Ndege yaanguka ziwa Manyara

Ndege yaanguka ziwa Manyara

wakyagara wakinyora

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Posts
735
Reaction score
288
Ndege ya kampuni ya Tanzanair iliyokuwa ikitokea Bukoba kuelekea Zanzibar,imeanguka hivi punde katika ziwa Manyara.

Mpaka muda huu bado inaelea majini,abiria wote sita pamoja na pilot wa saba bado wamo ndani ya ndege.

Taarfa za hivi pundei zinasema kuna boti imetoka Serena kwenda kuwaokoa.

Nitaendelea kuleta up

Chanzo: Niko na mtu ambaye anawasiliana na mmoja wa abiria waliomo ndani ya ndege hiyo.

Bado haijafahamika chanzo cha ndege hiyo kuanguka.mmoja kati ya abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni wakili protaz ishengoma.boti inayokwenda kuwaokoa imeshawaona lakini bado haijawafikia

Abiria wote wameokolewa,Mungu ni mkubwa.Pilot aliomba kubadili mwelekeo atue Arusha kwa dharura ikashindikana kuwahi akatua ziwani.
 
Asante kwa taarifa mkuu, tumepata habari hii lakini hatukuwa na uhakika wa idadi na correct destination, tulikuwa tunajua inatoka bukoba dar. Waiting for more updates. "over and out"
 
Nawapa pole waliopata hio ajali. Lakini ufike wakati sasa ufanyike uchunguzi wa kina kujua chanzo cha hizi ajali za ndege hasa ukanda huo manake kuna nyingine ilianguka recently
 
Duh tatizo nini ...?
Lakini kwenye maji kama pilot ni mzoefu ni safe than on ground pasiwe na mamba wala watu tu....!
 
Jitihada za haraka zifanyike kuwaokoa hao manusura kabla hali haijawa mbaya zaidi
 
kama ni habari za kweli, Mungu awasaidie waliokuwemo kwenye ndege hiyo.
 
Bado haijafahamika chanzo cha ndege hiyo kuanguka.mmoja kati ya abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni wakili protaz ishengoma.boti inayokwenda kuwaokoa imeshawaona lakini bado haijawafikia
 
....

.... walio design uwanja wa Manyara walikuwa na akili kweli kweli!!!!
 
Ndege ya kampuni ya tanzanair iliyokuwa ikitokea bukoba kuelekea zanzibar,imeanguka hivi punde katika ziwa manyara.mpaka muda huu bado inaelea majini,abiria wote sita pamoja na pilot wa saba bado wamo ndani ya ndege.taarfa za hivi karibuni zinasema kuna boti imetoka serena kwenda kuwaokoa.
Nitaendelea kuleta updates
source:niko na mtu ambaye anawasiliana na mmoja wa abiria waliomo ndani ya ndege hiyo.
ok, taarifa zimefika.
swali langu:mbona ndege ata ikijikwaluza tu na watu wawili inaonekan"big issue" kweli mpaka breaking newz...mara habari zilizotufikia hivi punde, lakini huko kwenye gari zetu za mkaa , au dala dala, au za mnadani zinamwaga abiria wa kutosha huwa inaoenekana ishu "minor" sana , hivi kwanini wa tz tunazikweza xana wakati kuna vyombo vya usafiri vinamajnga zaidi ya hivyo vindege vyetu. ni hayo tu.
 
Mwenyenzi MUNGU mwingi wa Rehema uwasadie hawa Ndugu zetu!

Mkuu turudishie newz mkubwa kama wameokolewa ama!
 
ok, taarifa zimefika.
swali langu:mbona ndege ata ikijikwaluza tu na watu wawili inaonekan"big issue" kweli mpaka breaking newz...mara habari zilizotufikia hivi punde, lakini huko kwenye gari zetu za mkaa , au dala dala, au za mnadani zinamwaga abiria wa kutosha huwa inaoenekana ishu "minor" sana , hivi kwanini wa tz tunazikweza xana wakati kuna vyombo vya usafiri vinamajnga zaidi ya hivyo vindege vyetu. ni hayo tu.

Nauli yako na wao inafanana?
 
Back
Top Bottom