Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,279
Mbunge wa Ngara (CCM), Ndaisaba Ruhoro amelitaka Bunge kutunga sheria itakayopiga marufuku matumizi ya vileo hadharani.
Ruhoro alitoa kauli hiyo wakati akichangia Mpango wa Serikali jana bungeni mjini Dodoma akibainisha kuwa kunywa pombe hadharani kunasimamisha shughuli za maendeleo kwa kuwa linashusha ufanisi wa kazi, kutaka watu wasinywe wakati wa kazi.
"Iletwe sheria hapa bungeni itakayopiga marufuku vileo kuuzwa muda wa kazi ili tuipitishe maana haisaidii watu wanashindwa kutimiza majukumu yao wakikimbilia kulewa," amehoji Ruhoro.
Ametaja kundi la vijana kuathirika na kudai wafanyakazi wengi wanatumia saa ya kazi kunywa pombe kwa kuwa muda wa kazi baa huwa zimefunguliwa.