupigizana kelele bali mnapaswa kuelewana