Ndani ya BBC: Kitila Mkumbo atetea 'Ushoga'

Ndani ya BBC: Kitila Mkumbo atetea 'Ushoga'

Tatizo la ushoga kwetu Africa ni kwamba watu wanaliangalia kwa jicho la Yule ni mdhambi, mimi ni mtakatifu. Hili jambo linahitaji umakini na hekima. Kusema kuwa shoga auwawe kweli ni kukosa haki za msingi za ubinadamu. Ushoga kama ni dhambi, basi ni dhambi kama ilivyo kuiba, kuua, udikteita na mengineyo. Mbona sijasikia Museveni anasema dikteita auwawe? Haya mambo inabidi tuyaangalie kwa macho mapana sana.

So ww binafsi ukilitazama kwa macho mapana unafikia conclusion ipi ???
 
Uganda ina haki ya kujiamulia mambo yake, sawa, lakini siyo kujiamulia kunyanyasa watu hovyohovyo. Leo hii Uganda ikidai kwamba watu wa kabila fulani ni duni na hivyo wanapaswa kuangamizwa kutoka kwenye ramani ya Uganda wewe utaona sawa? Utadai kwamba ni sawa tu kwa vile Uganda kama nchi wana haki ya kujiamulia chochote kile wapendacho?

Mashoga nao ni binadamu. Na kwa huo ubinadamu wao tu wanastahili kupewa haki zote za msingi kama binadamu wengine. Wewe kama hupendi ushoga wao achana nao. Fanya yako waache na wao wafanye yao. Kwani kinakuuma nini wao wakiwa mashoga? Inakuhusu nini wewe wao wakiwa mashoga? Is it that hard for you and your ilk to mind your own business and live your own life and leave others alone so they live their own lives too? Why you gotta be all up in their business? Good grief!!

That culture card is a bunch bunk. Homosexuality has always been there since the history of existence So don't even go there and act like it is absolutely brand spanking new to Uganda or any other African country, for that matter.

And you talk about the majority, well, what about the minorities and their right to exist in society? We can't all be the same, for god's sake.

Intelligent people always come up with a modus vivendi so that all can live in a society despite of their differences and ensure that the minorities' rights are protected.

You are way off base. Way way off base. Homosexuality has always been there in Uganda and everywhere and you can't pin it to any specific country as to its origins. I suggest you start reading omnivorously so you can expand those horizons because you appear to be somewhat ignorant on the subject.

Soma vitabu. Narudia tena, soma vitabu. Hakuna aliye-impose ugay Afrika. Ulikuwepo tokea enzi na enzi. Hata wanyama (wasio binadamu) nao wana hayo mambo (lakini sitegemei ulijue hilo kwa sababu umeonyesha ujinga tayari. Hivyo unaweza ku-google ili uweze kujifunza zaidi)

Kilichofanyika ndo haswa siyo demokrasia maana kwenye demokrasia haki za wachache nazo huheshimiwa . Uganda imepiga hatua nyuma kwenye hilo!!!!!!! Kwenye demokrasia hakuna mambo ya kusema sijui kwa vile wengi tunataka hivi basi wale wachache ambao wako kinyume na nyie wengi mnavyotaka, haki zao ziminywe. Hapana. Demokrasia ya ukweli haiko hivyo hata kidogo. Hata walio wachache nao wana nafasi yao katika jamii.

Wewe hujui kabisa maana ya demokrasia. Unadhania tu kwa vile wengi wamekataa jambo basi wale wachache ndo ile kwao, wanyanyaswe, waadhibiwe, waangamizwe, na upuuzi mwingine kama huo.

Hivi kuna ugumu gani kama wewe hupendi jambo fulani kuachana nalo na uwaache wale wanaopenda wajinafasi kwa raha zao?

Tunachotakiwa kuacha ni kukiuka haki za binadamu. Kwenye hizi nchi zetu uhai wa binadamu hauthaminiwi kabisa. Ona watu wanaotuhumiwa kuwa wezi wanavyouliwa mabarabarani mchana kweupe bila hata due process. Kinachohitajika ni mtu mmoja tu kupiga kelele za mwizi! mwizi! tosha. Iwe umeiba kweli au la watu hawajali hilo. Utapewa kipondo na kuchomwa moto hadi ufe mbele ya kadamnasi na hakuna mtu atakayekamatwa kwa kosa la mauaji.

I mean, hata kama mtu kaiba kweli, tuseme kanyakua pochi ya mtu. Ndo kweli apigwe hadi afe na watu waliojichukulia tu sheria mkononi? Na wewe hilo unaweza ukalitetea kwa kujenga hoja ya eti 'wengi waliamua apigwe hadi afe kwa hiyo ni sawa tu alichofanyiwa'? Hapana kwa kweli.

Waganda na demokrasia ni oxymoron. Hawaelewi maana yake. Hilo li-Museveni ni lidikteta na litafia madarakani. Hivyo sishangai sana kusaini sheria ya kijinga na kandamizi kwa Waganda ambao usikute nao ni walipa kodi wazuri kabisa.

Kama minority ni haki yao kwanini ushoga tu? Hata wezi nao ni minorities why dont we consider those for their right to steal? Ushoga kwa definition ya Uganda ni crime sasa niambie history iliyokuwa documented Uganda inayoonyesha mashoga walikuwepo bila punishment ( nipe reference msomi wewe intelligent) mm nitakupa yenye kuonyesha ni laana kwao kufanya hayo mambo. Tena watu wa jinsi hiyo waliuawa which I am against though kwasababu ya Ukristo ambao equally una group ushoga kama laana mbaya....

Kuhusu wanyama nipe reference ya mmoja wanao reproduce sexually aliye homo sexual.... Acha wanyama ambao wapo animal kingdom hata living organisms panua wigo ni tajie species moja inayo reproduce or copulate homosexually... Sitaki kusema huko unako kimbilia ndiyo part ya fani yangu

Besides, ungesema tuutete yshoga simply because ni sehemu ya culture ya waganda pengine ningejitahidi kukuelewa; sasa kwa huyo mtetezi wako anayesema eti itakosa misaada, what a shame! Sijuvuni kuwa race moja na kuushi continent moja na watu kama ninyi ambao kwenu mnaweza ku compromise values za societies zenu. I am ready to stand and be counted at the cost of my precious life!

STOP USHOGA IS A CURSE TO AFRICAN CULTURE!
 
Kuliangalia jamabo la ushoga kwa macho mapana ni kwanza kulichambua kwa udani. Makosa yanayo hakisiwa na sheria zetu na hatimaye kupata adhabu kisheria(za duniani) ni Makosa yake yanayo dhulu binadamu wenzetu na mazingira yetu. Hayo yanaunganisha wizi, kuua, kutesa, uongo n.k. Sasa ukiangalia ushoga kama ulivyo, sioni ni jinsi gani unaathili binadamu mwingine au mazingira zaidi ya kumuathili shoga mwenyewe. Sioni ni jinsi gani unaweza kutunga sheria ya kumuua mtu eti kwa kuwa ni shoga, huku madikteita, wala rushwa watesi wa watu wanapeta tu. Ukisema ushoga ni dhambi kwa Mungu, hapo siwezi kujadili maana macho ya Mungu yana upana zaidi ya uwezo wangu. Pia nafikiri binadamu kama tulivyo, kutenda dhambi ni jambo la kila siku maishani, hivyo sioni ni jinsi gani binadamu anaweza kumuhukumu mwenzake kwamba kakosa kwa misingi ya kumkosea Mungu na si kumkosea binadamu mwenzake au mazingira yake. Naomba kuwakilisha ndugu Mandela.
 
kama minority ni haki yao kwanini ushoga tu? Hata wezi nao ni minorities why dont we consider those for their right to steal? Ushoga kwa definition ya uganda ni crime sasa niambie history iliyokuwa documented uganda inayoonyesha mashoga walikuwepo bila punishment ( nipe reference msomi wewe intelligent) mm nitakupa yenye kuonyesha ni laana kwao kufanya hayo mambo. Tena watu wa jinsi hiyo waliuawa which i am against though kwasababu ya ukristo ambao equally una group ushoga kama laana mbaya....

Kuhusu wanyama nipe reference ya mmoja wanao reproduce sexually aliye homo sexual.... Acha wanyama ambao wapo animal kingdom hata living organisms panua wigo ni tajie species moja inayo reproduce or copulate homosexually... Sitaki kusema huko unako kimbilia ndiyo part ya fani yangu

1. Je ... Ushoga uliouelezea hapo ... Toka uzaliwe , jamiii uliyokulia ilikua inachukuliaje swala la ushoga , na mpaka sasa je hwli ikoje... Hapk sijazungumzia walio wengi .. Nimeongelea mwenekano .. Hata kama ni rafiki mmoja au familia yako ..

2.kuiba,kubaka na mengineyo yote haya ni makosa .. Na mpaka kuonekana ni makosa , ni kwamba jamii imechukia na kulaani juu ya hilo ..
Na sheria zipo kwa ajili ya hayo ..
Je kama ushoga umekataliwa kwenyewe jamii ya uganda ni vibaya kwa museven kuudhibiti kwa kuweka sheria.

Hapa utaniambia ni maamuzi ya wengi na wamedharau haki ya wachache ..
Kwani we unadhani mwzi anayeiba bank hauoni kwamba ni haki kuiba .. Lakini kwa vime jamii haitaki basi jamii iliyo wengi itasikilizwa.. Kwa sababu unachafua amani ya nchi.

Embu jiulize ,kwanini hii issue inashinikizwa saana na nchi za nje ya afrika ... ??? Kwani hatuna haki na sisi ya kufanya maamuzi yetu ???
 
Kama minority ni haki yao kwanini ushoga tu?

Nani kakwambia ni ushoga tu? Hata walemavu nao ni minorities vile vile.

Hata wezi nao ni minorities why dont we consider those for their right to steal?

Wow! I mean, are you serious? Hivi una akili kweli wewe? Hahahaaa daaah! Haya, hebu twende taratibu maana nadhani wavelengths zako ziko kidizaini dizaini.

Yaani kweli wewe wezi unawaita minorities? Na unauliza kwa nini hatuioni haki yao ya kuiba? Hmm...wewe, yaani siamini kabisa kama kuiba unaweza kukuona kuwa ni haki.

Mwizi anayeiba, kitendo cha yeye kuiba mali au vitu vya wengine (walivyojipatia kihalali kwa jasho lao) wewe unaona ni haki hiyo? Kuchukua vitu vya wengine unaona ni haki ya kuweza kulinganishwa na ushoga ambao mtu binafsi anajiamulia kivyavyake na mwenzake?

Yaani mwizi anayekutia hasara unaona ni sawa na shoga anayejifanyia mambo yake kwenye faragha yake huko? Unazungumzia haki za mwizi kuiba? Duuh....I swear I didn't see this coming! Poor thing, just bless your heart.

Bidada, hakuna mtu mwenye haki ya kuchukua vitu au mali za mwingine. Mwizi hana haki ya wizi. Mwizi anapoiba anamtia hasara yule aliyemwibia, hivyo kunakuwa na madhara hapo.

Lakini kwenye ushoga, madhali ni watu wazima wawili waliokubaliana wenyewe kufanyiana wanayotaka kufanyiana, basi hakuna madhara hapo. Hakuna anayetiwa hasara (au madhara kama yapo) pasi na ridhaa yake.

Sijui kama utakuwa umenielewa kwa kweli. Yaani mpaka nimekuonea huruma kabisa maana hicho kiwango cha kufikiri ulichokionyesha hapo hakinipi kabisa matumaini.

Ushoga kwa definition ya Uganda ni crime sasa niambie history iliyokuwa documented Uganda inayoonyesha mashoga walikuwepo bila punishment ( nipe reference msomi wewe intelligent)

Hiyo fasili si imeandikwa tu na watu? Kama imeandikwa tu na watu basi hata ubaguzi wa rangi nao kuna sehemu hapa duniani ilikuwa hivyo hivyo. Kuna sehemu ilikuwa ni jinai kwa watu wa rangi tofauti kuwa wapenzi.

Na kitu knachofanya jambo fulani liwe jinai ni sheria. Na kwa vile kitu au jambo fulani limekatazwa na sheria, hiyo haimaanishi hilo jambo lisiwe sawa. Sheria hutungwa na binadamu na hufutwa na binadamu pia. Uganda wanaweza kuifuta hiyo sheria dhalimu kama walivyoweza kuitunga.

mm nitakupa yenye kuonyesha ni laana kwao kufanya hayo mambo.

Laana kwa mujibu wa nani? Na hata kama ni laana, wewe laana ya mwingine inakuhusu nini? Si umwache tu alaanike kivyake......ya nini kujishughulisha na laana yake? Huna ya kufanya?

Tena watu wa jinsi hiyo waliuawa which I am against though kwasababu ya Ukristo ambao equally una group ushoga kama laana mbaya....

Wewe waache tu walaanike kivyao. Jali yako na utakatifu wako. Ya wengine waachie wao.
 
1. Je ... Ushoga uliouelezea hapo ... Toka uzaliwe , jamiii uliyokulia ilikua inachukuliaje swala la ushoga , na mpaka sasa je hwli ikoje... Hapk sijazungumzia walio wengi .. Nimeongelea mwenekano .. Hata kama ni rafiki mmoja au familia yako ..

2.kuiba,kubaka na mengineyo yote haya ni makosa .. Na mpaka kuonekana ni makosa , ni kwamba jamii imechukia na kulaani juu ya hilo ..
Na sheria zipo kwa ajili ya hayo ..
Je kama ushoga umekataliwa kwenyewe jamii ya uganda ni vibaya kwa museven kuudhibiti kwa kuweka sheria.

Hapa utaniambia ni maamuzi ya wengi na wamedharau haki ya wachache ..
Kwani we unadhani mwzi anayeiba bank hauoni kwamba ni haki kuiba .. Lakini kwa vime jamii haitaki basi jamii iliyo wengi itasikilizwa.. Kwa sababu unachafua amani ya nchi.

Embu jiulize ,kwanini hii issue inashinikizwa saana na nchi za nje ya afrika ... ??? Kwani hatuna haki na sisi ya kufanya maamuzi yetu ???

for @ Ame please n
 
Kuhusu wanyama nipe reference ya mmoja wanao reproduce sexually aliye homo sexual.... Acha wanyama ambao wapo animal kingdom hata living organisms panua wigo ni tajie species moja inayo reproduce or copulate homosexually... Sitaki kusema huko unako kimbilia ndiyo part ya fani yangu

Bofya hapo 1,500 animal species practice homosexuality

Besides, ungesema tuutete yshoga simply because ni sehemu ya culture ya waganda pengine ningejitahidi kukuelewa;

Mashoga nao ni binadamu na kama wanafanya mambo yao huko kivyao vyao bila bugudha kwa yeyote yule, basi wanastahili kuheshimiwa kama binadamu wengine na siyo kuadhibiwa kisa tu wao ni mashoga na mlio wengi hampendi mambo ya kishoga. Kama mtu hupendi hayo mambo usijihusishe nao. Ishi maisha yako waache na wao waishi kivyao.

sasa kwa huyo mtetezi wako anayesema eti itakosa misaada, what a shame!

Nani kasema hivyo? Nitajie huyo mtu na unipe nukuu ya alichokisema.

Sijuvuni kuwa race moja na kuushi continent moja na watu kama ninyi ambao kwenu mnaweza ku compromise values za societies zenu.

Wala hamna shida. Jisikie huru kujisikia vyovyote vile juu yangu na mimi wala sitaku-persecute kwa huo mtazamo wako.

I am ready to stand and be counted at the cost of my precious life!

And I'm ready to stand and be counted for fighting for the rights of everybody, including you.

STOP USHOGA IS A CURSE TO AFRICAN CULTURE!

Just mind your own business and let others be.
 
Nani kakwambia ni ushoga tu? Hata walemavu nao ni minorities vile vile.

Wow! I mean, are you serious? Hivi una akili kweli wewe? Hahahaaa daaah! Haya, hebu twende taratibu maana nadhani wavelengths zako ziko kidizaini dizaini.

Yaani kweli wewe wezi unawaita minorities? Na unauliza kwa nini hatuioni haki yao ya kuiba? Hmm...wewe, yaani siamini kabisa kama kuiba unaweza kukuona kuwa ni haki.

Mwizi anayeiba, kitendo cha yeye kuiba mali au vitu vya wengine (walivyojipatia kihalali kwa jasho lao) wewe unaona ni haki hiyo? Kuchukua vitu vya wengine unaona ni haki ya kuweza kulinganishwa na ushoga ambao mtu binafsi anajiamulia kivyavyake na mwenzake?

Yaani mwizi anayekutia hasara unaona ni sawa na shoga anayejifanyia mambo yake kwenye faragha yake huko? Unazungumzia haki za mwizi kuiba? Duuh....I swear I didn't see this coming! Poor thing, just bless your heart.

Bidada, hakuna mtu mwenye haki ya kuchukua vitu au mali za mwingine. Mwizi hana haki ya wizi. Mwizi anapoiba anamtia hasara yule aliyemwibia, hivyo kunakuwa na madhara hapo.

Lakini kwenye ushoga, madhali ni watu wazima wawili waliokubaliana wenyewe kufanyiana wanayotaka kufanyiana, basi hakuna madhara hapo. Hakuna anayetiwa hasara (au madhara kama yapo) pasi na ridhaa yake.

Sijui kama utakuwa umenielewa kwa kweli. Yaani mpaka nimekuonea huruma kabisa maana hicho kiwango cha kufikiri ulichokionyesha hapo hakinipi kabisa matumaini.

Hiyo fasili si imeandikwa tu na watu? Kama imeandikwa tu na watu basi hata ubaguzi wa rangi nao kuna sehemu hapa duniani ilikuwa hivyo hivyo. Kuna sehemu ilikuwa ni jinai kwa watu wa rangi tofauti kuwa wapenzi.

Na kitu knachofanya jambo fulani liwe jinai ni sheria. Na kwa vile kitu au jambo fulani limekatazwa na sheria, hiyo haimaanishi hilo jambo lisiwe sawa. Sheria hutungwa na binadamu na hufutwa na binadamu pia. Uganda wanaweza kuifuta hiyo sheria dhalimu kama walivyoweza kuitunga.

Laana kwa mujibu wa nani? Na hata kama ni laana, wewe laana ya mwingine inakuhusu nini? Si umwache tu alaanike kivyake......ya nini kujishughulisha na laana yake? Huna ya kufanya?

Wewe waache tu walaanike kivyao. Jali yako na utakatifu wako. Ya wengine waachie wao.

Bahati mbaya siwezi kukujibu point by point kwa device niliyonayo lakini acha nikupe msaada pengine you can recover your conscious!

Kitu gani kinakufanya wewe uchague wizi ambao ni tabia iwe mbaya kwa waganda kuliko ushoga ambao wao wana u perceive ni laana? Labda ujifikirie mwenyewe kati ya laana na tabia mbaya ipi ina hitaji heavy punishment.

Alafu una justify vipi perception yako ndiyo iwe benchmark ya ile ya waganda?

Then kama definition ya wizi inatumia maneno ya wanadamu na ufahamu wao vipi uikataye hii waliyojiwekea waganda wenye quality zote za ubinadamu kama wewe?

Kwakukusaidia google hii concept ya egocentrism wanayotumia wana soholojia ku iron out some of your doubts......

Kama ilivyo right kwako ku punish what you define crime ndivyo ilivyo kwa
Waganda katika jurisdiction yao ku exercise hiyo privilege na wewe una responsibility yakuheshimu rights zao kama ilivyo kwao kwako na Tanzania
Yako. How can I mind my iwn business wakati mm ni social being? Their behaviour wont exclude its impact to my life na wale nao associate nao.... Ni najisi bro na uovu sisi tunaukomesha kama big bro M7 alivyowafanyia.

Asante kwa reference hapo nakuvulia kofia na asante kwakuongeza reference kwenye folder zangu. Thanks a lot for your help be blessed for this!
 
1. Je ... Ushoga uliouelezea hapo ... Toka uzaliwe , jamiii uliyokulia ilikua inachukuliaje swala la ushoga , na mpaka sasa je hwli ikoje... Hapk sijazungumzia walio wengi .. Nimeongelea mwenekano .. Hata kama ni rafiki mmoja au familia yako ..

2.kuiba,kubaka na mengineyo yote haya ni makosa .. Na mpaka kuonekana ni makosa , ni kwamba jamii imechukia na kulaani juu ya hilo ..
Na sheria zipo kwa ajili ya hayo ..
Je kama ushoga umekataliwa kwenyewe jamii ya uganda ni vibaya kwa museven kuudhibiti kwa kuweka sheria.

Hapa utaniambia ni maamuzi ya wengi na wamedharau haki ya wachache ..
Kwani we unadhani mwzi anayeiba bank hauoni kwamba ni haki kuiba .. Lakini kwa vime jamii haitaki basi jamii iliyo wengi itasikilizwa.. Kwa sababu unachafua amani ya nchi.

Embu jiulize ,kwanini hii issue inashinikizwa saana na nchi za nje ya afrika ... ??? Kwani hatuna haki na sisi ya kufanya maamuzi yetu ???

Nadhani mm na wewe tupo ukurasa mmoja mazee!

Ebu basi tusimame nyuma ya big bro M7 kumpa nguvu...
 
Bahati mbaya siwezi kukujibu point by point kwa device niliyonayo lakini acha nikupe msaada pengine you can recover your conscious!

Let not your heart be troubled.

Kitu gani kinakufanya wewe uchague wizi ambao ni tabia iwe mbaya kwa waganda kuliko ushoga ambao wao wana u perceive ni laana?

Mimi nipige box masaa 60 kwa wiki, nipinde mgongo na kibyongo juu, Ijumaa ni payday niende kuchukua cheki yangu. Nikitoka hapo niende kui-cash lakini kabla sijafika kwenye check cashing store, uibuke from nowhere huku umenishikia bastola ukiniamrisha nikupe kila nilichonacho mfukoni la sivyo utakipasulia mbali kichwa changu. Natii amri yako, nakupa check yangu.

Narudi zangu nyumbani mikono mitupu. Check umenipora na kili kilichokuwemo mfukoni mwangu umekichukua kimaguvu. Mimi check yangu nimeifanyia kazi, nimeitolea jasho, wewe umekuja na kuichukua.

Kwa akili, hekima, na busara zako zote ulizopewa na ulizorithi, unaona ni sawa ulivyonifanyia? Unadhani baada ya kunipora nami ntafurahi tu, ntarudi nyumbani nikichekelea nikiwa na shauku ya kumsimulia Bi. Kibadiru ambaye naye ananisubiri nyumbani nije na mboga?

Sasa ushoga unajifanyia mwenyewe huko. Kama ni laana utalaanika mwenyewe. Kimbelembele cha mimi kuja kukulazimisha kufanya tofauti na utakavyo kinahusu nini?

Mbona ni suala jepesi kabisa hilo....

Yaani kama hilo la tofauti ya wizi na ushoga nalo unahitaji kuelezewa, basi, nasalimu amri maana naweza kuwa najadiliana na mtu mwenye uwezo wa chini kidogo.

Labda ujifikirie mwenyewe kati ya laana na tabia mbaya ipi ina hitaji heavy punishment.

Unaonaje tukianzia na fasili za hayo mambo mawili? Ili walau tukubaliane kabisa kwamba 'laana' maana yake ni hii na 'tabia mbaya' maana yake ni hii. Tuanzie hapo kwanza. Unaonaje?

Alafu una justify vipi perception yako ndiyo iwe benchmark ya ile ya waganda?

Waganda wapi unaowazungumzia wewe? Waganda mashoga au wale wanaopinga ushoga? Maana si Waganda wote wana 'benchmark' (whatever you meant by that) iliyo sawa.

Then kama definition ya wizi inatumia maneno ya wanadamu na ufahamu wao vipi uikataye hii waliyojiwekea waganda wenye quality zote za ubinadamu kama wewe?

Huwezi kulinganisha wizi na ushoga. Mtu yeyote yule mwenye akili tu za wastani anajua hilo. Sasa wewe sijui kwa nini tu umeng'ang'ania kulinganisha hayo mambo mawili.

Hivi kwa mfano, nikikuibia hela zako zote ulizozipata kwa kufanya kazi na ambazo zipo kwenye akaunti yako utafurahi?

Kwakukusaidia google hii concept ya egocentrism wanayotumia wana soholojia ku iron out some of your doubts......

Hata sijakuelewa hapo. Ni iron out doubts gani?

Kama ilivyo right kwako ku punish what you define crime ndivyo ilivyo kwa
Waganda katika jurisdiction yao ku exercise hiyo privilege na wewe una responsibility yakuheshimu rights zao kama ilivyo kwao kwako na Tanzania
Yako

But homosexuality is not and should not be a crime. No one is hurt by it. If you don't like it, don't partake in it. Mind yours and let others mind theirs.
 
Let not your heart be troubled.

Mimi nipige box masaa 60 kwa wiki, nipinde mgongo na kibyongo juu, Ijumaa ni payday niende kuchukua cheki yangu. Nikitoka hapo niende kui-cash lakini kabla sijafika kwenye check cashing store, uibuke from nowhere huku umenishikia bastola ukiniamrisha nikupe kila nilichonacho mfukoni la sivyo utakipasulia mbali kichwa changu. Natii amri yako, nakupa check yangu.

Narudi zangu nyumbani mikono mitupu. Check umenipora na kili kilichokuwemo mfukoni mwangu umekichukua kimaguvu. Mimi check yangu nimeifanyia kazi, nimeitolea jasho, wewe umekuja na kuichukua.

Kwa akili, hekima, na busara zako zote ulizopewa na ulizorithi, unaona ni sawa ulivyonifanyia? Unadhani baada ya kunipora nami ntafurahi tu, ntarudi nyumbani nikichekelea nikiwa na shauku ya kumsimulia Bi. Kibadiru ambaye naye ananisubiri nyumbani nije na mboga?

Sasa ushoga unajifanyia mwenyewe huko. Kama ni laana utalaanika mwenyewe. Kimbelembele cha mimi kuja kukulazimisha kufanya tofauti na utakavyo kinahusu nini?

Mbona ni suala jepesi kabisa hilo....

Yaani kama hilo la tofauti ya wizi na ushoga nalo unahitaji kuelezewa, basi, nasalimu amri maana naweza kuwa najadiliana na mtu mwenye uwezo wa chini kidogo.

Unaonaje tukianzia na fasili za hayo mambo mawili? Ili walau tukubaliane kabisa kwamba 'laana' maana yake ni hii na 'tabia mbaya' maana yake ni hii. Tuanzie hapo kwanza. Unaonaje?

Waganda wapi unaowazungumzia wewe? Waganda mashoga au wale wanaopinga ushoga? Maana si Waganda wote wana 'benchmark' (whatever you meant by that) iliyo sawa.

Huwezi kulinganisha wizi na ushoga. Mtu yeyote yule mwenye akili tu za wastani anajua hilo. Sasa wewe sijui kwa nini tu umeng'ang'ania kulinganisha hayo mambo mawili.

Hivi kwa mfano, nikikuibia hela zako zote ulizozipata kwa kufanya kazi na ambazo zipo kwenye akaunti yako utafurahi?

Hata sijakuelewa hapo. Ni iron out doubts gani?

But homosexuality is not and should not be a crime. No one is hurt by it. If you don't like it, don't partake in it. Mind yours and let others mind theirs.

Kwa akili yako hiyo ya kubeba mabox na kutaka kuihukumu dunia nzima kwasababu tu wewe ni mbeba ma box then kosa linalo kuwa linked mabox yako na kuko cost wewe ndilo lenye kuhitaji punishment na lile linalo wa cost wenzako differently linahitaji compromize; Nakubali hiyo akili yangu ni ndogo kama bomu la nuclear na yako ni kubwa kama box ulilozoea kuli beba, lol!

Maisha mema ila kumbuka mabox yana punguza life expectancy rudi nyumbani pengine akili itarudi yakutambua ushoga ni ugonjwa wa akili ambao tiba yake nikuepusha mazoea yanayopelekea kushawishi akili kufanya kinyume na asili....Effect yake ni mbaya kuliko madawa ya kulevya! Vipi hao right zao hao unaowabebea box wataitangaza lini iwe sheria ya dunia?
 
Ina maana hujui madhara watakayopata Uganda kwa kunyimwa hiyo misaada?You must be one those uninformed Chadema supporters whose decision making is ruled by emotions and not reasoning or rationale.Uganda waliahidiwa kupewa karibu dollar million 90 kwaajili ya mradi wa afya je unadhani Uganda watapata wapi pesa kufidia kiasi hicho cha pesa walichoahidiwa na World Bank (USA Agency) ili kuendelea na miradi ya afya waliyokwishaipanga?However i still support Museven decision to sign a bill that bans a same sex marriage in Uganda.
NCHI MASIKINI HAIWEZI
KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA
MSAADA KUTOKA NCHI ZA NJE- J.
K. Nyerere
 
Hili suala linachukuliwa kishabiki zaidi...
 
Kwa akili yako hiyo ya kubeba mabox na kutaka kuihukumu dunia nzima kwasababu tu wewe ni mbeba ma box then kosa linalo kuwa linked mabox yako na kuko cost wewe ndilo lenye kuhitaji punishment na lile linalo wa cost wenzako differently linahitaji compromize; Nakubali hiyo akili yangu ni ndogo kama bomu la nuclear na yako ni kubwa kama box ulilozoea kuli beba, lol!

Such a lightweight!

Maisha mema ila kumbuka mabox yana punguza life expectancy

Lete ushahidi wa kisayansi na si maneno ya kwenye vigodoro.

rudi nyumbani

Hujui nilipo na huna mamlaka ya kuniamrisha.

pengine akili itarudi yakutambua ushoga ni ugonjwa wa akili

Lete ushahidi wa kisayansi unaoonyesha ushoga ni ugonjwa wa akili. Maneno ya kwenye vigodoro hayana nafasi hapa!

ambao tiba yake nikuepusha mazoea yanayopelekea kushawishi akili kufanya kinyume na asili....

Hakika umeishiwa hoja (as if ulikuwa nazo to begin with).

Effect yake ni mbaya kuliko madawa ya kulevya! Vipi hao right zao hao unaowabebea box wataitangaza lini iwe sheria ya dunia?

Wewe jali maisha yako. Acha kujishughulisha na ushoga. Watu hawana time na wewe, maisha ni yai lakini kuhemka uhemke wewe. Huna maisha? Huna shughuli?
 
Goverment should not enforce morality. What happened to separation of church and state? Tunaambiwa kila kukicha serikali haina dini, iweje leo serikali hiyo hiyo inatekeleza amri kumi za Mungu.
 
ttz ni nn ?hivi mashoga wakipewa uhuru wao wa kupractice wanachokiamini nn ttz?

mm si mlevi na dini yangu inakataza sana, lkn nchi imeruhusu walevi kulewa na ttz hamna, kwa nn isiwe kwa hao ?
 
akiojiwa na charles hilary wa bbc, amemponda mseveni kuwa ana mapungufu hivyo kataka apate umaarufu kwa kupinga ushoga. Mimi nimejiuliza maswali mengi, kwa kuwa mseven ni dhaifu kwenye utawala wa kidemokrasia, ni dikteta basi ata ushoga aukubali? Mimi binafsi nimemuona dr kitila hamnazo. Ata kama mseven ana mapungufu, je ili la ushoga kafanya vibaya? Nakumbuka humu jf, watu wengi tumekuwa tunamponda mh rais kwa mambo mengi, lakini alipomshauri kagame aelewane na wapinzani, watz wengi tulimsapoti na ata wanyarwanda walivoanza kumshambuli Rais, wengi tulikuwa nyuma ya rais wetu. Je kitila alitaka M7 aruhusu ushoga? Kwa ili ya ushoga dr kitila huko peke yako labda wale masalia wako.

Kama ni Kweli Dr.Kitila amemponda Museven kwenye hili suala la aibu atakua amefanya makosa

Museven yupo sahihi .Cha msingi nchi za Afrika tuache utegemezi,ufisadi na matumizi mabaya ya raslimali zetu
 
nashukuru kwa vile nawe uneangalia ...
alikua na maana gani kusema ... Museven kajivisha ubabe asio kua na uwezo nao ?? .
alitaka Museven afanyahe instead...

uchumi wa uganda utakuwa chin ya haiti by 2016
 
Mbona umeandika utadhani watu wote wameona hicho kipindi. Ningekuona wa maana kama ungeweka na maelezo aliyotoa Kitila, kuliko kutuambia kuwa anatetea ushoga bila kusema kauteteaje.

huyu dogo ni kijana wa mbowe
 
Back
Top Bottom