Ndoa chungu, ndugu wamezidi, nishauri nifanyeje?

Ndoa chungu, ndugu wamezidi, nishauri nifanyeje?

Pole sana dada yangu.
NILICHOGUNDUA
-Ninyi ni wakulima
-Mnaendesha maisha kwa kutegemea mazao mliyovuna ya ghalani.
-Hamtegemei biashara
-Kinachokukwaza juu ya mumeo ni kitu kimoja tu,ndugu zake,hamna kingine.
USHAURI.
-Kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye anayewajaza,usitoe akiba yako yote kuhudumia.
-Hata siku ikitokea mnakaribia kushinda/kulala njaa,usitoe akiba yako yote.
-Fanya biashara zako kwa siri,asizijue,ili akiba yako izidi kutuna.
-Mkalishe chini umueleze
√ maisha ya siku hizi siyo kama ya zamani.
√ maisha yenu ya uzeeni itakuwaje
√ mboreshe kilimo kwa kutumia zana za kisasa kama trekta.
√ ndugu zake wanaokuja ni rasilimali kazi tosha msimu wa kilimo.
√ mazao machache ghalani bila pesa si kitu
√ thamani ya mazao yote ya ghalani na idadi mliyopo ndani ni sawasawa na masikini wa kutupwa.
 
Subra inahitajika zaidi hapo ongea na shem Vizuri na huruma isipite uwezo maisha y enyewe yalivyo magumu duuuh pole ila kaa nao kwa akili hao ndugu wa mumeo maan huwa wana mwanzo tu hao wala hawana mwisho mzuri
 
huyo jamaa yako ni mswahili tu,
ingawa tunajukumu la kusaidia ndugu zetu ila n vzr tuangalie kiasi ( it goes both way even for ladies).

Solution hapo ni kumuelekeza tu hamna jingine, taratiibu ataelewa na pia kupunguza stress uwe unamtoa out yeye kwa hela zako ili ajue na ww pia ni mtafutaji na unachangia uchmi wa familia nzima siyo yy pekee
 
Maisha haya yana historia ndefu. Inaonekana mme wako alikulia na kusomea kwenye maisha ya shida.

Jinsi walivyokua na familia yake baba, mama na wadogo/wakubwa zake yalikuwa maisha ya kuunga unga (samahani).

Roho yake ina upendo sana akikumbuka alipotoka.

Na inawezekana hata alichelewa kuoa na pengine alioa kwa shinikizo.

Shida kubwa ni kwamba hawataki kukusaidia kazi wanakuvunja mgongo tu, hapo nakupa pole.

Ila wamekuwa wengi, 10?!! Jaribu kuongea nae wapungue, ikiwezekana awasaidie wakiwa kwao.

Vumilia hiyo ndoa.
 
Vumilia 2 Miss, nawee leta ndugu zako
 
Katika lugha ya kawaida naweza kusema kuwa huyo mwanaume unayemuita mumeo.....ni moja kati ya wanaume wanaoingia kwenye ndoa hali ya kuwa hawajakomaa kiakili....na hawajui maana ya ndoa na kujenga misingi ya familia......

Mambo anayofanya si mambo yanayoonyesha kuwa hajui maana ya kujenga familia au yeye kuwa kichwa cha familia......

Kusaidia ndugu wenye uhitaji ni jambo la kawaida na ni jambo lenye kupendeza.....kutoa misaada hata kushindwa kutimiza majukumu yako wewe mwenyewe yanayogusa familia yako....ni ujinga unaoelekea kwenye upumbavu kama sio uwendawazimu......

Naweza kusema kuwa umepata bahati mbaya kupata mwanaume wa aina hiyo....lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya wewe kujutia maisha yako na kukosa raha......

Unaonekana ni mwanamke mwenye hekima na busara za hali ya juu na mpambanaji.....ulichokosa ni ni kiongozi wa kukuongoza kwenye mapambano hayo na kufikia mafanikio.......

Jaribu kutafuta sehemu tulivu na ukae na mumeo....umuelezee jinsi unavyokereka na jambo hilo kwa manufaa ya familia yenu nikiwa na maana vizazi vyenu.......ni maongezi ambayo kila mwanaume mwenye akili timamu yatamuingia akilini na kuwaza upya...........

Kurundika watu mbali mbali kwenye nyumba yenu si salama hasa kwa nyakati hizi zilizojaa wanadamu wenye roho za kinyama.......

Hujawahi kusikia kijana amekutwa akimnajisi mtoto wa dada yake na kumharibu.....!!! Na mengine mengi.....

Sio kama tunawachukia ndugu na jamaa zetu....bali tunajihami na matendo yao machafu kwenye familia zetu kwani wengi wao imani zimetoweka....na hawana utu kabisa......

Pigania ndoa yako kwa kiasi unachoona inatosha......na ukishindwa chukua hatua unazoona kuwa zinafaa.....

Maisha ni mafupi....hauna sababu ya kuishi kwa wasi wasi kwa sababu ya mwanadamu ambaye hajawahi kuridhika tangu kuumbwa kwa dunia hii......
 
Yaani kama ulikuwepo vile, coz kuna wengine wakubwa nawazidi labda miaka mitatu hv; basi wanataka nao wajipangie utaratibu wao; mwingine anataka anywe chai lita nzima pekeake, mwingine msosi anataka arudie full plate hata mara tatu, nikisema niwapeleke shamba wanapiga simu kwa Mr ati wanaumwa wanataka kurudi, nabaki napiga kazi mwenyewe, basii duuuh, stress za kila rangi!
dah pole sana dada...Mpaka nimeogopa ndoa
 
Tumia hao ndugu kwa uzalishaji, na kama mr hataki ongea nae mara kadhaa, ikishindikana muachie hiyo nyumba kwa muda peke yake ajifunze.
 
aisee pole mama uko kwenye wakat mgumu sana hakuna chalenge kama ya kuish na ndugu au kutegemewa na ndugu.
 
Huwez jua nani atakuja kukusaidia siku za mbelen(labda uzeeni).Huenda ni katka hao hao.Wasaidien tu dada angu kwanza maisha yenyew tunapta kila kitu tutakiacha
 
Hiyo misaada imezidi kiukweli,kuna namna yakusaidia kwa utaratibu mzuri hili na uchumi wa familia uendelee.
 
Muombe ruhusa ya kwenda kwenu kusalimia akikuruhusu, kaa mwezi mzima ili uone jinsi atakavyoulea huo ukoo wake. Pengine anataka kukutimua kijanja, si unaelewa tena akufukuzae hakwambii toka ni vitendo tuu.
Nilishawahi kufanya hivyo, nilisingizia shangazi ameeniita kuna jambo la muhimu sana anataka kuzungumza nami, nilikaa wiki tatu akanifuata kunirudisha home. Nilipokua home nilimweleza shangaziangu hali halisi lakini alichonijibu ni kwamba nisimuonee yeye anazeekea kwa mumewe mengi kayavumilia, akamalizia kwa kusema ndoa ya kikristo ina mlango mmoja tu ambao ni wa kuingilia, hakuna mlango wa kutokea! Basi nikabaki hoi, Mr alipokuja basi ni kugeuza tu
 
Yaani kama ulikuwepo vile, coz kuna wengine wakubwa nawazidi labda miaka mitatu hv; basi wanataka nao wajipangie utaratibu wao; mwingine anataka anywe chai lita nzima pekeake, mwingine msosi anataka arudie full plate hata mara tatu, nikisema niwapeleke shamba wanapiga simu kwa Mr ati wanaumwa wanataka kurudi, nabaki napiga kazi mwenyewe, basii duuuh, stress za kila rangi!
Mhh hao chapa ng'ombe nini?
kwa kweli hamtafanya maendeleo yoyote ktk familia.pole ndugu hizo ndio changamoto za ndoa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom