Ndege kutua na kupaa muda huo huo

Ndege kutua na kupaa muda huo huo

Yamakagashi amejitahidi lakini ni dhahiri hana utaalamu wowote kwenye mambo haya ila ya kusimuliwa. Kwenye ndege hakuna kuweka gear ila unatumia "power lever" na kasi ya ndege inatokana na msukumo wa hewa kwa kutumia propeller au jet thrust na si kupitia landing gear. Kwenye ndege hakuna muunganisho wowote kati ya engine na landing gear.
Kasi ya ndege inaongezwa na kifaa kinachoitwa "throttle" na hii sio gear
 
Point yangu pia inaenda na tukio la kuapply reverse ili kusaidia ndege kusimama alafu baadae ubadilishe ghafla haliwezi kuaribu engine?
Kwa msaada wa Google, inaonesha ndehe ya abiria (jetliner) ili iweze kuruka ni lzm ifikie mwendokasi wa 240–285 km/h, bila hivyo haiwezi kuruka. Na ikifikia mwendokasi huo, haiwezi simama, ni lzm iruke hlf izungue irudi kutua.
 
Sawa mkuu ila naona uliishia kwenye piston engines
Hata gas turbine engine ,unatumia throttle kuongeza kasi bcoz throttle inaongeza fuel into combustion chamber ambayo itasababisha thrust kubwa result yake ni speed kubwa
 
Nimeona mijadala mbalimbali ya ndege na baadhi ya changamoto za kutua au kupaa. Swali langu ni kuwa je kuna uwezekano baada ya ndugu kugusa ardhi ikaunganisha na kupaa tena. Yaani kwa mfano imeshatua na kukawa na dharura mfano runway ni fupi au kuna kizuizi mbele na kuwa haiwezi kumaliza runway salama
Kama mhandisi mstaafu naomba nitoe somo. "Touch and go" yaani kutua na kuruka hufanyika sana wakati was kuwafundisha marubani na mara chache chake baada ya matengezo. Hii hufanyika pakiwepo na mawasiliano na air traffic controller wa uwanja husika.
Kwa ndege kubwa ya abiria au mizigo hili linawezekana lakini itategemea sana na mazingira. Kama ndio tu imegusa chini, ambayo ina maana kawaida in mwanzo wa run way, ndege bado ina kasi kubwa, hivyo inahitaji kuongeza kasi kidogo tena kufika take-off speed. Katika mazingira haya ni rahisi kupaa baada ya umbali mdogo wa run way.
Iwapo ndege itakuwa imepunguza kasi sana itahitaji umbali mrefu wa run way ili kufikia take-off speed, na kwa hiyo uwezekano wa kupaa utategemea urefu wa run way ulio mbele au kama ni kukwepa kitu, umbali wa hicho kitu na ndege ilipo. Vinginevyo ndege itapitiliza kwenye run way au kugonga hicho ilichotaka kukikwepa.
Kila jitihada hufanyika hali kama isitokee kwa kuhakikisha run way iko safi na wazi kabla ndege haijapewa clearance ya kutua na hii ndo mojawapo ya kazi kubwa ya air traffic controller.
Naomba kuwasilisha.

Naelewa mkuu ila katika ulimwengu wa gas turbines tunazungumzia power plant na fuel control unit siyo engine na carburetor.
 
Naelewa mkuu ila katika ulimwengu wa gas turbines tunazungumzia power plant na fuel control unit siyo engine na carburetor.
Nimekuelewa ila kasi inapatikana kutokana na kias cha mafuta unachochoma
 
Umeniambia matukio haya hutokea mara 1-3 kwa safari 1000 "

Hivi ni wewe umeniambia au ni wikipedia hiyo ndio inasema hivyo

Besides 1-3 ya Approaches 1000 na sio safari 1000
Approaches na safari ni vitu viwili tofauti

Anyway ka Google tena soma kwa utulivu tatizo langu halipo kwenye hizo aina sijui ya emergency though hiyo go around procedure inaweza pia ikawa engaged bila kuwa na emergency
67210f7a2e6123ab2fce244814bb6a01.jpg

Anyway Kinana mshamurudisha toka mlipo mtuma ?
Labda ndege iliyomleta ilitake off baada ya kutua JNIA
 
fastjet ilishatikea mwanza, ilitoch town ikapaa kutokana na hali mbaya ya hewa
 
Kuna emergency mbili katika maisha ya ndege
1 Emergency landing
2 Emergency take off
Na siku zote pilot mzuri wa ndege anapimwa kwa emergency situation hasa ktk landing na take off hasa ktk upande wa weather conditions pia landing na take off clealence zinatolewa na watu si machine na unapozungumzia watu pia unatakiwa kujua kuna human error. Run way ya ndege inatakiwa kusiwepo na kitu chochote ambacho kinaweza kusababisha hatari ya aina yeyote na usafiri wa ndege ndio usafiri wenye safety precocious kubwa kuliko usafiri wowote unaojua

Inawezekana kabisa kitendo kama hicho utokea mara 1-3 kwa safari 1000 , so ni mara chache sana kutokea hasa kwa ndege za abiria lakini kwa ndege za jeshi hasa Jet Fighter kutua kwenye Carrier inatokea mara nyingi sana

Kitendo cha kufanya hvyo kinaitwa Go-around ambapo air traffic control wanapokwambia ur clear to land lakini kabla ujafanya hvyo kukatokea hatari ambayo inaweza kusababisha ajari kama kukiwa na gari,ndege au kitu chochote kwenye run way hapo hapo unaweza pewa amri ya kupaa tena ndege za kisasa kama Boeing na Airbus ni nyepesi sana kufanya hvyo ni ku apply full power kwenye engine kwa kupeleka mbele mpaka mwisho ile giar then unabonyeza kuna button zimeandikwa TO/GA, unapobonyeza tayari ndege automatically inajua ni emergency inaongeza airspeed(thrust) kwenye engine ambazo zinapush landing gear mpaka kufikia take off speed kwa muda mfupi sana

Lakini kitendo cha Go-around kwa Jet ni cha kawaida sana hasa wanapotua kwenye carrier, kwani mpaka ndege kutua na kusimama kunatakiwa kuwe na Run way ya kutosha. Sasa kwenye Carrier ni sehemu ndogo sana kulinganisha na uwanja wa ndege pale kunakuwa na kamba maalum inaitwa arrestor cables ambapo pilot anatakiwa akitua tu landing gear za nyuma kunasa kwenye cable za arrestor cables ambazo zinakuwa chini ambazo zinadaka ndege na kufanya isimame yani kama inavutwa nyuma na kupaa hvyo hvyo kuna kifaa ambapo landing gear za mbele uwekwa then kuna machine inapush ndege mpaka kufikia take off speed kwa muda mfupi na umbali mfupi
Sasa pilot wengi wa Jet Fighter kutua kwenye Carrier inatokea umekosea mahesabu ya kunasa arrestor cables njia pekee ni ku apply full power kwenye engine na kufanya touch en go , kwani usipofanya hvyo ndege inakwenda kutumbukia baharini na ndege inakuwa kaburi lako kwani ni kawaida sana vyombo vya moto kama gari au ndege Zikiingia kwenye maji zinarock milango na mfumo wa umeme unakufa so uwezi ku operate chochote kwenye cockpit ya ndege.
Nashukuru sana mkuu. Hakika Jf ni kila kitu
 
Wataalamu wamesha ongea sana
Sisi wataalamu wa aerodynamics tunajua ivyo vitu.
Usipojua hata force 4 zinazo iwezesha ndege kufanya maneuverability basi huwez elewa nini kinafanyika.
Tupe darasa mkuu. Wengine ndio timeanza safari za kutumia ndege so kupata ufahamu kunakupunguzia mashaka ukiwa mawinguni
 
Wikipedia si source pekee ya kujua kitu hata Wikipedia wenyewe wanategemea source zingine kutoa taarifa au habari zao ndio maana mwisho wa taarifa zao wanaweka Reference kama kuonyesha source na sehemu taarifa zao walipozitoa, pia jambo la ndege si nuclear science kwamba ni watu au nchi chache ndizo zenye access ya kujua ni vitu vinavyofundishwa kwa mtu yeyote so kujua ndege au process zinazohusika na ndege ni elimu kama ilivyo elimu nyingine yeyote ambayo watu wanasomea hata ww unaweza kusoma
Siku zote unapokwenda hospitali unajua siku ya kwenda siku ya kutoka anajua doctor so comrade bado hajarudi akirudi mtapewa taarifa
Endeleeni kutupa elimu kwa njia hii mwisho tutapata majibu ya ndege na Kinana pia
 
Kwa msaada wa Google, inaonesha ndehe ya abiria (jetliner) ili iweze kuruka ni lzm ifikie mwendokasi wa 240–285 km/h, bila hivyo haiwezi kuruka. Na ikifikia mwendokasi huo, haiwezi simama, ni lzm iruke hlf izungue irudi kutua.
Hapa ndio kuna hatari kubwa. Niliona clip moja wakati ndege inaondoka ikashika moto ila still hakusimama na matokeo yake ikaanguka. Ni kitu gani kinachozuia ishindwe kusimama ikiwa katika speed hiyo
 
Kama mhandisi mstaafu naomba nitoe somo. "Touch and go" yaani kutua na kuruka hufanyika sana wakati was kuwafundisha marubani na mara chache chake baada ya matengezo. Hii hufanyika pakiwepo na mawasiliano na air traffic controller wa uwanja husika.
Kwa ndege kubwa ya abiria au mizigo hili linawezekana lakini itategemea sana na mazingira. Kama ndio tu imegusa chini, ambayo ina maana kawaida in mwanzo wa run way, ndege bado ina kasi kubwa, hivyo inahitaji kuongeza kasi kidogo tena kufika take-off speed. Katika mazingira haya ni rahisi kupaa baada ya umbali mdogo wa run way.
Iwapo ndege itakuwa imepunguza kasi sana itahitaji umbali mrefu wa run way ili kufikia take-off speed, na kwa hiyo uwezekano wa kupaa utategemea urefu wa run way ulio mbele au kama ni kukwepa kitu, umbali wa hicho kitu na ndege ilipo. Vinginevyo ndege itapitiliza kwenye run way au kugonga hicho ilichotaka kukikwepa.
Kila jitihada hufanyika hali kama isitokee kwa kuhakikisha run way iko safi na wazi kabla ndege haijapewa clearance ya kutua na hii ndo mojawapo ya kazi kubwa ya air traffic controller.
Naomba kuwasilisha.
Kudos mkuu
 
Kuna dogo ana malizia masomo yake ya urubani nampiga maswali nayatoa hapa basi ananiona leo nipo vizuri kumbe hahahahah
 
Hali ya hewa ni mbaya lakini ndege imeshayouch down. Kuna athari gani tena?
ilishindwa kuendelea kutokana na uwanja kujaa maji iabidi irudi hewani, kumbuka haiuland kabisa iligusa kidogo ikapaa tena
 
Point yangu pia inaenda na tukio la kuapply reverse ili kusaidia ndege kusimama alafu baadae ubadilishe ghafla haliwezi kuaribu engine?
Ndege haisimami kwa kutumia revers ina simama kwa kutumia brak ikisaidiwa na wings za nyuma kukumba upepo
 
Back
Top Bottom