Ripoti ya IMF yafichua madai ya “mtego wa madeni" yaliyotengenezwa na Marekani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
VCG111465819175.jpg


Shirika la Fedha la Kimataifa IMF hivi karibuni lilitoa ripoti ya mtazamo wa uchumi wa Afrika ikikiri kuwa China sio chanzo kikuu cha mzigo wa madeni katika Afrika Kusini mwa Sahara. Wachambuzi wanasema wakati Marekani na nchi nyingine za kimagharibi zinaendelea kuishutumu China kwa kutengeneza "mtego wa madeni" barani Afrika, Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, ambalo Marekani ina nguvu halisi ya kura ya turufu, na limepongezwa hadharani na Waziri wa Fedha wa Marekani Jannet Yellen kuwa Shirika hilo limeonyesha utamaduni wa Marekani, sasa linachagua kujitenga na "mtego wa simulizi" wa Marekani kwa kutaja ukweli halisi, kitendo ambacho ni sawa na kuichapa Marekani usoni hadharani.

Kwa miaka mingi, Marekani imekuwa ikitunga uongo kwamba ufadhili wa China umesukuma mzigo wa madeni wa baadhi ya nchi za Afrika kufikia viwango visivyoweza kuhimilika, lakini ukweli ni kwamba asilimia 80 ya madeni yanayokabili nchi za Afrika yanatokana na taasisi za fedha za kimataifa na wakopeshaji wa kibiashara wa nchi za Magharibi, ambapo Marekani ina nafasi kubwa. Wakati huo huo, tafiti nyingi zimethibitisha kuwa mikopo ya China imekuwa na matokeo chanya kwa Afrika. Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, ahadi za ufadhili za China kwa Afrika zimefikia takriban dola za Marekani bilioni 160, ambazo zimeenda kwenye nchi zenye kipato cha chini au cha wastani barani Afrika. Tofauti na wakopeshaji wa kibiashara wa nchi za Magharibi wanaolenga kujipatia faida, ufadhili wa China barani Afrika unatilia mkazo zaidi maendeleo katika sekta kama afya, elimu, mafunzo, kilimo, chakula na nyanja nyinginezo ambazo zinahusiana kwa karibu na maisha ya watu wa Afrika, na kulingana na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya 2030.

Katika Kongamano la Uwekezaji barani Afrika la mwaka 2023 lililofanyika hivi karibuni nchini Morocco, marais wengi wa nchi na wajasiriamali wakubwa wa Afrika wamekubaliana kuwa Afrika inaweza kutumia ipasavyo utajiri wa rasilimali ambazo ni nyenzo zinazohitajika kwenye sekta ya teknolojia ya juu, na soko lake linalokua ili kujiwezesha kuwa mshiriki muhimu katika mnyororo wa uzalishaji kiviwanda duniani. Ili kufikia lengo hilo, Afrika inaweza kutumia kikamilifu ushirikiano kati yake na China katika ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kuvutia uwekezaji zaidi ili kuboresha kiwango cha mawasiliano barani Afrika. Hii inaonyesha kwamba licha ya Marekani kuendelea kuunda "mtego wa simulizi" kuhusu China barani Afrika, utambuzi wa ufadhili wa China barani Afrika unaendelea kuongezeka mbele ya matokeo halisi moja baada ya nyingine.

Hata hivyo, China imekuwa mhusika mkuu katika kukuza urekebishaji wa muundo wa madeni wa nchi za Afrika. Kwa mujibu wa utafiti mpya uliotolewa na Taasisi ya China na Afrika katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani, China imechangia asilimia 63 ya kiasi cha kusitisha madeni kilichokubaliwa na kundi la G20, na kupita kile cha jumla cha nchi za G7. Kama alivyosema Aly-Khan Satchu, mchambuzi wa masuala ya uchumi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ukweli umethibitisha mara kwa mara kwamba Afrika inachukuliwa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi kama rafiki wa raha tu, kama haina tena thamani ya kimkakati, inaweza kutupwa wakati wowote.
 
Ote hao hakuna mwema hata mmoja na huenda miaka 30 au 20 ijayo china akawa ana makoloni yake ya kutosha tu africa au china ikawa ndani ya baadhi ya nchi za Africa kutokana na madeni.

Kwan kila sku demand ya ardhi na raw materials vinapungua so wanatafuta kwa kupitia mikopo na riba za ajabu
 
Nchi za Afrika zimekuwa na mikakati ya muda mrefu kutengeneza Bank of Afrika ambayo itazikopesha nchi za afrika kwa masharti nafuu, lakini sifahamu ni kwanini hawatekelezi hilo. Wanasema Tukakope world bank kuna masharti nafuu, au huko IMF.

Mkikopa kwenye mataifa mnajiuza kwa hayo mataifa. Na hakuna nchi itakupa masharti nafuu.

Waarabu hawapokei riba kwa sheria za dini, kwanini tusikope huko mikopo isiyo na riba. Nilisikia wanaanzisha Islamic Bank huko Zanzibar, waanze mapema tukakope bila riba.

Mikopo ingekuwa na tija ningesema tukope tu, lakini nchi hii wanakopa wao tunallipa sisi. Viongozi hawalipi kodi, mishahara yao haikatwi kodi. Bora tuache tu.
 
Back
Top Bottom