Ndege yaanguka ziwa Manyara

Ndege yaanguka ziwa Manyara

ok, taarifa zimefika.
swali langu:mbona ndege ata ikijikwaluza tu na watu wawili inaonekan"big issue" kweli mpaka breaking newz...mara habari zilizotufikia hivi punde, lakini huko kwenye gari zetu za mkaa , au dala dala, au za mnadani zinamwaga abiria wa kutosha huwa inaoenekana ishu "minor" sana , hivi kwanini wa tz tunazikweza xana wakati kuna vyombo vya usafiri vinamajnga zaidi ya hivyo vindege vyetu. ni hayo tu.
...au kurahisisha sema, maji yakikatika masaa sita Masaki/Mikocheni/Mbezi beach sio wala engineer wa dawasko anaenda kusimamia zoezi la kuyarejesha bali waziri mkuu lakini wakati huo huo Yombo/Mnyamani visima vikikauka mwaka mzima hata mjumbe wa shina hajui!
Hiyo ni asili ya binadamu na haiepukiki maana kuna binadamu wanaofikiri sana, wanaofikiri kiasi na wasiopoteza muda wao kufikiri kabisa. Wengi tunaamini kuwa wanaofikiri sana na kiasi hupenda kutumia vyombo hivi vya usafiri. ...is it offending!?
 
Nawapa pole waliopata hio ajali. Lakini ufike wakati sasa ufanyike uchunguzi wa kina kujua chanzo cha hizi ajali za ndege hasa ukanda huo manake kuna nyingine ilianguka recently

JK style, unataka iundwe tume??? Sababu ni uchakavu wa hizo ndege na uzembe wa mamlaka husika.>>>
 
Ndege ya kampuni ya tanzanair iliyokuwa ikitokea bukoba kuelekea zanzibar,imeanguka hivi punde katika ziwa manyara.mpaka muda huu bado inaelea majini,abiria wote sita pamoja na pilot wa saba bado wamo ndani ya ndege.taarfa za hivi karibuni zinasema kuna boti imetoka serena kwenda kuwaokoa.
Nitaendelea kuleta updates
source:niko na mtu ambaye anawasiliana na mmoja wa abiria waliomo ndani ya ndege hiyo.

Asante kwa taarifa; ila kwa maelezo yako inaonyesha ndege hiyo haijaanguka, isipokuwa imetua kwa dharura majini.
 
Air Tanzania, sikio la kufa! Ni hujuma au uchawi, hili shirika mbona linateketea kwa kasi ya kutisha sana?
 
Hivi videge vya ajabu ajabu vinaruhusiwa kuruka vitakuja leta majanga makubwa. Community Airline ilizuiliwa kwa majungu sasa ndio haya tunashuhudia ufisadi katika sekta ya anga. Tuwaombee majeruhi watoke salama.
 
Back
Top Bottom