Nchi za Afrika zinazoongozwa vizuri

Nchi za Afrika zinazoongozwa vizuri

Ghana si wale hata mwaka hawajamaliza,toka litokee sakata la uchumi,kwamba wamekopa kupitiliza mpaka uchumi unabembea kwenye kamba???

GDP per Capita ya Tanzania ni dola 1,300

GDP per capita ya Ghana ni dola 2,300

Nani yupo kwenye hali mbaya zaidi?
 
GDP per Capita ya Tanzania ni dola 1,300

GDP per capita ya Ghana ni dola 2,300

Nani yupo kwenye hali mbaya zaidi?
hizi ni namba tu.hata upatikanaji wake hauna uhalisia.wastani wa uchumi wa kila mwananchi yaani idadi yao gawa kwa pato la nchi nzima kwa mwaka.

Mfano angalia nigeria na tz,ila utaambiwa nigeria kuna maisha ya hovyo kuliko hapa.
 
wewe ninachoona ulichokiweka hapa unataka mawazo ya kukisifia na kukikubali hutaki mtu wa kupinga. Hii inaikosesha maana halisi hii mada kwa upana wakoe.
Nakuhitaji unisifie kwa kitu gani? Unisifie mimi kwani mimi ndiye ninayefanya kazi za kukusanya data kutoka mataifa mbalimbali ili kutoa report kama hizi?

Hizi ni report ambazo zinatokana na data zilizokusanywa kwenye mataifa mbalimbali. Haya ni majumuisho. Kama wewe una report yenye data na majumuisho tofauti na haya, ilete. Kisha tujadili na kuona kwa nini kuna utofauti.

Kama hakuna report inayotofautiana na hii, na kwa vile imefanywa na taasisi inayokubalika kimataifa kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa, report hii inachukuliwa kuwa ndiyo fact.

Na hapo, kwa wenye weledi, mjadala wetu ungelenga zaidi maeneo ambayo sisi tunafanya vibaya, na kwa nini tunafanya vibaya. Na kuangalia athari za hayo maeneo ambako tunafanya vibaya. Tunanufaika nini au tunaathirika vipi kwa kuzidi kukumvatia huo ubaya.

Lakini kukazania tu kusema kuwa report siyo ya kweli wakati hakuna research inayotoa matokeo tofauti, tinakuwa ni wapiga kelele badala ya kuwa wajadili hoja.
 
Kwanini unakinzana na wanaotoa sababu zao ambazo zipo tofauti na wewe.
 
Nchi yeyote unapima ubora au utawala bora kwa kuangalia mfumo wa haki, na upatikanaji wa viongozi na uwajibishwaki wa viongozi

sasa Tanzania angalia tu hayo maeneo ni almost poor mahakama zimeoza mahakimu wanafanya kazi kwa vimemo, viongozi wanaiba kura kama njia ya kupatika na hawawajibishwi hata wakiiba
wewe hicho chanzo alichotoa unakiamini na je hizo nchi aliwahi ishi? unaweza ukawa sigimbi huko unaongelea vitu vya kwa madiba bila kujua uhalisia ukoje.
 
Mkuu sikupingi, ila mahakama za SA zimeoza kuliko unavyodhani tofauti ni kwamba wana uzungu mwingi tu. Nimeuliza hapa nchi gani unaua leo tena mchana kweupe na unaendelea kudunda mitaani na kama una hela ya kulipa wakili expensive kesi unashinda!?,mbaya zaidi ukiwa sio raia wa SA (kwarakwara),kesi inakosa nguvu. Ndo huo uhuru wa mahakama mnaosema SA wametuzidi!?, Xenophobia police walikuwa wanakaa mbali wanaangalia tu.
 
Boss, support your arguments with data, this is how critical people do.
Kuna vitu havihitaji hata data ..
Ingia Google...weka images ..halafu Google Burkina Faso na Tanzania...
Au Gambia na Tanzania....
Hata uki Google GDP na GNP....Tu Kati ya Seychelles na Gambia...utapata majibu...
 
Mkuu sikupingi, ila mahakama za SA zimeoza kuliko unavyodhani tofauti ni kwamba wana uzungu mwingi tu. Nimeuliza hapa nchi gani unaua leo tena mchana kweupe na unaendelea kudunda mitaani na kama una hela ya kulipa wakili expensive kesi unashinda!?,mbaya zaidi ukiwa sio raia wa SA (kwarakwara),kesi inakosa nguvu. Ndo huo uhuru wa mahakama mnaosema SA wametuzidi!?, Xenophobia police walikuwa wanakaa mbali wanaangalia tu.
Acha uongo dp world wamesema any dispute ya mkataba kesi iamuliwe south afrika

Kwa afrika hakuna nchi yenye muhimil imara kama mahakama
Maswala ya xenophobic sio kazi ya mahakama ni polisi wapeleke ushahid unaoeleweka
 
wewe hicho chanzo alichotoa unakiamini na je hizo nchi aliwahi ishi? unaweza ukawa sigimbi huko unaongelea vitu vya kwa madiba bila kujua uhalisia ukoje.
Mfano sahivi machawa ndo wanaoteuliwa yaan ndo njia ya kupata viongozi tanzania alafu unafananisha na south afrika

Unavyoangalia nchi nzuri
Unaangalia mahakama
Mfumo wa kupata viongozi
 
Tanzania inaendeshwa vizuri kuliko South Africa...

Burkina Faso utalinganisha na Tanzania?

Kwamba Seychelles inaendeshwa vibaya kulinganisha na Burkina Faso na South Africa?

Another on-line trash list
Mkuu ungemwonyesha na ushahidi kabisa
 
Wewe ni mtupu sana. Umewekewa na link ambayo hata kama una akili ndogo ungeweza kusoma na kuelewa vigezo vilivyotumika. Hawa watafiti hawakurupuki kama unavyofanya wewe, kuropoka tu kuwa Tanzania inaongozwa vizuri kuliko South Afrika.
Hao ndio "machawa" tunaowashuhudia sasa kila kona ya nchi siku hizi. Hawana tena akili za kufikiri 'objectively' juu ya jambo lolote isipokuwa matumbo yao tu basi.

Hawa ndio wanaotakiwa kusakwa kila mahala na kuwaonyesha wananchi genge lililo mstari wa mbele katika kunyimwa haki zao za kuchagua viongozi wanaowataka wao kwa hadaa za kipuuzi zinazotumiwa na genge hili.
 
Tanzania ni full raha, kikubwa ukijua kuzitumia fursa zilizopo muda mchache tu unajipata.
Naunga mkono hoja yako.
Nchi yetu imejaaliwa fursa kibao, lakini watu wake wamelalaa wanasubiri ajira mijini.
Tumekuwa watu wa kusubiri wanasiasa watuelekeze cha kufanya.
 
Kaka marekani Kuna uhalifu kuzidi Tanzania,swali langu je Tanzania Kuna utawala Bora kuzidi Marekani sababu serikali imeshindwa dhibiti uhalifu??
Data za nini mimi ni mtanzania niliyeishi SA zaidi ya miaka 10 na nina watoto huko. Data nilizonazo sio za kusoma mitandaoni na kuleta links hapa, mimi mwenyewe ni data tosha. SA unayoiongelea ni ya kipindi Cha makaburu kabla ya 1994 Mandela kuwa Raisi. Wazungu waliweza kudhibiti nchi shida yao ilikuwa ubaguzi wa rangi tu. Baada ya ANC kuchukua nchi, ni vurugu mechi. Naweza kutoa maelezo hata kurasa 15 hakuna kitu utaniambia kuhusu SA, muulize mtu yeyote aliyekaa SA hata miezi 6 tu, kama uongozi wa SA ni mzuri kuliko Tanzania atakushangaa sana. Kule kila kitu kinajiendea tu Ili mradi. Raia wanaweza kuamka siku hiyo hawataki raia wa nchi nyingine mtaani kwao, wakawakimbiza kuwaibia vitu na mali na gari za Polisi zinapita zinawaangalia kwa mbali tu. Halafu unaniambia South Africa Ina uongozi bora kuliko TZ!??,.. achana na data za Wikipedia na mtandaoni muulize mtu aliyepo huko akuelezee ndo utaelewa.
 
Mfano sahivi machawa ndo wanaoteuliwa yaan ndo njia ya kupata viongozi tanzania alafu unafananisha na south afrika

Unavyoangalia nchi nzuri
Unaangalia mahakama
Mfumo wa kupata viongozi
we unafikiri wanateuliwa tuu bila kufanyiwa vetting si ndio unahisi wengi tunaruhusiwa kuona nje ya kikombe ila kilichomo ndani haturuhusiwi, nchi haiendeshwi kama kikoba mzee.
 
Nchi yeyote unapima ubora au utawala bora kwa kuangalia mfumo wa haki, na upatikanaji wa viongozi na uwajibishwaki wa viongozi

sasa Tanzania angalia tu hayo maeneo ni almost poor mahakama zimeoza mahakimu wanafanya kazi kwa vimemo, viongozi wanaiba kura kama njia ya kupatika na hawawajibishwi hata wakiiba
Jamaa ndio anafananisha south Africa na bongo. Utawala wa sheria ulioko south huwezi fananisha na utawala wa sheria ya bongo. Bongo hakuna sheria ila watu ndio wako juu ya sheria..

Polisi wa south Africa hata shati haruhusiwi kukushika, ukimwomba ID lazima akupe, bongo polisi ndio hakimu, ndio mtunga sheria na ndio pia raisi..

Angalia sakati la zuma na mwanasheria mkuu,
 
Mkiwa mnasoma vitu mahali vitafakari kwa kutumia akili zenu mkigundua ni takataka msivi copy na kuvi paste sehemu nyingine. Umewahi kuishi South Africa hata wiki moja tu!?,hiyo nchi imeoza kwenye kila nyanja. Wazungu wanaoangalia future ya vizazi vyao wanahama Kila siku, kule imebakia maendeleo ya vitu na miundo mbinu basi. Uhalifu upo juu sana, elimu imeshavurugwa. Corruption serikalini ipo kiwango cha SGR, maadili hakuna kabisa. Pamoja na madhaifu ya serikali yetu lakini huwezi kusema tumezidiwa na South Africa, Burkina Faso, Lesotho, Gambia... Never. Hapo wanaotuzidi kiuhalisia ni Botswana, Ghana na Namibia basi. Wengine hakuna lolote.
Ni kwamba umeisahau Mauritius au unaamini Tanzania tupo vizuri kuliko Mauritius?
 
CCM imeshindwa kabisa kuiweka nchi katika utawala mzuri. Siyo mimi ninayesema, bali data zinaongea:

Below are the 10 best governed countries in Africa according to World Economics:

Rank Country. Rank. Score:

1 Mauritius B. 69.3
2 Namibia B. 69.1
3 South Africa B. 65.5
4 Botswana B. 65.1
5 Ghana B. 61.7
6 Senegal C. 53.6
7 Malawi C. 52.9
8 Lesotho C. 52.3
9 Burkina Faso C. 51.8
10 Gambia C. 50.6

Mnaochangia msiropoke, zingatieni vigezo vilivyozingatiwa:

The cornerstone of effective governance globally lies in embracing principles such as transparency, accountability, inclusivity, and adherence to the rule of law.

Kwa vigezo hivyo, ndiyo unaweza kuelewa kwa nini Tanzania ambayo hata mahakama zake hazipo huru, haiwezi kuwa miongoni mwa nchi zinaxoongozwa vyema. Kukosekana kwa uhuru wa mahakama kwa Tanzania, ni jambo dhahiri, ndiyo maana hakuna mwekezaji yeyote mkubwa ambaye yupo Tanzania aliwahi kukubali mgogoro wowote baina yake na Serikali utatuliwe na mahakama za Tanzania.
Ukishaweka lengo la kutawala miaka 1000, kama machawa wanavoxema, akili zte znahamia huko, yaani mnaxema "liwalo na liwe" lazima tushinde. Halafu mnatunga masheria ya kuhakikisha hilo linatendeka. Ndo ujue midomo haixaidii xana, watu wenye akili zao wanaona
 
CCM imeshindwa kabisa kuiweka nchi katika utawala mzuri. Siyo mimi ninayesema, bali data zinaongea:

Below are the 10 best governed countries in Africa according to World Economics:

Rank Country. Rank. Score:

1 Mauritius B. 69.3
2 Namibia B. 69.1
3 South Africa B. 65.5
4 Botswana B. 65.1
5 Ghana B. 61.7
6 Senegal C. 53.6
7 Malawi C. 52.9
8 Lesotho C. 52.3
9 Burkina Faso C. 51.8
10 Gambia C. 50.6

Mnaochangia msiropoke, zingatieni vigezo vilivyozingatiwa:

The cornerstone of effective governance globally lies in embracing principles such as transparency, accountability, inclusivity, and adherence to the rule of law.

Kwa vigezo hivyo, ndiyo unaweza kuelewa kwa nini Tanzania ambayo hata mahakama zake hazipo huru, haiwezi kuwa miongoni mwa nchi zinaxoongozwa vyema. Kukosekana kwa uhuru wa mahakama kwa Tanzania, ni jambo dhahiri, ndiyo maana hakuna mwekezaji yeyote mkubwa ambaye yupo Tanzania aliwahi kukubali mgogoro wowote baina yake na Serikali utatuliwe na mahakama za Tanzania.
"The cornerstone of effective governance globally lies in embracing principles such as transparency, accountability, inclusivity, and adherence to the rule of law". Hii lugha hawaijui na ndiyo muhimu kwenye kujibu, bila kuwatafsiria watajibu kimhemko na tofauti na kinachoongelewa.
 
Back
Top Bottom