Ndoa chungu, ndugu wamezidi, nishauri nifanyeje?


sisame

sisame

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Messages
365
Likes
308
Points
80
sisame

sisame

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2016
365 308 80
Wandugu Salaam,

Mimi nipo kwenye ndoa miaka saba sasa na tuna mtoto mmoja, tunaishi Nyanda za juu kusini. Tuliishi kwa amani miaka mitatu tu, tukiwa mimi na mume wangu na mtoto. Baada ya hapo imekua tabu, mimi kwetu kuna ahueni ya kiuchumi, yaani sitegemewi na wazazi wangu labda mimi ndio niombe msaada kwako. Lakini kwa upande wa mume wangu imekua tatizo yeye ndio anaetegemewa, yaani ndio star kwao.

Sasa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio wategemezi wanazidi, watoto wa ndugu zake wa kuwasomesha ndio wanazidi, applicants wa misaada kutoka kwao ndio wanazidi wanaomba hata ambavyo wangeweza kujisaidia wenyewe kwa jinsi anavyowaendekeza.

Anafanya bidii kuwatafuta watoto wa ndugu zake hata waliotelekezwa na wazazi wao tena wakingali hai anawajaza home. Yote hayo ninayavumilia na ninapambana nayo. Mimi sijabahatika kupata ajira tangu nimehitimu masomo yangu, yeye ndio ana ajira. Lakini mimi sijabweteka najishughulisha na kilimo na hata chakula tunachokula (mpunga na mahindi) nalima mwenyewe.

Sasa kila nikijaribu kumuelimisha kwamba sichukii kuwasaidia ndugu zake na hata kuwasomesha watoto wa ndugu zake bali kuwepo na namna ya kuwasaidia wakiwa makwao na si kuwajaza hapa home inaleta stress maisha yanazidi kuwa magumu mwenzangu hataki tena ananichefua kwa kunijibu ati kwani kuna shida gani mbona chakula kipo ndani, yaani hakuna shida ya chakula kabisa.

Hakika majibu haya yananivunja moyo kuendelea na kilimo, nawaza labda niache kabisa kulima ili nione kama ataweza kununua chakula cha kulisha familia kubwa namna hii. Kubwa zaidi sasa na linalonichanganya hasa na ninaomba ushauri wenu ndugu wana MMU; Ni kwamba kama vile hawa waliopo hapa home na tunaowasomesha huko makwao hawatoshi, sasa amemtafuta binti wa marehemu kaka yake ambae ana umri wa miaka 24 na ana watoto wawili, anataka amtoe huko anakoishi (anaishi mikoa ya Mashariki, anajishughulisha na kuuza bar, kwa mujibu wa maelezo ya baba mtu) aje tuishi nae hapa home.

Nimemuuliza sababu ya kumchukua binti mkubwa kama huyo tena aliyezoea maisha ya bar; kanijibu anatanga tanga kwa sababu baba yake alikufa, ngoja aje tukae nae tuwasomeshe na hao watoto wake (binti kasema watoto wote hawana baba); hivi ninapoleta uzi huu baba mtu kishaanza mchakato wa kutafuta shule kwa ajili ya mtoto (mjukuu) mkubwa ambae ana miaka sita. Anamtafutia private school aanza chekechea mwakani.

Kazi anayofanya ni ya kipato cha kawaida kiasi kwamba misaada imezidi uwezo (wanadrain) mara nyingi tunabaki hatuna hata senti tano! Hata ninapofurukuta kwa kufanya biashara ndogondogo mbali na kilimo najikuta mtaji unakata, nabaki kuzubaa tu.

Sasa jamani mwenzenu kama binadamu, tena kijana mwenye ndoto za maisha ya mbeleni nashindwa la kufanya, naishiwa hamu ya hii ndoa yangu, natamani nitoke nikapange na mwanangu nipambane kivyangu lakini tena roho inanisuta! NIPO NJIA PANDA, nifanyeje jamani na tabia ya mwanaume huyu! Na hasa huyu binti na watoto wake, natamani nipate namna nyingine ya kumsaidia lakini asije hapa home coz tayari tupo kumi hadi sasa, na hiki ni kipindi cha likizo huwa tunafika mpaka kumi na tano na haya ni maisha ya mjini (u can imagine)!

Msaada jamani!

Nawaomba wale wanaolete mizaha wapite kimya coz nahisi wataniongezea stress.
 
A

ammoshi

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2013
Messages
401
Likes
297
Points
80
A

ammoshi

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2013
401 297 80
Dah pole dada maana kuishi na watoto wasio wako kuna mengi...mueleweshe kwa upole maana hao watu ni wengi kama vipi awasaidie wakiwa kwao maana hapo kazi zitazidi na kuishi na mtu mzima mwenzio kazi maana ataona vya baba yangu.Mungu akusaidie upite salama
 
LadyAJ

LadyAJ

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2015
Messages
7,143
Likes
9,261
Points
280
LadyAJ

LadyAJ

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2015
7,143 9,261 280
Japokua waswahili husema ukipenda boga, penda na ua lake lakini hayo maua ya mumeo yamezidi mwenzangu kha!? Hapo ukija kutahamaki baadae mme zeeka mtoto wenu hatokua na Mbele wala nyuma mtamuacha mbwiii kwa kuendekeza ndugu,pole
 
belionea

belionea

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2014
Messages
903
Likes
652
Points
180
belionea

belionea

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2014
903 652 180
Vumilia tu jaman ndoa ni kuvumiliana kama uliweza kuvulimilia hiyo miaka saba ila itabidi utafute ajira au biashara yeyote ya kukuingizia kipato ili uwe independent na sio kutegemea mshahara wa mumeo
 
Sakayo

Sakayo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Messages
39,354
Likes
112,278
Points
280
Sakayo

Sakayo

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2015
39,354 112,278 280
Daaah, hiyo ni changamoto kwa kweli.
Sikushauri uwafukuze maana ndugu wa mume watakuona mbaya. Sasa wewe bana hiyo faida yako unayopata kwenye kilimo na biashara zako. Kidogo tumia kuhudumia familia ila hakikisha unajiwekea akiba kidogo kwa ajili ya maendeleo, huyo anayelea ukoo mwache aendelee kama hakuelewi atakuja kushtuka akiwa ameshachelewa.
 
sisame

sisame

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Messages
365
Likes
308
Points
80
sisame

sisame

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2016
365 308 80
Dah pole dada maana kuishi na watoto wasio wako kuna mengi...mueleweshe kwa upole maana hao watu ni wengi kama vipi awasaidie wakiwa kwao maana hapo kazi zitazidi na kuishi na mtu mzima mwenzio kazi maana ataona vya baba yangu.Mungu akusaidie upite salama
Yaani kama ulikuwepo vile, coz kuna wengine wakubwa nawazidi labda miaka mitatu hv; basi wanataka nao wajipangie utaratibu wao; mwingine anataka anywe chai lita nzima pekeake, mwingine msosi anataka arudie full plate hata mara tatu, nikisema niwapeleke shamba wanapiga simu kwa Mr ati wanaumwa wanataka kurudi, nabaki napiga kazi mwenyewe, basii duuuh, stress za kila rangi!
 
sisame

sisame

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Messages
365
Likes
308
Points
80
sisame

sisame

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2016
365 308 80
Japokua waswahili husema ukipenda boga, penda na ua lake lakini hayo maua ya mumeo yamezidi mwenzangu kha!? Hapo ukija kutahamaki baadae mme zeeka mtoto wenu hatokua na Mbele wala nyuma mtamuacha mbwiii kwa kuendekeza ndugu,pole
Na hawatokumbuka kama baba yake alimaliza nguvu zake kwa kuwahangaikia wao! Yaani hadi sielewi!
 
sisame

sisame

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Messages
365
Likes
308
Points
80
sisame

sisame

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2016
365 308 80
Daaah, hiyo ni changamoto kwa kweli.
Sikushauri uwafukuze maana ndugu wa mume watakuona mbaya. Sasa wewe bana hiyo faida yako unayopata kwenye kilimo na biashara zako. Kidogo tumia kuhudumia familia ila hakikisha unajiwekea akiba kidogo kwa ajili ya maendeleo, huyo anayelea ukoo mwache aendelee kama hakuelewi atakuja kushtuka akiwa ameshachelewa.
Ahsante kwa ushauri, nitaufanyia kazi
 
kenstar

kenstar

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Messages
2,300
Likes
1,404
Points
280
kenstar

kenstar

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2015
2,300 1,404 280
Ni mzigo sana kujaza watu sababu kila mmoja ana tabia yake tatizo huyo mumeo ashauriki siku hizi tunasaidia MTU akiwa mbali,sababu hawana shukrani hao wala kuja kuwa kumbuka mifano ni mingi na zaid watakuja kuwalaumu tu,Raha ya ndoa ni kuwa na amani ya maamuzi ya pamoja.
 
Brightfame

Brightfame

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2016
Messages
1,151
Likes
1,109
Points
280
Age
47
Brightfame

Brightfame

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2016
1,151 1,109 280
Muombe ruhusa ya kwenda kwenu kusalimia akikuruhusu, kaa mwezi mzima ili uone jinsi atakavyoulea huo ukoo wake. Pengine anataka kukutimua kijanja, si unaelewa tena akufukuzae hakwambii toka ni vitendo tuu.
 
kopites

kopites

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2015
Messages
5,079
Likes
4,328
Points
280
kopites

kopites

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2015
5,079 4,328 280
Duh!...kumi?hao ni noooma.
 
Mbimbinho

Mbimbinho

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2009
Messages
6,821
Likes
3,891
Points
280
Mbimbinho

Mbimbinho

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2009
6,821 3,891 280
Fanya hivi,
1. Acha kulima kwa msimu mmoja tu
2. Na wewe tafutiza ndugu zako hata wa mbaali kama watano hivi walete hapo home mkae now kwa mwaka mmoja tu.

Then tarehe 23/11/2017 njoo hapa tuletee mrejesho. sawa mama. Pole mama.
 
Reina princess

Reina princess

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Messages
1,330
Likes
1,430
Points
280
Reina princess

Reina princess

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2015
1,330 1,430 280
Duh pole sana
 
GOOGLE

GOOGLE

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
1,870
Likes
719
Points
280
GOOGLE

GOOGLE

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2012
1,870 719 280
Kama ulisoma zama zetu methali hii si ngeni kwako, jibu afu tukushauri.


Ukipenda Ua.......
 

Forum statistics

Threads 1,273,551
Members 490,428
Posts 30,484,754