Ndala Kasheba

Buswelu

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
1,998
351
Wadau

kuna wimbo mmoja watiwa kesi ya khanga au monica uliimbwa na huyu nguli au bendi ambayi akiitumikia kama kuna mdau anao au link napoweza download please naomba.

Natanguliza shukrani

Buswelu
 
Buswelu naona post yako ni ya muda kidogo na haijapata majibu.
Ni kweli, wimbo wa Kesi ya Khanga au Monica uliimbwa na Ndala Kasheba akiwa na bendi yake ya Zaita musica mwaka 1990.
Wimbo huo ulirekodiwa tena 2003 wakati wa ziara ya Kasheba, King Kiki na Kasongo mpinda jijini London UK.
Unapatikana kwenye album iitwayo Safari ya London. Kama bado hujaupata ni PM
 
Utafute utaupata na jana nmekutana na Ndala Kasheba ofisin kwetu alikuwa kwa masuala ya kusimamiwa haki zake kny muziki na nimeongea naye meng juu ya muziki hapa nyumban na Congo alikotoka. Hebu tafuta hyo safar ya London utapata

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Acha kuongopea watu Mkuu. Freddy Ndala Kasheba ni Al marhuni miaka mingi tu iliopita. Labda kama ulikutana na mzimu jana
 
Hahaaa kaka ni King Kikiii mkuu nakubaliana na ww ndiye nlikutana naye mkuu sorry,mzee wa kitambaa cheupe akiwa na mwanaye Kitobo. So sorry

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Utafute utaupata na jana nmekutana na Ndala Kasheba ofisin kwetu alikuwa kwa masuala ya kusimamiwa haki zake kny muziki na nimeongea naye meng juu ya muziki hapa nyumban na Congo alikotoka. Hebu tafuta hyo safar ya London utapata

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums

Mwanamdodo umenitisha wewe kwamba umekutana juzi na Maestro Ndala Kasheba Mzee wa kombora la nyuzi 12.
 
2.Kesi ya Khanga(Monica)-ZAITA Musica

Mama nipe nauli nikamfuate Monika ee,amekimbilia Zambia na treni ya mizigo ee,kisa cha kukimbia madeni yamemzidi doti kumi za khanga alizokopa hajalipa ee,anatafutwa na Polisi popote hapatikani,na mimi rafiki yake nipo nje kwa mdhamana ee,nililala rumande siku mbili kituoni,usumbufu nilioupata kwa kweli sina raha ee

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi

Mahakamani wameshapanga siku ya kusikiliza kesi,asipokuja nitapelekwa jela kutumikia kifungo,ee Monika eeeh uko wapi ee,Monika eeh

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi eeeeh

Similar Discussions

Back
Top Bottom