Ndoa chungu, ndugu wamezidi, nishauri nifanyeje?

Yaani kama ulikuwepo vile, coz kuna wengine wakubwa nawazidi labda miaka mitatu hv; basi wanataka nao wajipangie utaratibu wao; mwingine anataka anywe chai lita nzima pekeake, mwingine msosi anataka arudie full plate hata mara tatu, nikisema niwapeleke shamba wanapiga simu kwa Mr ati wanaumwa wanataka kurudi, nabaki napiga kazi mwenyewe, basii duuuh, stress za kila rangi!
Haaaaaa hapana dada hiyo its too much!!! Hapo machokifanya n sawa na huruma za mshumaaaa!!! K ukweli wote familia zetu n tegemez lakin mmeo anaendekeza!!! Watu kumi uwaleee wew!?? Hapana akuonee na huruma na wew una wazaz!! Sikushaur ufanye nn ila ukiona mzigo mzito achana nao utakuua siku c zako!! Kwenu hukuua mama!! Binafs nimekuonea huruma!!! Kama n somo la uchoyo ulifel kabisa!!! Mungu akubariki kwa moyo huo,,,,lakin wema usizid uwezo!!!
 
Huwez jua nani atakuja kukusaidia siku za mbelen(labda uzeeni).Huenda ni katka hao hao.Wasaidien tu dada angu kwanza maisha yenyew tunapta kila kitu tutakiacha
Moja, Umewahi kuishi na ndugu wangapi maximum kwenye nyumba yako ambapo wwwe ndo unagharamia mahitaji yote?

Mbili, Ndugu hao walikuwa wanakupa ushirikiano au ndo ndugu mzigo kuamka saa 3 asb kazi hataki kufanya ila msosi kama kawa

Tatu, Inahitajika extraordinary heart kumudu hii kitu labda tu kama tunaongea bila kuvaa viatu hivyo.

Mwisho, concern ya dada si kutokuwasaidia bali ikiwezekana wasaidiwe wakiwa huko walipo kama vile kutuma ada, kuwapa mitaji nk unless kama kuna umuhimu mkubwa sana wa wao kuja nyumbani
 
Bora nionekane na roho mbaya, sina moyo huo. Pole sana sista, ukiolewa/ukioa familia duni kiuchumi, tegemea yote hayo, kuishi na lundo la watu ndani, kusomesha ndugu na kutoa misaada kila kukicha.

Mtu anaolewa/anaoa anakuja na wadogo zake, watoto wa dada na kaka zake, hapo ndio mmeanza maisha, unadhani mtaendelea kweli? I don't do that, bora nionekane roho ya korosho tu.
 
sijui imani yako ila kuna sehemu nilisoma inasema hivi, AMETAPANYA AMEWAPA MASKINI..thawabu yake itaambatana naye.. KUTOA NI MOYO. huwezi jua hicho kilimo na hyo kazi aliyokuwa nayo Mungu amewapa ili msaidie hao ndugu zake. vitu vingine huwa hatutazami kwa jicho la tofauti.
wakati npo sekondari tulikuwa tunaishi na ndugu kibao walisomeshwa na mzazi wengine walikuwa nyumbani na wengine huko waliko, kuna siku moja niliumwa mbaya njiani nkiwa kwenye mishe mishe nkapelekwa kinondoni hosptal na kondata wa daladala ambaye alikuwa anamgonga binamu yangu wakati anasoma.
sijui nimekushauri au nimetok upupu.
 
Kuna dada mmoja pale mwanza aliikimbia ndoa yake kwa sababu ya hao hao ndugu

Eti watu watano wanatoka kijijini 300km kumleta mgonjwa mmoja bugando ambaye angeweza kuletwa na mtu mmoja au wawili

Walikuwa wanaenda ndugu pale ambao hata kitafuta lineage lazima koo 4 zihusike ili uje upate undugu wake na wewe

Bora hata hao ndugu wawe cooperative ndo kwanza walikuwa wanamtia stress asubuhi mpaka jioni

Mwishowe wakawagombanisha yeye na mumewe, akajiondokea
 
Huyo ni chaguo lakoooo,chaguo lako hata kama......
Ila mkuu pole bhana mi sitaki Fanya kosa la kuolewa na MTU kikwete kwao,utajitahid mwanzoni baadae hutashindwa.
 
Kusaidia ni vyema ila msaada usizidi uwezo....... msaada usiumize wengine...msaada usifanye ushindwe kuhudumia damu yako.


Sasa inaonekana mumeo mshahara wake hauna majukumu makubwa kutokana na wewe kumsaidia......

Sasa.... (nakushauri kwa mujibu wa maelezo yako...changanya na zako)


1. Jaribu kutafuta solution kabla hujakimbia nyumba hivyo:-

2. Usiache kulima, bali unacholima kiasi kidogo ndio kiingie nyumbani. Ukiweza hifadhi hukooooo uuze na kikufae wakati wa dhiki

3. Ukiuza fungua akaunti yako binafsi uhifadhi. Ujipe malengo kama kununua kiwanja na kuwekeza kwa siku za taabu....believe me mkikosa kipato leo hao ndugu hamtawaona

4. It seems like mumeo hana majukumu (kama kipato chake ni cha kawaida).
Hivyo mpe majukumu .... kuanzia
- ujenzi (kama hamjanjenga)
- bajeti ya nyumba, 100% aikave mwenyewe...si anajua huna ajira??????
-hgs
-ada za wanao na iwe shule za maana sio st kayumba
-huduma zako

5. Hao ndugu wape majukumu...hakuna kukaa bure....wazalishe (kama kuna wakubwa) na wafanye kazi zote za ndani....kuwe na discipline.....mfano walime mbogamboga kutengeneza bajet...watwange mahindi au kukoboa mpunga ili msave

6. Endelea kumshauri mwenzako wakati mwingine ni vyema kusaidia ndugu walipo. Watu wanapojazana mnawalindaje watoto? Kumbuka wanaobaka watoto na kuwafanyia vitendo viovu asilimia kubwa ni ndugu.....

Tabia za watoto mnazijengaje kama kuna watu wa kila aina wenye tabia zao?????

Mnavyotoa tu mnaweza kuwekeza??????

Binti wa miaka 24 anayejitegemea kumtoa aliko ni akili kweli?????


Yaani hapo ukilima na kuvuna ndugu zihifadhiiiiiii zitakufaa...... angalia kesho yako. Ndugu wanaweza kusepa hao wewe na mumeo mtaishije kama hamna cha kujishikiza? Ajira huwa zinaisha alishawaza ajira ikiisha hata ghafla mtaishije????

Hakatazwi kusaidia kwao ila lazima kwake pia ajijenge na kuandaa kesho ya wanae
 
Yaani kama ulikuwepo vile, coz kuna wengine wakubwa nawazidi labda miaka mitatu hv; basi wanataka nao wajipangie utaratibu wao; mwingine anataka anywe chai lita nzima pekeake, mwingine msosi anataka arudie full plate hata mara tatu, nikisema niwapeleke shamba wanapiga simu kwa Mr ati wanaumwa wanataka kurudi, nabaki napiga kazi mwenyewe, basii duuuh, stress za kila rangi!
Zungumza na mumeo.
Mnapowapa kazi na yeye anazipangua maana yake ni nini?

Kula waache wale mpaka wanye mezani.
Ila weka utaratibu

Chai kuanzia saa 12:00asbh mwisho kunya ni saa 9:00 asubuji. Hujanywa ndani ya mida hiyo piga pasi ndefu.

Lunch ni kuanzia saa sita mchana hadi saa nane

Dinner kati ya saa kumi na mbili jioni hadi saa mbili
(Chakula lazima mle pamoja..... inapotokea sababu ya msingi.mtu hayupo ndio mida hiyo inahusu)

It's your house your rule

Na wakumbushe asiyefanya kazi asile

Mkiishi na watu wengi halafu mmoja akawaendekeza anakujengea uadui na haiketi discipline!!!!!!
 
Wandugu Salaam!
Mimi nipo kwenye ndoa miaka saba sasa na tuna mtoto mmoja, tunaishi nyanda za juu kusini.Tuliishi kwa amani miaka mitatu tu, tukiwa mimi na mume wangu na mtoto. Baada ya hapo imekua tabu, mimi kwetu kuna ahueni ya kiuchumi, yaani sitegemewi na wazazi wangu labda mimi ndio niombe msaada kwako. Lakini kwa upande wa mume wangu imekua tatizo yeye ndio anaetegemewa....yaani ndio star kwao. Sasa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio wategemezi wanazidi, watoto wa ndugu zake wa kuwasomesha ndio wanazidi, applicants wa misaada kutoka kwao ndio wanazidi wanaomba hata ambavyo wangeweza kujisaidia wenyewe kwa jinsi anavyowaendekeza. Anafanya bidii kuwatafuta watoto wa ndugu zake hata waliotelekezwa na wazazi wao tena wakingali hai anawajaza
home. Yote hayo ninayavumilia na ninapambana nayo.
Mimi sijabahatika kupata ajira tangu nimehitimu masomo yangu, yeye ndio ana ajira. Lakini mimi sijabweteka najishughulisha na kilimona hata chakula tunachokula (mpunga na mahindi) nalima mwenyewe. Sasa kila nikijaribu kumuelimisha kwamba sichukii kuwasaidia ndugu zake na hata kuwasomesha watoto wa ndugu zake bali kuwepo na namna ya kuwasaidia wakiwa makwao na si kuwajaza hapa home inaleta stress maisha yanazidi kuwa magumu...mwenzangu hataki tena ananichefua kwa kunijibu...ati kwani kuna shida gani mbona chakula kipo ndani, yaani hakuna shida ya chakula kabisaa! Hakika majibu haya yananivunja moyo kuendelea na kilimo, nawaza labda niache kabisa kulima ili nione kama ataweza kununua chakula cha kulisha familia kubwa namna hii.
Kubwa zaidi sasa na linalonichanganya hasaa na ninaomba ushauri wenu ndugu wana MMU; Ni kwamba kama vile hawa waliopo hapa home na tunaowasomesha huko makwao hawatoshi, sasa amemtafuta binti wa marehemu kaka yake ambae ana umri wa miaka 24 na ana watoto wawili, anataka amtoe huko anakoishi (anaishi mikoa ya Mashariki, anajishughulisha na kuuza bar, kwa mujibu wa maelezo ya baba mtu) aje tuishi nae hapa home. Nimemuuliza sababu ya kumchukua binti mkubwa kama huyo tena aliyezoea maisha ya bar; kanijibu anatanga tanga kwa sababu baba yake alikufa, ngoja aje tukae nae tuwasomeshe na hao watoto wake (binti kasema watoto wote hawana baba); hv ninapoleta uzi huu baba mtu kishaanza mchakato wa kutafuta shule kwa ajili ya mtoto (mjukuu) mkubwa ambae ana miaka sita. Anamtafutia private school aanza chekechea mwakani. Kazi anayofanya ni ya kipato cha kawaida kiasi kwamba misaada imezidi uwezo (wanadrain) mara nyingi tunabaki hatuna hata senti tano! Hata ninapofurukuta kwa kufanya biashara ndogondogo mbali na kilimo najikuta mtaji unakata, nabaki kuzubaa tu!
Sasa jamani mwenzenu kama binadamu, tena kijana mwenye ndoto za maisha ya mbeleni nashindwa la kufanya, naishiwa hamu ya hii ndoa yangu, natamani nitoke nikapange na mwanangu nipambane kivyangu lakini tena roho inanisuta! NIPO NJIA PANDA, nifanyeje jamani na tabia ya mwanaume huyu! Na hasa huyu binti na watoto wake, natamani nipate namna nyingine ya kumsaidia lakini asije hapa home coz tayari tupo kumi hadi sasa, na hiki ni kipindi cha likizo huwa tunafika mpaka kumi na tano na haya ni maisha ya mjini (u can imagine)!! Msaada jamani!
Nawaomba wale wanaolete mizaha wapite kimya coz nahisi wataniongezea stress
Kama kweli unajiamini ww ni jembe,mpe conditions zako achague yeye either kusuka au kunyoa

Haiwezekani azidi tu kuiongezea familia mzigo Afrika shida ndio asili yetu yeye hata afurukute vp hatoweza kuzimaliza anatakiwa ajue tu kuwa unatakiwa usaidie unapoweza tu
 
Hapana kwa kweli, huyu dada angekuwa na roho mbaya wasingekaa hapo, omba ruhusa uende kwenu ukae huko mwezi hata mmoja, ukirudi muda wa kilimo tayari usilime kaa uone chakula kilichopo kikiisha atamudu kuhudumia lifamilia lote hilo? Anza biashara uwe busy na mambo yako, hapo wamekufanya chuma ulete tu utashindwa hata kupata maendeleo sababu ya upendo wa mshumaa unamulika huku unaungua
 
Hapana kwa kweli, huyu dada angekuwa na roho mbaya wasingekaa hapo, omba ruhusa uende kwenu ukae huko mwezi hata mmoja, ukirudi muda wa kilimo tayari usilime kaa uone chakula kilichopo kikiisha atamudu kuhudumia lifamilia lote hilo? Anza biashara uwe busy na mambo yako, hapo wamekufanya chuma ulete tu utashindwa hata kupata maendeleo sababu ya upendo wa mshumaa unamulika huku unaungua
 
Pole sana dada yangu.
NILICHOGUNDUA
-Ninyi ni wakulima
-Mnaendesha maisha kwa kutegemea mazao mliyovuna ya ghalani.
-Hamtegemei biashara
-Kinachokukwaza juu ya mumeo ni kitu kimoja tu,ndugu zake,hamna kingine.
USHAURI.
-Kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye anayewajaza,usitoe akiba yako yote kuhudumia.
-Hata siku ikitokea mnakaribia kushinda/kulala njaa,usitoe akiba yako yote.
-Fanya biashara zako kwa siri,asizijue,ili akiba yako izidi kutuna.
-Mkalishe chini umueleze
√ maisha ya siku hizi siyo kama ya zamani.
√ maisha yenu ya uzeeni itakuwaje
√ mboreshe kilimo kwa kutumia zana za kisasa kama trekta.
√ ndugu zake wanaokuja ni rasilimali kazi tosha msimu wa kilimo.
√ mazao machache ghalani bila pesa si kitu
√ thamani ya mazao yote ya ghalani na idadi mliyopo ndani ni sawasawa na masikini wa kutupwa.
Ahsante sana kwa ushauri wako, very analytical, stay blessed!
 
Back
Top Bottom