Nchi za kiafrika kupewa unafuu wa kulipa madeni bila mashariti,kuna hatari malengo yasitimiea na nafuu hiyo kutumika kutimiza vipaumbele vya watawala

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Nashauri nchi wahisani na taasisi za fedha za kimataifa kuja na mpango maalumu wa kuhakikisha unafuu wa kulipa madeni ulitolewa unakuwa na mashariti maalumu kwa nchi zote zilizopata unafuu huo.

Nasema hivi kwasababu inawezekana kabisa kwa baadhi ya nchi zetu za kiafrika kutumia unafuu huo kutimiza vipaumbele vya watawala katika mataifa hayo na si kwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa katika kutoa unafuu huo.

Kwa mfano,kuna wanaoweza kutumia unafuu huu kukopa tena kwa siri mikopo mingine ya muda mfupi au kutumia fedha ambazo zingetumika kulipa madeni yaliyofutwa/yaliyositishwa kutimiza malengo yao ya kisiasa,n.k badala ya kutumia unafuu huo kuokoa uchumi wa nchi nzao na kuokoa sekta zinazoathirika vibaya na covid-19 kama vile sekta ya usafiri wa anga kwa sekta binafsi zilizoko katika mataifa hayo.

Binafsi sina imani kabisa na baadhi ya viongozi wa nchi zetu za kiafrika kwani kuna wengine hawajali tabu na mateso wanayopata raia wao bali vipaumbele vyao ni kusalia madarakani na kutimiza malengo yao ya kisiasa hata kwa gharama ya wananchi wao walio masikini.
 
Mbona umetumia Lugha ya Kimatumbi. Je Mabeberu Watapataje ujumbe wako maana ndio wenye sauti katika Taasisi za Kifedha kama ; IFM, World Bank. Pia Kama unaweza zitaje hizo nchi unazodhani zinaweza kuutumia ndivyo sivyo unafuu huu uliotolewa.
 
Back
Top Bottom