Ndio hivyo tena, tumeikosa. Dangote

Ndio hivyo tena, tumeikosa. Dangote

Dangote hajawa tajiri kwa kuendekeza ujinga. Kenya wanatarajia kuanza kuvuna mafuta yao mwishoni mwa mwaka huu kutoka South Lokichar Basin, Turkana. Aidha, South Sudan ni mzalishaji mkubwa wa mafuta. Sasa hivi wanasafirisha mafuta hayo kupitia Sudan ambayo imegubikwa na vita. Alternative ya kuaminika kwao ni kuyasafirisha kupitia Kenya. Kwa hiyo refinery hiyo italishwa na mafuta yao wenyewe na ya kutoka South Sudan. Aidha, mazao yake yatapata soko sio Kenya tu bali mpaka Ethiopia, nchi ambayo uchumi wake unakua kwa kasi sana. Na muhimu kuliko yote ni kuwa amewekeza tayari Tanzania na anajua changamoto zetu kwenye biashara. Changamoto kama wana siasa kuingilia utendaji, sheria zisizo eleweka, wizi uliokithiri n.k.). Kwa hali hiyo hauwezi kumlaumu kwa kuona kuwa atafaidika zaidi akiwekeza Kenya kuliko Tanzania.

Badala ya kujaribu kumshawishi tuboreshe mazingira ya kufanya biashara na tuwafunge gavana za spidi wana siasa wetu.

Amandla...
Sahihi sahihi nakumbuka awamu ya nne mwisho mwisho kuna mikataba ilipitishwa kwa hati ya dharura mwishoni bungeni kama 19 lakini ndio kipindi kiwanda kinaanza lakini kama ujuavyo wizi mwingi 10% baada tu ya kubadilika utawala timbwili likaanza mara Dang'ote abadilishe awe anatumia gesi kumbe kuna wajanja tayari wanamiliki hilo bomba tayari. Kwahiyo kugoma kuwekeza tena Tanga ashafanya risk analysis hasa kwa siasa zetu zisizotabilika kwenye masuala ya biashara ashaona hatuna viongozi wako makini kwenye hilo hivyo kina Kitila kwenda kupeleka kinyago haikusaidia maana ashatendwa hapo nyuma
 
Dangote hajawa tajiri kwa kuendekeza ujinga. Kenya wanatarajia kuanza kuvuna mafuta yao mwishoni mwa mwaka huu kutoka South Lokichar Basin, Turkana. Aidha, South Sudan ni mzalishaji mkubwa wa mafuta. Sasa hivi wanasafirisha mafuta hayo kupitia Sudan ambayo imegubikwa na vita. Alternative ya kuaminika kwao ni kuyasafirisha kupitia Kenya. Kwa hiyo refinery hiyo italishwa na mafuta yao wenyewe na ya kutoka South Sudan. Aidha, mazao yake yatapata soko sio Kenya tu bali mpaka Ethiopia, nchi ambayo uchumi wake unakua kwa kasi sana. Na muhimu kuliko yote ni kuwa amewekeza tayari Tanzania na anajua changamoto zetu kwenye biashara. Changamoto kama wana siasa kuingilia utendaji, sheria zisizo eleweka, wizi uliokithiri n.k.). Kwa hali hiyo hauwezi kumlaumu kwa kuona kuwa atafaidika zaidi akiwekeza Kenya kuliko Tanzania.

Badala ya kujaribu kumshawishi tuboreshe mazingira ya kufanya biashara na tuwafunge gavana za spidi wana siasa wetu.

Amandla...

..hazina ya mafuta ya Kenya ni ndogo sana ukilinganisha na Uganda.

..mafuta ya South Sudan sikuyafikiria kama chanzo cha refinery ya Lamu.

..Nakushukuru kwa kuiweka mezani hoja ya mafuta ya South Sudan.

..kwa upande mwingine, Lamu haijafikiwa na bomba la mafuta ghafi. Tanga inatarajia kufikiwa na bomba la mafuta ghafi hivi karibuni.

..Nilitarajia uwepo wa bomba la mafuta kitakuwa kigezo muhimu ktk maamuzi ya Aliko Dangote.
 
Kuna mpango tayari wa kujenga bomba kati ya South Sudan na Lamu ( LAPPSET project). By the time refinery inakamilika, pipeline nayo itakuwa tayari. Wakati huo huo itaweza kusafisha mafuta yanayoletwa kwa meli.
Changamoto nyingine kuhusu hii pipeline ya kutoka Uganda hadi Tanga ni madai ya uharibifu wa mazingira na haki za raia waliokuwa wanaishi katika maeneo linapopita. Shutuma hizi zinaweza hata kuathiri access yake kwenye soko la nchi za magharibi. Hizi unknowns zitamfanya investor makini yeyote kusita.

Amandla...
 
..hivi hakuna uwezekano wa kujenga bomba toka South Sudan mpaka Hoima-Uganda?

..kwa hiyo bomba jipya likawa South Sudan -- Uganda -- Tanzania.

..wakifanikisha hilo Dangote itabidi akae.

Cc Fundi Mchundo
Sio rahisi. Lamu ni karibu zaidi na linapita nchi moja tu sio mbili. Na hali ya usalama kaskazini mwa Uganda haiaminiki sana. Aidha, ukiangalia mazingira ya kisiasa katika nchi hizi tatu Kenya wako stable zaidi. Na mfumo wa sheria wa Kenya unaaminika zaidi kwenye kulinda haki za investor kuliko ya Tanzania na Uganda.

Kumbuka Tanzania Mkuu wa Wilaya, Mkoa na Waziri wote wanajiona wana haki ya kumuingilia investor. Na bila shaka Dangote ana experience ya huo usumbufu Tanzania.

Amandla...
 
..hazina ya mafuta ya Kenya ni ndogo sana ukilinganisha na Uganda.

..mafuta ya South Sudan sikuyafikiria kama chanzo cha refinery ya Lamu.

..Nakushukuru kwa kuiweka mezani hoja ya mafuta ya South Sudan.

..kwa upande mwingine, Lamu haijafikiwa na bomba la mafuta ghafi. Tanga inatarajia kufikiwa na bomba la mafuta ghafi hivi karibuni.

..Nilitarajia uwepo wa bomba la mafuta kitakuwa kigezo muhimu ktk maamuzi ya Aliko Dangote.
Sababu nyingine ni mafuta mengi offshore Somalia washaanza kuchimba kupitia waturuki. Na Lamu siyo mbali
 
Lakini sisi ni watu waajabu. Tuna gesi kibao kusini. Msumbiji nao wana gesi nyingi kuliko sisi. Tulipaswa kuendeleza Lindi kama sehemu ya kuchakata na kusafirisha gesi yetu na ya Msumbiji. Majadiliano yalifika mbali tukayapiga stop. Saa hizi tungekuwa mbali sana. Tunatanguliza mno siasa.

Amandla...
 
Ndio hivyo tena, tumeikosa.

Dangote ameiambia BBC, ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta katika mji wa Lamu nchini Kenya utaanza Oktoba 2026. Ujenzi utagharimu Dola za Kimarekani bilioni 15.5 badala ya bilioni 20 zilizotajwa awali. Upungufu wa gharama umetokana na uzoefu wa kujenga kiwanda kama hicho kule nchini Nigeria.

Nawasilisha!
Dr. Chris Cyrilo.
Mwache Dangote ajenge refinery yake Lamu, na sisi na Uganda tuendelee na mpango wetu tujenge refinery yetu Tanga, unless kama crude oil ya Uganda, itatosha ku feed refineries zote mbili to the full capacity na ziada yauzwe nje, ni refinery yetu ndio ita make profits, kwasababu hiyo ya Dango te itamlazimu ku import crude ndipo asafishe wakati yetu ni tunakinga tuu kutoka bombani!.
P
 
Sababu nyingine ni mafuta mengi offshore Somalia washaanza kuchimba kupitia waturuki. Na Lamu siyo mbali

..Somalia na Uturuki bado wako katika hatua ya utafutaji, hawajaanza kuchimba.

..Pia Kenya hawajaanza kujenga bomba la kutoa mafuta Turkana kupeleka Lamu.

..South Sudan akijenga bomba mpaka Hoima Uganda, ili kuunganisha kuja Tanga, mradi wa refinery Lamu utakuwa na wakati mgumu sana.

..Nadhani suala hili limemtibua Museveni kuliko Samia kwasababu mafuta siyo ya Tanzania, mafuta ni ya Uganda.
 
Nadhani suala hili limemtibua Museveni kuliko Samia kwasababu mafuta siyo ya Tanzania, mafuta ni ya Uganda.
 
Halafu cha kuchekesha, ukiangalia bajeti yetu ya nishati, hakuna hata dalili ya hiyo Tanga Energy Hub hadi walipochelewa kushtuka. Ni too little, too late. Unasubiri Dangote atangaze Lamu ndio unakimbilia kusaini MoU na Uganda kama unafanya dharura ya msiba.
Refinery ilikuwa lazima ijengwe Tanga, watanzania tukiwa na sifa ya kupinga kinachofanywa na serikali yetu haraka sana tukaanza kumpigia promotion Dangote bila ya kujua nini haswa ambacho serikali inaweza kukifanya chenye faida kwa miaka mingi ijayo.
 
Nauliza tu Dangote alikataa ile 10% ya uchochoroni nini ?
Mama alizingua kwa kauli yake hata mimi ningekuwa Ruto ninge mind.

Yaani unamsogezea mtu chakula, anaanza kuuliza kwanini mmepika bila yeye kuwepo (tena kwa ukali).

My take: Ruto alikuwa anamzawadia mama ajisafishe na 29 badala yake ika back fire.
Baada ya hotuba ile ya Ruto mama alitakiwa pale pale awakaribishe asiwape nafasi ya kubadili mawazo.
 
..hazina ya mafuta ya Kenya ni ndogo sana ukilinganisha na Uganda.

..mafuta ya South Sudan sikuyafikiria kama chanzo cha refinery ya Lamu.

..Nakushukuru kwa kuiweka mezani hoja ya mafuta ya South Sudan.

..kwa upande mwingine, Lamu haijafikiwa na bomba la mafuta ghafi. Tanga inatarajia kufikiwa na bomba la mafuta ghafi hivi karibuni.

..Nilitarajia uwepo wa bomba la mafuta kitakuwa kigezo muhimu ktk maamuzi ya Aliko Dangote.

mafuta ya uganda siyo sababu ya uamuzi wa kujenga refinery hata kwa upande wa tanzagiza, nafikiri sababu ya kujenga refinery ni pia kuwa msambazaji petroleum products kwenye nchi ambazo hazina uwezo wa ku-refine mafuta ghafi i.e watakuwa wana-import mafuta ghafi pia ktk nigeria, gulf states au other oil producing countries na ku-refine halafu kuuza kwingineko kama vile india anavyofanya, mafuta yetu leo hii yanatoka india huko ndiko tunakonunua na siyo gulf states, india ndiye anayenunua mafuta ghafi ktk gulf states au hata iran anafanya refining na ku-export finished products kwetu hata kenya wana-import sehemu kubwa tu ya mafuta yao ktk india.

hivyo lengo la kujenga refinery linajumuisha hilo pia na siyo tu mafuta ya uganda, hakuna atakayekubali kuwekeza hela yake kujenga refinery kutegemea mafuta ya uganda kwani hailipi btw uwezo wa kuagiza mafuta ghafi tulikuwa nao tiper yetu ilikuwa inafanya refining ya mafuta ghafi mpaka 30% ya matumizi yetu ya ndani hivyo ilikuwa ni swala la kuwekeza tu zaidi tiper na leo hii tungekuwa mbali sana lkn kama kawaida waliua tiper na leo hii wamegeuza matanki ya kuhifadhia imports ktk india, hivyo ukinuliza mimi ni kwamba tunarudi nyuma, na ukitaka kujua nani aliua tiper angalia nani anatawala biashara ya kuagiza mafuta ktk india na ndiyo maana waliua tiper halafu the same people mnategemea wafanye maamuzi kwa manufaa ya nchi? hawa wote oilcom, lake oil &co. waliibuka baada ya tiper kufa halafu wanajiita self made billionaires ...
 
Back
Top Bottom