Inawezekana kabisa kitendo kama hicho utokea mara 1-3 kwa safari 1000 , so ni mara chache sana kutokea hasa kwa ndege za abiria lakini kwa ndege za jeshi hasa Jet Fighter kutua kwenye Carrier inatokea mara nyingi sana
Kitendo cha kufanya hvyo kinaitwa Go-around ambapo air traffic control wanapokwambia ur clear to land lakini kabla ujafanya hvyo kukatokea hatari ambayo inaweza kusababisha ajari kama kukiwa na gari,ndege au kitu chochote kwenye run way hapo hapo unaweza pewa amri ya kupaa tena ndege za kisasa kama Boeing na Airbus ni nyepesi sana kufanya hvyo ni ku apply full power kwenye engine kwa kupeleka mbele mpaka mwisho ile giar then unabonyeza kuna button zimeandikwa TO/GA, unapobonyeza tayari ndege automatically inajua ni emergency inaongeza airspeed kwenye landing gear mpaka kufikia take off speed kwa muda mfupi sana
Lakini kitendo cha Go-around kwa Jet ni cha kawaida sana hasa wanapotua kwenye carrier, kwani mpaka ndege kutua na kusimama kunatakiwa kuwe na Run way ya kutosha. Sasa kwenye Carrier ni sehemu ndogo sana kulinganisha na uwanja wa ndege pale kunakuwa na kamba maalum inaitwa arrestor cables ambapo pilot anatakiwa akitua tu landing gear za nyuma kunasa kwenye cable za arrestor cables ambazo zinakuwa chini ambazo zinadaka ndege na kufanya isimame yani kama inavutwa nyuma na kupaa hvyo hvyo kuna kifaa ambapo landing gear za mbele uwekwa then kuna machine inapush ndege mpaka kufikia take off speed kwa muda mfupi na umbali mfupi
Sasa pilot wengi wa Jet Fighter kutua kwenye Carrier inatokea umekosea mahesabu ya kunasa arrestor cables njia pekee ni ku apply full power kwenye engine na kufanya Go-around, kwani usipofanya hvyo ndege inakwenda kutumbukia baharini na ndege inakuwa kaburi lako kwani ni kawaida sana vyombo vya moto kama gari au ndege Zikiingia kwenye maji zinarock milango na mfumo wa umeme unakufa so uwezi ku operate chochote kwenye cockpit ya ndege.