Ndege yatolewa majini Bukoba

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
72,997
Reaction score
102,836
Hii ndege kwa jinsi ilivyobondeka mbele, haikuwa 'runway overshoot', yawezekana palikuwa na shida, ni wakati uchunguzi wa makini ufanyike.

Ni kama 'imestall'. Aliyesema alifanya mawasiliano na marubani aliwasiliana nao kwa njia gani? Maji yamewaanza marubani kwanza.

Hiyo athari kutokana na hizi picha yaonesha wengi wamekufa kabla ya maji kuwakuta kutokana na kuvunjika viungo.

 
Hata wale waokoaji waliozamia ndani ya ndege walisema hilo.
Walisema walikuta wengine washakata moto, wana majeraha usoni na wengine mikanda ilikua imewabana so walifirukuta hapo mpka wakakata moto, hasa waliokua wamekaa mbele.
 
Eeeh Mungu
Hii si ajali ya kawaida

Mbona kama imebondwa ama iligonga mwamba?

maharage ya ukweni ulisema hii kitu
 
Mzigo ni kama uli pigwa mtama hewani uka shukia kichwa.alie kua ana wasiliana na rubani sijui waliongeaji apo
Ingeshukia kichwani, hiyo sehemu yote ya mbele na juu ingekuwa imeharibika sana. Lakini iko almost intact. Lakini ukiangalia vizuri, uharibifu mkubwa umetokea sehemu ya mbele KWA CHINI.

Hii inaonesha kwamba ilikuwa katika harakati za kutua. Sehemu ya mbele ikajiburuza chini (kwenye kina kifupi cha maji), ikapinda na kusababisha upande wa nyuma kuning'inia (kuelea) juu ya maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…