Kuhoji ruzuku ya CHADEMA na kutokuhoji ruzuku ya CCM ni ujinga

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,484
2,362
Nimeshangazwa sana na MAKADA wa CCM kuhoji RUZUKU ya CHADEMA ya BIL.2.7 fedha ambazo kwa CCM ni pesa ya MBOGA tu .CCM inapokea zaidi ya mara 10 ya RUZUKU inayopokea.

Na CHADEMA na hakuna hata siku moja CCM imewatangazia WANACHAMA wake kiasi cha RUZUKU inachopata na Matumizi yake. LAKINI leo hii MAKADA wa CCM wameshupaza SHINGO zao eti Wanahoji Ruzuku ya CHADEMA
Nilitegemea Wangekitaka CHAMA chao kwanza Kiwafahamishe kinapokea RUZUKU kiasi gani na MATUMIZI yake.

Sehemu kubwa ya MATUMIZI ya CCM yanagharamiwa na SERIKALI kama vile MAGARI KUMBI za MIKUTANO yake n.k Mfano wa KUMBI mara kadhaa CCM imekuwa inafanyia VIKAO vyake IKULU Jengo la SERIKALI tofauti na CHADEMA mpaka wakodi ukumbi.

Misafara ya VIONGOZI wa CCM wanatumia Magari ya SERIKALI kinachofanyika ni KUBADILISHA Namba za Usajili tofauti na CHADEMA.

Nawashauri MAKADA wa CCM HOJINI RUZUKU za CCM na MATUMIZI yake kwani ni FEDHA nyingi sana Ruzuku ya CHADEMA waachieni Wanachadema wenyewe WAHOJI.
 
Kwa hiyo kila wanalolifanya ccm, na chadema ni sawa kulifanya?
Mi nilidhani chadema ni chama antagonist wa ccm, kumbe nao ni walewale tu 🤔😔
Basi tuna safari ndefu sana.
 
Kwa hiyo kila wanalolifanya ccm, na chadema ni sawa kulifanya?
Mi nilidhani chadema ni chama antagonist wa ccm, kumbe nao ni walewale tu 🤔😔
Basi tuna safari ndefu sana.

..Ruzuku ya Ccm 1.3 billion kila mwezi ni kufuru.

..Mtoa mada ana hoja kwamba kwenye ruzuku tuanze kuwahoji Ccm.

..Je, inaingia akilini kwa chama tawala kupewa billion 1.3 kila mwezi wakati serikali imeelemewa na madeni ktk taasisi nyeti kama Tanroads?

Cc Nguruvi3
 
Nilimshangaa Kinana akihoji ruzuku bila kujiuliza licha ya 'advantage' ya kutumia serikali bado CCM wanapewa ruzuku
Rais SSH anafanya ziara za kichama kwa kodi za Wananchi , si ruzuku. Mzee Kinana anajua hili, kajitoa ufahamu tu.

Upotoshaji ni kudhani ruzuku ni hisani na CDM wameipata kupitia Wabunge! si kweli ni kupitia kura za uchaguzi

Katika nchi masikini kama Tz, ruzuku za Bil 1.3 ili akina DAB wapite barabarani wakieneza unafiki na uongo si sawa.
 
Hicho ndio kinasikitisha, kwamba hata wale wachache kama Kinana tuliodhani wanaweza kuwa na akili tofauti kiasi unagundua kuwa wote ni walewale! Sasa nani ni nafuu huko aliyebaki?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu ataunga mkono hoja za ccm,uko kumejaa watu warafi wa madaraka na wenye tamaa ya mali.Mzee kinana kutokana na maswahibu yaliyo mpata kipindi cha Shujaa JPM,nilitegemea awe na akili ya kimageuzi ili yasije tokea tena mwisho amekuwa bure kabisa.

Wemejimelikisha mali za wananchi kuwa za chama chao.wameipoteza Tanganyika kwa uroho wa madaraka,lakini bado haitoshi wanajiona wenyewe ndo wenye wajibu wa kutoa haki kwa hisani hawa ndo wapumbavu wakubwa wa taifa hili.

Ni muda wa CCM kuondoka kwenye madaraka.Ili kuliponya taifa.
 
Back
Top Bottom