Wee na akina sie ndio Omujubi ametuambia ni lile kundi la watu wanaofikiria kidogo au hatupotezo muda kabisa kufikiria, sasa tutawezaje kufikiria habari za tanzaniair, zanair, eagle air n.k? Wacha tusikilizie new Challenge au Sumri ndio saizi yetu kaka.Duh, nilifikiri mwandishi amekosea tu kuandika, kumbe kweli kuna shirika la ndege linaitwa tanzanair? Sijawahi kulisikia.
Naam, bila shaka. Hii ni fani ambayo haitaki kuingiliwa. Kuna Rubani mmoja wa Air Tanzania alitua kwenye majani Oman miaka ile ya Air Tanzania ya kweli baada ya tairi kugoma kufunguk, na abiria wote walisalimika bila majeruhi. Hao ni marubani ambao walikuwa trained jeshi, Entebbe then Russia au Cuba kabla hajapewa ndege. Nashangaa siku hizi eti kuna vyuo vya urubani hadi 'Tabata Magengeni' na vinaachwa tu. tutarajie maafa makubwa huko tuendako?huyo rubani ni jinias
Nimepokea taarifa hizi kutoka huko arusha lakini sina uhakika, na kwa kuwa hapa ndo kwao na uhakika, kama kuna mtu ana data kamili atujuze.
Lawrence (Lau) Masha ‏@laumasha2hNdege ya kampuni ya Tanzanair iliyokuwa ikitokea Bukoba kuelekea Zanzibar,imeanguka hivi punde katika ziwa Manyara.
Mpaka muda huu bado inaelea majini,abiria wote sita pamoja na pilot wa saba bado wamo ndani ya ndege.
Taarfa za hivi pundei zinasema kuna boti imetoka Serena kwenda kuwaokoa.
Nitaendelea kuleta up
Chanzo: Niko na mtu ambaye anawasiliana na mmoja wa abiria waliomo ndani ya ndege hiyo.
Nawapa pole waliopata hio ajali. Lakini ufike wakati sasa ufanyike uchunguzi wa kina kujua chanzo cha hizi ajali za ndege hasa ukanda huo manake kuna nyingine ilianguka recently
Tukio lolote linaripotiwa jomba!!!wacha kulalamika kitabaka!ok, taarifa zimefika.
swali langu:mbona ndege ata ikijikwaluza tu na watu wawili inaonekan"big issue" kweli mpaka breaking newz...mara habari zilizotufikia hivi punde, lakini huko kwenye gari zetu za mkaa , au dala dala, au za mnadani zinamwaga abiria wa kutosha huwa inaoenekana ishu "minor" sana , hivi kwanini wa tz tunazikweza xana wakati kuna vyombo vya usafiri vinamajnga zaidi ya hivyo vindege vyetu. ni hayo tu.
Imetua katika Ziwa kwa dharura badala yake ingeanguka nchi kavu hakungekuwa na kiumbe hai. Hongera kwake rubani maana kutua ziwani nako ni tukio la kutisha sana.
Tanapa wamefanikisha uokoaji wa ndege husika ndani ya ziwa manayara wah
dah! Ndugu ziwa manyara hakuna mamba na pia si sehemu zote zenye vipoko kwani ni ziwa la maji chumvi na viboko hawaishi sehemu hizo ila wanaisha kwenye mito na mifereji ambayo ina maji yasiyo na chumvi
poleni jee kuna mtu alopoteza maisha
Ehhh! Mjombaangu jamani
Air Tanzania, sikio la kufa! Ni hujuma au uchawi, hili shirika mbona linateketea kwa kasi ya kutisha sana?