Ndoa chungu, ndugu wamezidi, nishauri nifanyeje?

Ndoa chungu, ndugu wamezidi, nishauri nifanyeje?

Samahani kama nitakukwaza kwa maswali yangu...
1. Mmeo ana umri gani?? Mmezidiana sana umri??
2. Mmeo ana mtoto wa nje??
3. Mmeo ni mlevi?? Ana akili timamu? Ana elimu gani??
4. Una uhakika anakupenda??

Hiyo namba nne hiyo ndiyo ya msingi zaidi kwa maana kwa hakika kama anakupenda angekusikiliza.
SIJUI NI MFUMO DUME NDIO UNAMSUMBUA HATA SIELEWI!!
 
... Kumbe wa hivi pia wapo nilidhani ni kwangu tu. Ngoja nisome comment huenda nami zikanisaidia. Bora kwako 10 kwangu 12 na wanafunzi wakifunga shule plus wageni tunafikaga mpaka 16 nyie acheni.

Wanaume muwe mnawashauri wanaume wenzenu maana sisi tukisema wanasema oooh hatupendi ndugu za mume.
 
Fanya hivi,
1. Acha kulima kwa msimu mmoja tu
2. Na wewe tafutiza ndugu zako hata wa mbaali kama watano hivi walete hapo home mkae now kwa mwaka mmoja tu.

Then tarehe 23/11/2017 njoo hapa tuletee mrejesho. sawa mama. Pole mama.
Nafikiri ukifuata huu ushauri huenda mmeo akabadili mtazamo wake.
 
... Kumbe wa hivi pia wapo nilidhani ni kwangu tu. Ngoja nisome comment huenda nami zikanisaidia. Bora kwako 10 kwangu 12 na wanafunzi wakifunga shule plus wageni tunafikaga mpaka 16 nyie acheni.

Wanaume muwe mnawashauri wanaume wenzenu maana sisi tukisema wanasema oooh hatupendi ndugu za mume.
Wakati mnaolewa mlituambia tuwashauri??? Endeleeni kufanya kazi, malalamiko ni mpaka 2020.
 
Hawa ndugu hawa mhh. Mm yalisha nikuta.
Mr alichukua mtoto wa mama ake mdogo ambaye ni marehemu akaamua amsomeshe, akamchukua na mdogo wake walioshare baba akampeleka nae shule. Baada kama ya miaka mitatu hivi mr akapata matatizo kazini. Kipato kikashuka sana . yule mdogo akawa ndio kamaliza la saba hela ya kumpeleka private hatuna, bahatinzuri mtoto alifaulu ikabidi asome shule ya serikali. Yule mwingine alikuwa form three boarding ada ilikuwa kubwa sana ikabidi tumrudishe asome day. YALIYOTUPATA SITAKUJA NISAHAU. ndugu wa mume walianza kumlaumu mr, kejeli za kila namna eti kwanini mtoto asome shule ya serikali, na kwanini mwingine arudi day!!!!! Walikuja kwa dharau kuwachukua watoto wao hata bila ya ridhaa yetu sisi walezi. Nikikumbuka machozi yaliyomdondoka mr kwaajili ya wema wake napata chuki kuu kwa ndugu zake.

Naona haya yako nbiona kuwapata na nyie
 
Katika lugha ya kawaida naweza kusema kuwa huyo mwanaume unayemuita mumeo.....ni moja kati ya wanaume wanaoingia kwenye ndoa hali ya kuwa hawajakomaa kiakili....na hawajui maana ya ndoa na kujenga misingi ya familia......

Mambo anayofanya si mambo yanayoonyesha kuwa hajui maana ya kujenga familia au yeye kuwa kichwa cha familia......

Kusaidia ndugu wenye uhitaji ni jambo la kawaida na ni jambo lenye kupendeza.....kutoa misaada hata kushindwa kutimiza majukumu yako wewe mwenyewe yanayogusa familia yako....ni ujinga unaoelekea kwenye upumbavu kama sio uwendawazimu......

Naweza kusema kuwa umepata bahati mbaya kupata mwanaume wa aina hiyo....lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya wewe kujutia maisha yako na kukosa raha......

Unaonekana ni mwanamke mwenye hekima na busara za hali ya juu na mpambanaji.....ulichokosa ni ni kiongozi wa kukuongoza kwenye mapambano hayo na kufikia mafanikio.......

Jaribu kutafuta sehemu tulivu na ukae na mumeo....umuelezee jinsi unavyokereka na jambo hilo kwa manufaa ya familia yenu nikiwa na maana vizazi vyenu.......ni maongezi ambayo kila mwanaume mwenye akili timamu yatamuingia akilini na kuwaza upya...........

Kurundika watu mbali mbali kwenye nyumba yenu si salama hasa kwa nyakati hizi zilizojaa wanadamu wenye roho za kinyama.......

Hujawahi kusikia kijana amekutwa akimnajisi mtoto wa dada yake na kumharibu.....!!! Na mengine mengi.....

Sio kama tunawachukia ndugu na jamaa zetu....bali tunajihami na matendo yao machafu kwenye familia zetu kwani wengi wao imani zimetoweka....na hawana utu kabisa......

Pigania ndoa yako kwa kiasi unachoona inatosha......na ukishindwa chukua hatua unazoona kuwa zinafaa.....

Maisha ni mafupi....hauna sababu ya kuishi kwa wasi wasi kwa sababu ya mwanadamu ambaye hajawahi kuridhika tangu kuumbwa kwa dunia hii......
Upo sawa mkuu
 
Yaani kama ulikuwepo vile, coz kuna wengine wakubwa nawazidi labda miaka mitatu hv; basi wanataka nao wajipangie utaratibu wao; mwingine anataka anywe chai lita nzima pekeake, mwingine msosi anataka arudie full plate hata mara tatu, nikisema niwapeleke shamba wanapiga simu kwa Mr ati wanaumwa wanataka kurudi, nabaki napiga kazi mwenyewe, basii duuuh, stress za kila rangi!

Ukweli utakuweka HURU. Kwa mawazo yangu jitahidi kujipambanua kwao vile unawaza moyoni mwako nadhani utakua na amani moyoni mwako.
 
... Kumbe wa hivi pia wapo nilidhani ni kwangu tu. Ngoja nisome comment huenda nami zikanisaidia. Bora kwako 10 kwangu 12 na wanafunzi wakifunga shule plus wageni tunafikaga mpaka 16 nyie acheni.

Wanaume muwe mnawashauri wanaume wenzenu maana sisi tukisema wanasema oooh hatupendi ndugu za mume.
Mimi pia nina family kubwa, wote ni ndugu wa mume wangu,
Bahati njema ni kuwa, I learned to love them. Japo vikwazo vya hapa na pale vipo nachukulia ni mapungufu ya kiubinadamu, huwa natake easy ili kuipa afya akili yangu.
 
Yaani kama ulikuwepo vile, coz kuna wengine wakubwa nawazidi labda miaka mitatu hv; basi wanataka nao wajipangie utaratibu wao; mwingine anataka anywe chai lita nzima pekeake, mwingine msosi anataka arudie full plate hata mara tatu, nikisema niwapeleke shamba wanapiga simu kwa Mr ati wanaumwa wanataka kurudi, nabaki napiga kazi mwenyewe, basii duuuh, stress za kila rangi!
Pole mummyto... Kuwa na subira, japo kuishi na ndugu ni mtihani, halafu wakishakuja mjini wanajidai hata vyombo hawajui kuosha. Muhimu ni kuwa wewe ndio mama hapo nyumbani kwako, usiruhusu mtu akupangie utaratibu, amri hapo ni mbili tu, ya mumeo na ya kwako, atakayehisi anakwazika ajue hapo hapamfai kuishi, aondoke taratibu.
 

Asprin ndugu yangu! Ngoja nijibu maswali yako kama ifuatavyo
1. Yeye ni mkubwa sana kwangu ananizidi miaka tisa.......niko in my early 30's yuko ktk his early 40's
2. Hana mtoto wa nje, labda kama kanificha, lakini sijapata kusikia habari ya mtoto wa nje
3. Hatumii kilevi cha aina yoyote, hata sigara
havuti, ana AKILI TIMAMU kabisa, ni msomi mwenye shahada ya Uzamili ktk fani ya misitu (Master's Degree)
4. Kwa umri wangu na utashi alionijalia Manani nina upeo wa kutambua kama napendwa au laah; Ninao ujasiri wa kusema kwamba ananipenda sana kama mke na mama mtoto wake.
5. KARIBU!!!
Basi mvumilie na usiache kumshauri. Hakuna "bahari" ya ndoa iliyotulia, mawimbi hayakosekani.
 
Kama eneo unaloishi ni kubwa mimi nikushauri jenga mabanda ya nguruwe uanze ufugaji hao hao wapangie mabanda kila mtu yake kulisha na kufanyia usafi pia nunua baiskeli uwape zamu yakuzunguruka machineni kutafuta pumba za kulishia hao nguruwe si hawataki shamba! Asiyetaka akupishe full stop.
Huwezi ishi na mtu ambae hataki kazi asiye fanya kazi asile.
 
... Kumbe wa hivi pia wapo nilidhani ni kwangu tu. Ngoja nisome comment huenda nami zikanisaidia. Bora kwako 10 kwangu 12 na wanafunzi wakifunga shule plus wageni tunafikaga mpaka 16 nyie acheni.

Wanaume muwe mnawashauri wanaume wenzenu maana sisi tukisema wanasema oooh hatupendi ndugu za mume.
pole mwaya

Sipati picha nina vichwa 12 ndani

Halafu viwe vijeuri maana bora wawe 12 wanaojituma na wenye utii

Usisahau kuweka akiba......wakiondokaga hao hutowaona.... mie wazazi wangu walihudumia ndugu weeee walipotetereka kidogo ndio walikuwa wa kwanza kusambaza maneno ya kejeli.... hamad mambo yakaaa sawa na watoto tumekuwa tuliwatiririshaje...
 
Fanya hivi,
1. Acha kulima kwa msimu mmoja tu
2. Na wewe tafutiza ndugu zako hata wa mbaali kama watano hivi walete hapo home mkae now kwa mwaka mmoja tu.

Then tarehe 23/11/2017 njoo hapa tuletee mrejesho. sawa mama. Pole mama.
hahaa sasa watakua na kijiji nyumbani
 
hii kali ya kufunga mwaka .tafuta chuo mbali mwambie unataka ukasome kama mwaka hivi umuachie waumini wake hapo
watu 15 nani anasonga ugali?
Well Miss Natafuta, kama ulivyosuggest, huo ni muda muafaka kwake wa kuongeza elimu, hata mpaka kiwango cha Udoctor na ikiwezekana na Uprofessor. Ni kusoma kwa kwenda mbele tena ikiwezekana mbali na hapo wakati wa likizo aje awashuhudie waumini wenzie hata kwa siku 3, tuone hapo nani atakuwa mjanja
 
... Kumbe wa hivi pia wapo nilidhani ni kwangu tu. Ngoja nisome comment huenda nami zikanisaidia. Bora kwako 10 kwangu 12 na wanafunzi wakifunga shule plus wageni tunafikaga mpaka 16 nyie acheni.

Wanaume muwe mnawashauri wanaume wenzenu maana sisi tukisema wanasema oooh hatupendi ndugu za mume.
Usipoangalia mtabaki masikini, kusaidia ndugu ni kitu muhimu na chenye thawabu kubwa, lakini kisizidi uwezo wenu hasa kwenye kipato chenu.

Hao wanaume wanaokusanya ndugu 12 at per ndani ya nyumba huwa wanafikiria nini? Au mna bangalore linawatosha wote? Manake a simple three-bedroom house mnalalaje?

Poleni wanawake na wanaume wote mnaoweza kuvumilia hayo. Kwa nini msitume misaada huko waliko, kwani ni lazima wasaidiwe hapo nyumbani kwenu??
 
Mimi pia nina family kubwa, wote ni ndugu wa mume wangu,
Bahati njema ni kuwa, I learned to love them. Japo vikwazo vya hapa na pale vipo nachukulia ni mapungufu ya kiubinadamu, huwa natake easy ili kuipa afya akili yangu.
Naomba kuuliza coz one thing I don't understand, hao ndugu kwa nini msiwasaidie huko wanakoishi? Kama ni shule, mnasomesha idadi mnayoweza lakini sio lazima muishi nao, mnawapeleka shule, wakifunga wanaenda kwa wazazi wao.

Au hawana wazazi? Coz kama ni yatima that's a different story.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom