Ndoa chungu, ndugu wamezidi, nishauri nifanyeje?

Ndoa chungu, ndugu wamezidi, nishauri nifanyeje?

wewe omba likizo dada mwambie naenda kwa mama siku tatu mbili we unapiga mwezi alaf atajua ugumu upo wap.!!ila pia kama kisirani atakupa tiketi ya kuondokeamaana sisi wanaume wa sasa tupo kama mh wa mwanza hatupend ujinga
 
Hapana, moto hauzimwi kwa moto, asifanye hivyo!

Mkuu ni kweli moto hauzimwi kwa moto, ila unajua kuwa moto unazuiwa kwa moto?? Watu wa Iringa hasa mufindi wanakopanda miti ya mbao wanaelewa hii theory.
 
Wandugu Salaam,

Mimi nipo kwenye ndoa miaka saba sasa na tuna mtoto mmoja, tunaishi Nyanda za juu kusini. Tuliishi kwa amani miaka mitatu tu, tukiwa mimi na mume wangu na mtoto. Baada ya hapo imekua tabu, mimi kwetu kuna ahueni ya kiuchumi, yaani sitegemewi na wazazi wangu labda mimi ndio niombe msaada kwako. Lakini kwa upande wa mume wangu imekua tatizo yeye ndio anaetegemewa, yaani ndio star kwao.

Sasa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio wategemezi wanazidi, watoto wa ndugu zake wa kuwasomesha ndio wanazidi, applicants wa misaada kutoka kwao ndio wanazidi wanaomba hata ambavyo wangeweza kujisaidia wenyewe kwa jinsi anavyowaendekeza.

Anafanya bidii kuwatafuta watoto wa ndugu zake hata waliotelekezwa na wazazi wao tena wakingali hai anawajaza home. Yote hayo ninayavumilia na ninapambana nayo. Mimi sijabahatika kupata ajira tangu nimehitimu masomo yangu, yeye ndio ana ajira. Lakini mimi sijabweteka najishughulisha na kilimo na hata chakula tunachokula (mpunga na mahindi) nalima mwenyewe.

Sasa kila nikijaribu kumuelimisha kwamba sichukii kuwasaidia ndugu zake na hata kuwasomesha watoto wa ndugu zake bali kuwepo na namna ya kuwasaidia wakiwa makwao na si kuwajaza hapa home inaleta stress maisha yanazidi kuwa magumu mwenzangu hataki tena ananichefua kwa kunijibu ati kwani kuna shida gani mbona chakula kipo ndani, yaani hakuna shida ya chakula kabisa.

Hakika majibu haya yananivunja moyo kuendelea na kilimo, nawaza labda niache kabisa kulima ili nione kama ataweza kununua chakula cha kulisha familia kubwa namna hii. Kubwa zaidi sasa na linalonichanganya hasa na ninaomba ushauri wenu ndugu wana MMU; Ni kwamba kama vile hawa waliopo hapa home na tunaowasomesha huko makwao hawatoshi, sasa amemtafuta binti wa marehemu kaka yake ambae ana umri wa miaka 24 na ana watoto wawili, anataka amtoe huko anakoishi (anaishi mikoa ya Mashariki, anajishughulisha na kuuza bar, kwa mujibu wa maelezo ya baba mtu) aje tuishi nae hapa home.

Nimemuuliza sababu ya kumchukua binti mkubwa kama huyo tena aliyezoea maisha ya bar; kanijibu anatanga tanga kwa sababu baba yake alikufa, ngoja aje tukae nae tuwasomeshe na hao watoto wake (binti kasema watoto wote hawana baba); hivi ninapoleta uzi huu baba mtu kishaanza mchakato wa kutafuta shule kwa ajili ya mtoto (mjukuu) mkubwa ambae ana miaka sita. Anamtafutia private school aanza chekechea mwakani.

Kazi anayofanya ni ya kipato cha kawaida kiasi kwamba misaada imezidi uwezo (wanadrain) mara nyingi tunabaki hatuna hata senti tano! Hata ninapofurukuta kwa kufanya biashara ndogondogo mbali na kilimo najikuta mtaji unakata, nabaki kuzubaa tu.

Sasa jamani mwenzenu kama binadamu, tena kijana mwenye ndoto za maisha ya mbeleni nashindwa la kufanya, naishiwa hamu ya hii ndoa yangu, natamani nitoke nikapange na mwanangu nipambane kivyangu lakini tena roho inanisuta! NIPO NJIA PANDA, nifanyeje jamani na tabia ya mwanaume huyu! Na hasa huyu binti na watoto wake, natamani nipate namna nyingine ya kumsaidia lakini asije hapa home coz tayari tupo kumi hadi sasa, na hiki ni kipindi cha likizo huwa tunafika mpaka kumi na tano na haya ni maisha ya mjini (u can imagine)!

Msaada jamani!

Nawaomba wale wanaolete mizaha wapite kimya coz nahisi wataniongezea stress.
Kwanza kabisa pole sana dada angu. Na Mungu akutie nguvu sana katika hayo yote unayopitia.

Niseme tu kwamba, hali kama hizo uwa mara nyingi zinatokea kwa ndoa ambapo unakuta mawazo ya mwanaume ni final. Kwa hiyo unakuta mume wako anaona hayo unayo mshauri ni bure.

Hatuwezi jua nini hasa kinampelekea kujisikia ana responsibility kubwa hivyo kwa ndugu zake labda hapo nyuma kabla hamjakuta walimsaidia sana. Kwa hiyo ni kama he is returning a favor.

Cha msingi lakini ni kuwa na msimamo juu ya kile unachomweleza lakini usiweke heshima kando Tafadhali. Ongea nae ila kwa heshima ukiona hakuna mabadiliko unaweza kushirikisha wazee wenye hekima. Muweke kikao myajadili, kuwa wazi jinsi hali hiyo inavyokuumiza.

Mungu akutangulie
 
Mungu anisaidie, maana kwa akili zangu siwezi!!
 
Kweli kuna familia nyingine zina uchumi mdogo kwa hiyo aliyetoka mmoja ndo anatakiwa abebe mzigo;
Huyo anayekuja na watoto ampangishie chumba mtaani vinginevyo ujuwe ndo mwisho wa ndoa yako
na hao watoto awapeleke shule za kawaida;

Endelea kumshauri na kumsaidia pia;
Ahsante kwa ushauri, ubarikiwe!
duuu pole sana ndugu.yan najitahid kuimajin ingekuwa mimi ningefanyaje.mi nimeisha maisha ya hivyo baba ndugu kibao mpaka watoto tunasaulika hata kula chakula kizur ilishindikana ni kula ugali maharage kama shule za boarding.na mwisho baada ya kufanikiwa hakuna aliyetukumbuka zaid ya kutuangamiza.tenda mema uende zako usingoje shukran.kama walivyo shauri wenzangu mama mazao yanauzika siku hizi .fanya mambo yako wewe kama Weka akida yako na mfungulie mtoto account muwekee akiba.vaa tinted asikuumize kichwa fanya yako.
 
Kama unalima panua mashamba wapeleke wakalime badala ya kuajiri watu watumie hao wa nyumbani mwako
Mleta uzi chukua ushauri wa............. mbavusimba...........
Mbavusimba ungekuwa unakula komoni ningekutafta jioni
 
Kwanza kabisa pole sana dada angu. Na Mungu akutie nguvu sana katika hayo yote unayopitia.

Niseme tu kwamba, hali kama hizo uwa mara nyingi zinatokea kwa ndoa ambapo unakuta mawazo ya mwanaume ni final. Kwa hiyo unakuta mume wako anaona hayo unayo mshauri ni bure.

Hatuwezi jua nini hasa kinampelekea kujisikia ana responsibility kubwa hivyo kwa ndugu zake labda hapo nyuma kabla hamjakuta walimsaidia sana. Kwa hiyo ni kama he is returning a favor.

Cha msingi lakini ni kuwa na msimamo juu ya kile unachomweleza lakini usiweke heshima kando Tafadhali. Ongea nae ila kwa heshima ukiona hakuna mabadiliko unaweza kushirikisha wazee wenye hekima. Muweke kikao myajadili, kuwa wazi jinsi hali hiyo inavyokuumiza.

Mungu akutangulie
Amina!
 
Ahsante dear! Nitaendelea kusugua goti coz bila Yesu siwezi
 
MUMEO NAYE ANA SHIDA ....SEMA NDIO ANAAMUA YEYE SASA USISHINDANE NAYE YEYE NI KICHWA,,..SASA MAKE SURE UNAKUWA NA UJANJA WA KUWKA AU KUFICHA UNTOUCHABLE AMOUNTS KWA AJILI YA BAADAE..MAANA KAJISAHAU HUYO KASHIKWA AKILI...SIOLAZIMA WAJAZANE HAPO NDIO IONEKANE UNASAIDIA
 
Wadada kabla ya kuolewa, jitajid vyovyote vile kumjua mumeo mtarajiwa na mazingira aliyoishi kabla hamjajuana. Kuna koo zingine unakuta alisomeshwa na wana ukoo, lazima arudishe fadhila
 
Wadada kabla ya kuolewa, jitajid vyovyote vile kumjua mumeo mtarajiwa na mazingira aliyoishi kabla hamjajuana. Kuna koo zingine unakuta alisomeshwa na wana ukoo, lazima arudishe fadhila
Basi ndio labda inanicost mimi sasa, mweeeeh, Mungu anisaidie coz mume nampenda ila haya mambo ndio yananichosha yananifanya nione nimepotea. Mimi tangu nakua sijawahi yaona mambo haya, nimeona watu wakisaidia ndugu zao lakini si kwa kiwango cha kujifilisi, kujitia madeni na mifadhaiko! Khaaaaaaa!!!
 
Yaani kama ulikuwepo vile, coz kuna wengine wakubwa nawazidi labda miaka mitatu hv; basi wanataka nao wajipangie utaratibu wao; mwingine anataka anywe chai lita nzima pekeake, mwingine msosi anataka arudie full plate hata mara tatu, nikisema niwapeleke shamba wanapiga simu kwa Mr ati wanaumwa wanataka kurudi, nabaki napiga kazi mwenyewe, basii duuuh, stress za kila rangi!
Samahani kama nitakukwaza kwa maswali yangu...
1. Mmeo ana umri gani?? Mmezidiana sana umri??
2. Mmeo ana mtoto wa nje??
3. Mmeo ni mlevi?? Ana akili timamu? Ana elimu gani??
4. Una uhakika anakupenda??

Hiyo namba nne hiyo ndiyo ya msingi zaidi kwa maana kwa hakika kama anakupenda angekusikiliza.
 
Dah pole dada maana kuishi na watoto wasio wako kuna mengi...mueleweshe kwa upole maana hao watu ni wengi kama vipi awasaidie wakiwa kwao maana hapo kazi zitazidi na kuishi na mtu mzima mwenzio kazi maana ataona vya baba yangu.Mungu akusaidie upite salama
CUT YOUR COAT ACORDING TO YOUR SIZE, MSAADA USIZIDI UWEZO. FAMILIA NI BABA, MAMA NA WATOTO. MWAMBIE MUMEO ANA MFUMO DUME NA NI BWEGE VILE VILE, NAPASUA JIPU.
 
Samahani kama nitakukwaza kwa maswali yangu...
1. Mmeo ana umri gani?? Mmezidiana sana umri??
2. Mmeo ana mtoto wa nje??
3. Mmeo ni mlevi?? Ana akili timamu? Ana elimu gani??
4. Una uhakika anakupenda??

Hiyo namba nne hiyo ndiyo ya msingi zaidi kwa maana kwa hakika kama anakupenda angekusikiliza.
Asprin ndugu yangu! Ngoja nijibu maswali yako kama ifuatavyo
1. Yeye ni mkubwa sana kwangu ananizidi miaka tisa.......niko in my early 30's yuko ktk his early 40's
2. Hana mtoto wa nje, labda kama kanificha, lakini sijapata kusikia habari ya mtoto wa nje
3. Hatumii kilevi cha aina yoyote, hata sigara
havuti, ana AKILI TIMAMU kabisa, ni msomi mwenye shahada ya Uzamili ktk fani ya misitu (Master's Degree)
4. Kwa umri wangu na utashi alionijalia Manani nina upeo wa kutambua kama napendwa au laah; Ninao ujasiri wa kusema kwamba ananipenda sana kama mke na mama mtoto wake.
5. KARIBU!!!
 
pole but kaa ukijua ata mkibaki wawili wewe na mmeo still hela haitatosha nikuibie dada kila binadamu ana riziki yake
yaani huwezi jua kuna riziki mnazipata kupitia hao mlionao koz na wao wanariki zao sema kwa 7bu mungu hawezi kukuleza kuwa hii riziki ni imekuja kwa ajili ya fulani
so labda uwe na yako tu ndo utoke
15 sio watu wengi kuna familia tukikukabidhi basi siku hiyox2 utachomoka kwa mmeo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom