Ndoa chungu, ndugu wamezidi, nishauri nifanyeje?

Huyo mume sio msukuma kweli? [emoji23]
Msukuma kafanya nini tena? Wasukuma siye wapole hatuna neno na mtu jamani mambo mengi mnatusingizia tu. Na kama uliona Msukuma mmoja wa hovyo basi please usijuimuishe wote. Na kama ni +ke niPM nije nikuonyeshe kwa mifano upole, ukarimu na utu wa Wasukuma.
 
Dadaangu, ngoja nikupe mfano halisi, mimi nimelelewa na mama tu ambapo mama alikuwa na position nzuri kikazi kiasi kusoma shule nzuri ilikuwa sio tatizo, wala kuhudumia familia ilikuwa sio tatizo, (tumezaliwa wawili tu mimi na kaka yangu) kuna kipindi mama alihamishwa kikazi kutoka mkoa fulani akarudishwa kwenye mkoa alipozaliwa (kwao) hapo ndipo kimbembe kilipoanza, watoto wa dada zake , kaka zake, ndugu wengine wa mbali wote walikusanyika nyumbani kwasababu katika ukoo wao angalau mamangu alikuwa successful, ilikuwa inafika time familia inakuwa na watu 23, ikipungua inakuwa na watu 13-15. Uzuri mama alikuwa mkoani kwao kwahiyo alienda kijijini kwao kutafuta mashamba na vijana wasaidizi wa mashamba akawatafutia na sehemu ya kuishi (alikuwa na nyumba huko kijijini) kwahiyo chakula cha nyumbani kikawa kinatoka mashambani, hii ilisababisha ahueni ya maisha pale nyumbani,
Lakini kwa ukubwa ule wa familia matumizi ya pesa yalikuwa makubwa mno, kusomesha shule za private wengine walisoma za kawaida tu. Kiukweli mama alikuwa akionekana nje ana maisha mazuri lakini kwenye familia alikuwa akijibana mno.
Pamoja na yote aliyokuwa akiwafanyia ndugu ni mtu ambaye anaongoza kwa kusemwa na kulaumiwa kwenye ukoo wao, this looks funny I guess.
Matokeo ya hayo maisha mama mpaka ana staafu kazi alikuwa na maisha magumu mno, hakuwa amesave chochote wala hakuinvest chochote. Lakini pia wote aliowalea sidhani kama wanamkumbuka kwa chochote.
Hata nyumba yake ni ile ile aliyokuwa akiishi miaka yote, ikabidi mimi na kakaangu tushikane mashati tumjengee mama na tumtafutie hata kausafiri kake ka bei rahisi, hela ambazo tungeweza kufanyia maendeleo ya familia zetu.
Ndugu hawana aibu jamani na bado hadi sa hivi wengine wanampelekea vitoto (nakuwaga mkali kama mbogo nikiambiwa kuna kitoto kwa mama ) Wakati mama ili ale ni lazima mimi na kakaangu tutume hela na angalau kuna kabiashara tumemfungulia tumemuwekea na msichana huyo msichana ndiye anayeishi nae hadi sasa. Tatizo mamaangu nae mbishiiii, nikitaka kumchukua niishi nae anasema ye hawezi kuishi kwa watu hahaha!
Hiyo story yako ni reflection ya hii niliyokueleza kwahiyo akili kichwani kwako.
 
Wandugu Salaam!
Mimi nipo kwenye ndoa miaka saba sasa na tuna mtoto mmoja, tunaishi nyanda za juu kusini.Tuliishi kwa amani miaka mitatu tu, tukiwa mimi na mume wangu na mtoto. Baada ya hapo imekua tabu, mimi kwetu kuna ahueni ya kiuchumi, yaani sitegemewi na wazazi wangu labda mimi ndio niombe msaada kwako. Lakini kwa upande wa mume wangu imekua tatizo yeye ndio anaetegemewa....yaani ndio star kwao. Sasa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio wategemezi wanazidi, watoto wa ndugu zake wa kuwasomesha ndio wanazidi, applicants wa misaada kutoka kwao ndio wanazidi wanaomba hata ambavyo wangeweza kujisaidia wenyewe kwa jinsi anavyowaendekeza. Anafanya bidii kuwatafuta watoto wa ndugu zake hata waliotelekezwa na wazazi wao tena wakingali hai anawajaza
home. Yote hayo ninayavumilia na ninapambana nayo.
Mimi sijabahatika kupata ajira tangu nimehitimu masomo yangu, yeye ndio ana ajira. Lakini mimi sijabweteka najishughulisha na kilimona hata chakula tunachokula (mpunga na mahindi) nalima mwenyewe. Sasa kila nikijaribu kumuelimisha kwamba sichukii kuwasaidia ndugu zake na hata kuwasomesha watoto wa ndugu zake bali kuwepo na namna ya kuwasaidia wakiwa makwao na si kuwajaza hapa home inaleta stress maisha yanazidi kuwa magumu...mwenzangu hataki tena ananichefua kwa kunijibu...ati kwani kuna shida gani mbona chakula kipo ndani, yaani hakuna shida ya chakula kabisaa! Hakika majibu haya yananivunja moyo kuendelea na kilimo, nawaza labda niache kabisa kulima ili nione kama ataweza kununua chakula cha kulisha familia kubwa namna hii.
Kubwa zaidi sasa na linalonichanganya hasaa na ninaomba ushauri wenu ndugu wana MMU; Ni kwamba kama vile hawa waliopo hapa home na tunaowasomesha huko makwao hawatoshi, sasa amemtafuta binti wa marehemu kaka yake ambae ana umri wa miaka 24 na ana watoto wawili, anataka amtoe huko anakoishi (anaishi mikoa ya Mashariki, anajishughulisha na kuuza bar, kwa mujibu wa maelezo ya baba mtu) aje tuishi nae hapa home. Nimemuuliza sababu ya kumchukua binti mkubwa kama huyo tena aliyezoea maisha ya bar; kanijibu anatanga tanga kwa sababu baba yake alikufa, ngoja aje tukae nae tuwasomeshe na hao watoto wake (binti kasema watoto wote hawana baba); hv ninapoleta uzi huu baba mtu kishaanza mchakato wa kutafuta shule kwa ajili ya mtoto (mjukuu) mkubwa ambae ana miaka sita. Anamtafutia private school aanza chekechea mwakani. Kazi anayofanya ni ya kipato cha kawaida kiasi kwamba misaada imezidi uwezo (wanadrain) mara nyingi tunabaki hatuna hata senti tano! Hata ninapofurukuta kwa kufanya biashara ndogondogo mbali na kilimo najikuta mtaji unakata, nabaki kuzubaa tu!
Sasa jamani mwenzenu kama binadamu, tena kijana mwenye ndoto za maisha ya mbeleni nashindwa la kufanya, naishiwa hamu ya hii ndoa yangu, natamani nitoke nikapange na mwanangu nipambane kivyangu lakini tena roho inanisuta! NIPO NJIA PANDA, nifanyeje jamani na tabia ya mwanaume huyu! Na hasa huyu binti na watoto wake, natamani nipate namna nyingine ya kumsaidia lakini asije hapa home coz tayari tupo kumi hadi sasa, na hiki ni kipindi cha likizo huwa tunafika mpaka kumi na tano na haya ni maisha ya mjini (u can imagine)!! Msaada jamani!
Nawaomba wale wanaolete mizaha wapite kimya coz nahisi wataniongezea stress
Qualification yako ni nini
Kama msomi achana na kilimo tafuta ajira
Umueekee mtoto wako hakiba
 
Mkuu aziza miradi mikubwa ya ufugaji biashara na kilimo washirikishe hao ndugu ili wapunguze ugumu wa maisha
 
Ishakuwa Gozi.

Haohao Ndugu wa Mumeo ndio watakaokuweka kwenye wakati mgumu.

Watamtia maneno Mumeo mpaka itafikia wewe kuachika.

Hapo usalama wa Ndoa yako kuanzia hivi sasa ni mdogo sana
 
Hivi mkimtendea mtu wema mnasubiri awakumbuke? Siyo mnatenda wema kwa faida yake?

Ewe mrembo fata roho ya mumeo wacha roho mbaya.

Hao hawakupunguzii riziki yako uliyopangiwa.

Hicho mlichonacho cha kuwapa ndugu zenu unafikiri mlikipata kwa uhodari wenu?
 
Dadaangu, ngoja nikupe mfano halisi, mimi nimelelewa na mama tu ambapo mama alikuwa na position nzuri kikazi kiasi kusoma shule nzuri ilikuwa sio tatizo, wala kuhudumia familia ilikuwa sio tatizo, (tumezaliwa wawili tu mimi na kaka yangu) kuna kipindi mama alihamishwa kikazi kutoka mkoa fulani akarudishwa kwenye mkoa alipozaliwa (kwao) hapo ndipo kimbembe kilipoanza, watoto wa dada zake , kaka zake, ndugu wengine wa mbali wote walikusanyika nyumbani kwasababu katika ukoo wao angalau mamangu alikuwa successful, ilikuwa inafika time familia inakuwa na watu 23, ikipungua inakuwa na watu 13-15. Uzuri mama alikuwa mkoani kwao kwahiyo alienda kijijini kwao kutafuta mashamba na vijana wasaidizi wa mashamba akawatafutia na sehemu ya kuishi (alikuwa na nyumba huko kijijini) kwahiyo chakula cha nyumbani kikawa kinatoka mashambani, hii ilisababisha ahueni ya maisha pale nyumbani,
Lakini kwa ukubwa ule wa familia matumizi ya pesa yalikuwa makubwa mno, kusomesha shule za private wengine walisoma za kawaida tu. Kiukweli mama alikuwa akionekana nje ana maisha mazuri lakini kwenye familia alikuwa akijibana mno.
Pamoja na yote aliyokuwa akiwafanyia ndugu ni mtu ambaye anaongoza kwa kusemwa na kulaumiwa kwenye ukoo wao, this looks funny I guess.
Matokeo ya hayo maisha mama mpaka ana staafu kazi alikuwa na maisha magumu mno, hakuwa amesave chochote wala hakuinvest chochote. Lakini pia wote aliowalea sidhani kama wanamkumbuka kwa chochote.
Hata nyumba yake ni ile ile aliyokuwa akiishi miaka yote, ikabidi mimi na kakaangu tushikane mashati tumjengee mama na tumtafutie hata kausafiri kake ka bei rahisi, hela ambazo tungeweza kufanyia maendeleo ya familia zetu.
Ndugu hawana aibu jamani na bado hadi sa hivi wengine wanampelekea vitoto (nakuwaga mkali kama mbogo nikiambiwa kuna kitoto kwa mama ) Wakati mama ili ale ni lazima mimi na kakaangu tutume hela na angalau kuna kabiashara tumemfungulia tumemuwekea na msichana huyo msichana ndiye anayeishi nae hadi sasa. Tatizo mamaangu nae mbishiiii, nikitaka kumchukua niishi nae anasema ye hawezi kuishi kwa watu hahaha!
Hiyo story yako ni reflection ya hii niliyokueleza kwahiyo akili kichwani kwako.
Ahsante sana mkuu! This is exactly what we r going through and definetly our destination will be like mom's!
 
Wala usimpigie

Ila jiandae kisaikolojia huyo binti nahisi atakuwa jipu

Ndugu jiwekee akiba ya mbeleni...kama huna kiwanja nunua sasa

Hao ndugu zake awahudumie mwenyewe na alishe familia........ utakuja baki mdomo wazi
Ahsante sana
 
Hivi mkimtendea mtu wema mnasubiri awakumbuke? Siyo mnatenda wema kwa faida yake?

Ewe mrembo fata roho ya mumeo wacha roho mbaya.

Hao hawakupunguzii riziki yako uliyopangiwa.

Hicho mlichonacho cha kuwapa ndugu zenu unafikiri mlikipata kwa uhodari wenu?
Ahsante pia kwa mchango wako
 
Ajira ngumu mkuu, nadhani unaielewa hali halisi ya ajira hapa nchini, so kuliko kukaa bure niliona bora nifanye kilimo na pia huwa nahangaika na biashara ndogondogo
Qualification yako ni nini
Kama msomi achana na kilimo tafuta ajira
Umueekee mtoto wako hakiba
 
Kuna wakati inabidi kufanya maamuzi magumu.

Na huo ndio wakati wenyewe. ..tabia ya mumeo ni kujifanya ana uwezo.

Na hii inatokana na juhudi zako za kuleta chakula ndio maana ana jeuri.

Hapo nyumba ikiwa na njaa wote hao wataaga mmoja mmoja wawaache peke yenu.

Kama kweli unataka wasiendelee kujazana Hapo jibu lipo wazi ACHA KULIMA
 
Na hawatokumbuka kama baba yake alimaliza nguvu zake kwa kuwahangaikia wao! Yaani hadi sielewi!
Thubutuuu yake!
Nani akumbuke wema wa baba yao au wako

Nina mifano hai, nae mume wa mama angu mdogo (mpare) alileta ukoo mzima kwake eti anasomesha!

Hao ndugu kwanza walimroga kaka yao akawa anamuona mama etu ka takataka, wee! ndoa ikamshinda akasepa na watoto wake watatu ( na kashaolewa na mtu mwingine) uzuri yy ni mwajiriwa,

Wale ndugu za mume wa mamdogo sasa hivi wamepata kazi, kaka yao katumbuliwa na ana BP + Kisukari! Hakuna hata anayemjali!

Yaani sasa hivi ni anajuta kinoma mke hana, kazi hana, hela hana, ndugu zake wamekula kona! Amekonda ka mshumaa!

( na bado ana skendo ya kumtoa kafara mtoto wao wa kike wa miaka 12 ili atajirike, na bado kaangukia pua)

Ila wapare hapana asee!
 
Muombe ruhusa ya kwenda kwenu kusalimia akikuruhusu, kaa mwezi mzima ili uone jinsi atakavyoulea huo ukoo wake. Pengine anataka kukutimua kijanja, si unaelewa tena akufukuzae hakwambii toka ni vitendo tuu.
Yaaani wewe una akili sana

Nimewaza hilo hilo coz (refer my quote hapo juu) kumbe hata mama angu mdogo mume wake alikuwa ameshamchoka ndo maana akamletea ukoo wote!

Ila mungu huyu jamani ukimuona huyo baba sasa hivi unatema mate chini!
 
Pole sana nimejitahidi kuvaa kiatu chako nimeshindwa una moyo wa peke ako mm nisingeweza ata kama kuwasaidia bora tuwasaidie wakiwa mbali
Shunie kuwasaidia ndugu si vibaya hata kidogo ni jambo linalopendeza!

Tatizo ni ile respond yao kwake! Hawatoi ushirikiano wowote wa kuzalisha yaani na kama mamizigo tu yanayosubiri kula!

Asee mi siwezi na nilivyo na fragile heart!

Huyu Dada asipochukua hatua madhubuti atakuja kulia kilio kibaya sana! Nimeshashuhudia haya mambo!
 
Mimi ni miongoni mwa vijana waliosomeshwa na baba Mdogo kuanzia sekondari hadi chuo kikuu na ndani alikuwa na watoto wa ndugu zake 13+ na mama mkewake alikuwa na watoto 2 tu. Sasa mateso ilikuwa kulima na hadi ziliota sugu mikononi na kwa kuwa nilihitaji kusoma nilikomaa sana na nilikuwa nikitoka shule jioni shambani.

My point is that; kama wangekuwa wanajielewa na kukusaidia shughuri za shamba na mambo mengine basi mambo yangeenda safi ila kwa hali hiyo naamini mnakaribisha umaskini huko mbeleni.

Jaribu kukaa nae ili nae akae na hao ndugu zake ili wafike shambani na kuongeza uzalishaji bila kufanya hivyo umaskini upo njiani.

Ikumbukwe kuwa katika nchi maskini duniani 70% ni zile ambazo zimekumbatia extended family. Sikatai kulea ndugu ila kama wazazi wao wapo basi wakae kwa wazazi wao na msaada wa kusomeshwa uwafuate huko mn kama hawana msaada wa kiuchumi basi inakera na soon as possible naiona ndoa yenu itagubigwa na wingu la ugomvi.
 
Daaah huo mbona mtihani mkubwa Sana,hebu jaribu kuacha kulima mwaka huu uone kitakachoendelea km na shamba hawataki kwenda unapotezaje nguvu ya kulisha mijitu mikubwa namna hiyo looh
 
Wandugu Salaam!
Mimi nipo kwenye ndoa miaka saba sasa na tuna mtoto mmoja, tunaishi nyanda za juu kusini.Tuliishi kwa amani miaka mitatu tu, tukiwa mimi na mume wangu na mtoto. Baada ya hapo imekua tabu, mimi kwetu kuna ahueni ya kiuchumi, yaani sitegemewi na wazazi wangu labda mimi ndio niombe msaada kwako. Lakini kwa upande wa mume wangu imekua tatizo yeye ndio anaetegemewa....yaani ndio star kwao. Sasa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio wategemezi wanazidi, watoto wa ndugu zake wa kuwasomesha ndio wanazidi, applicants wa misaada kutoka kwao ndio wanazidi wanaomba hata ambavyo wangeweza kujisaidia wenyewe kwa jinsi anavyowaendekeza. Anafanya bidii kuwatafuta watoto wa ndugu zake hata waliotelekezwa na wazazi wao tena wakingali hai anawajaza
home. Yote hayo ninayavumilia na ninapambana nayo.
Mimi sijabahatika kupata ajira tangu nimehitimu masomo yangu, yeye ndio ana ajira. Lakini mimi sijabweteka najishughulisha na kilimona hata chakula tunachokula (mpunga na mahindi) nalima mwenyewe. Sasa kila nikijaribu kumuelimisha kwamba sichukii kuwasaidia ndugu zake na hata kuwasomesha watoto wa ndugu zake bali kuwepo na namna ya kuwasaidia wakiwa makwao na si kuwajaza hapa home inaleta stress maisha yanazidi kuwa magumu...mwenzangu hataki tena ananichefua kwa kunijibu...ati kwani kuna shida gani mbona chakula kipo ndani, yaani hakuna shida ya chakula kabisaa! Hakika majibu haya yananivunja moyo kuendelea na kilimo, nawaza labda niache kabisa kulima ili nione kama ataweza kununua chakula cha kulisha familia kubwa namna hii.
Kubwa zaidi sasa na linalonichanganya hasaa na ninaomba ushauri wenu ndugu wana MMU; Ni kwamba kama vile hawa waliopo hapa home na tunaowasomesha huko makwao hawatoshi, sasa amemtafuta binti wa marehemu kaka yake ambae ana umri wa miaka 24 na ana watoto wawili, anataka amtoe huko anakoishi (anaishi mikoa ya Mashariki, anajishughulisha na kuuza bar, kwa mujibu wa maelezo ya baba mtu) aje tuishi nae hapa home. Nimemuuliza sababu ya kumchukua binti mkubwa kama huyo tena aliyezoea maisha ya bar; kanijibu anatanga tanga kwa sababu baba yake alikufa, ngoja aje tukae nae tuwasomeshe na hao watoto wake (binti kasema watoto wote hawana baba); hv ninapoleta uzi huu baba mtu kishaanza mchakato wa kutafuta shule kwa ajili ya mtoto (mjukuu) mkubwa ambae ana miaka sita. Anamtafutia private school aanza chekechea mwakani. Kazi anayofanya ni ya kipato cha kawaida kiasi kwamba misaada imezidi uwezo (wanadrain) mara nyingi tunabaki hatuna hata senti tano! Hata ninapofurukuta kwa kufanya biashara ndogondogo mbali na kilimo najikuta mtaji unakata, nabaki kuzubaa tu!
Sasa jamani mwenzenu kama binadamu, tena kijana mwenye ndoto za maisha ya mbeleni nashindwa la kufanya, naishiwa hamu ya hii ndoa yangu, natamani nitoke nikapange na mwanangu nipambane kivyangu lakini tena roho inanisuta! NIPO NJIA PANDA, nifanyeje jamani na tabia ya mwanaume huyu! Na hasa huyu binti na watoto wake, natamani nipate namna nyingine ya kumsaidia lakini asije hapa home coz tayari tupo kumi hadi sasa, na hiki ni kipindi cha likizo huwa tunafika mpaka kumi na tano na haya ni maisha ya mjini (u can imagine)!! Msaada jamani!
Nawaomba wale wanaolete mizaha wapite kimya coz nahisi wataniongezea stress

Elewaneni kwa amani
 
Pole sana dada kwa hayo yalokukuta, shida kubwa hapo ni kutokujitambua na kupenda sifa. Hakuna kusaidia kwa namna hiyo bali ni kupumbaza watu, kuwadekeza huku akiiumiza familiya.

Kusaidia siyo kubaya ila saidia mtu kwa kumtegemeza mwenyewe yaani kama kumpatia mtaji afanye biashara itakayomsaidia yeye na familia yake, kumtafutia shamba alime asaidie familia yake, amtafutie kazi itakayomuingizia kipato cha kuendesha familia yake. Huku ndiko kusaidia kunakopungiza tegemezi, yeye naona anaongeza tegemezi badala ya kupunguza, mwisho wa siku atawafanya watu washindwe kuendesha maisha yao wenyewe kwa kulemaa na misaada.

Hata maandiko matakatifu hupinga sana uvivu, asiyefanya kazi na asile, watu wafanye kazi kadri iwezekanavyo ili nao wasaidie watu wengine siyo wao tuu ndo wameumbiwa kusaidiwa.

Cha kufanya: zungumza na mwenzi wako kwa upole na upendo mkubwa ukimwelimisha ubaya wa anachokifanya kwa sasa na baadae kisha toa mtazamo wako wa namna nzuri ya kusaidia ndugu na jamaa huku familia yenu ikibakia kuwa na furaha na amani.

Mungu akutie nguvu na kuwapatia hekima na maarifa ya kumaliza jambo hili.kwa uzuri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom