Nchi za Afrika zinazoongozwa vizuri

Nchi za Afrika zinazoongozwa vizuri

Mkiwa mnasoma vitu mahali vitafakari kwa kutumia akili zenu mkigundua ni takataka msivi copy na kuvi paste sehemu nyingine. Umewahi kuishi South Africa hata wiki moja tu!?,hiyo nchi imeoza kwenye kila nyanja. Wazungu wanaoangalia future ya vizazi vyao wanahama Kila siku, kule imebakia maendeleo ya vitu na miundo mbinu basi. Uhalifu upo juu sana, elimu imeshavurugwa. Corruption serikalini ipo kiwango cha SGR, maadili hakuna kabisa. Pamoja na madhaifu ya serikali yetu lakini huwezi kusema tumezidiwa na South Africa, Burkina Faso, Lesotho, Gambia... Never. Hapo wanaotuzidi kiuhalisia ni Botswana, Ghana na Namibia basi. Wengine hakuna lolote.
Ungesoma vigezo vilivyotumika na si vigezo vya maisha yenu ya mitaani, kwa vigezo ulivyoelezea basi Tanzania tuko juu sana kuliko Marekani!
Juzi spika wa bunge la Afrka Kusini alifikishwa mahakamani kw tuhuma za rushwa, hapa Tanzania asingeweza kufikishwa mahakamani hata kama angeiba, sheria inamlinda.
 
Jamaa ndio anafananisha south Africa na bongo. Utawala wa sheria ulioko south huwezi fananisha na utawala wa sheria ya bongo. Bongo hakuna sheria ila watu ndio wako juu ya sheria..

Polisi wa south Africa hata shati haruhusiwi kukushika, ukimwomba ID lazima akupe, bongo polisi ndio hakimu, ndio mtunga sheria na ndio pia raisi..

Angalia sakati la zuma na mwanasheria mkuu,
Tanzania polisi anaweza akakulima makofi na kipigo juu na hafanywi chochote Tanzania ni nchi ya hovyo sana ukipata changamoto za kipolisi na kimahakama utaelewa hii inchi inanuka rushwa
 
"The cornerstone of effective governance globally lies in embracing principles such as transparency, accountability, inclusivity, and adherence to the rule of law". Hii lugha hawaijui na ndiyo muhimu kwenye kujibu, bila kuwatafsiria watajibu kimhemko na tofauti na kinachoongelewa.
Tanzania bado kuna mtaji wa wajinga wengi sana na ndo kichaka cha ccm kuwepo mpaka leo madarakani
 
Tanzania inaendeshwa vizuri kuliko South Africa...

Burkina Faso utalinganisha na Tanzania?

Kwamba Seychelles inaendeshwa vibaya kulinganisha na Burkina Faso na South Africa?

Another on-line trash list
Kwenye hio list awatoe SA kule wanakufa watu km kuku wa kideli
 
Kwanini unakinzana na wanaotoa sababu zao ambazo zipo tofauti na wewe.

Siwezi kukinzana na mtu anayetoa hoja yenye mantiki.

Sasa mtu anayesema kuwa haiwezekani Malawi iwe na better governance kuizidi Tanzania. Huyu ametoa hoja au ameropoka? Anayetoa hoja ni yule anayetoa sababu na vielelezo.

Kwa mfano aseme kuwa Tanzania inaizidi Malawi kwa transparency kwa sababu 1, 2 3. Tanzania inaizidi Malawi kwa accountability kwa sababu 1, 2, 3. Tanzania inaizidi Malawi kwenye independence of the judiciary. TZ inaizidi Malawi kwenye suala la utawala wa sheria kwa sababu ya vielelezo vifuatavyo, n.k. Siyo mtu anasema tu kuwa haiwezekani. Hana sababu wala kigezo. Huyo utasema ametoa hoja au amepiga kelele?
 
Mkuu sikupingi, ila mahakama za SA zimeoza kuliko unavyodhani tofauti ni kwamba wana uzungu mwingi tu. Nimeuliza hapa nchi gani unaua leo tena mchana kweupe na unaendelea kudunda mitaani na kama una hela ya kulipa wakili expensive kesi unashinda!?,mbaya zaidi ukiwa sio raia wa SA (kwarakwara),kesi inakosa nguvu. Ndo huo uhuru wa mahakama mnaosema SA wametuzidi!?, Xenophobia police walikuwa wanakaa mbali wanaangalia tu.

Yawezekana kukawa na mapungufu katika mifumo huko South Africa, ndiyo maana ina score ya daraja la B, siyo A. Lakini sisi hatupati B wala C.

Unaposema kuwa mtu yeyote ambaye ana pesa eti anaweza kufanya uovu na asichukuliwe hatua, ni sweeping statement isiyo na uhalisia. Hivi Zuma unaweza kusema hakuwa na hela ya kuwalipa mawakili maarufu ili ashinde kesi, kama pesa ndiyo kigezo pekee cha kushinda kesi? Ule mtandao wa wahindi matajiri watoaji rushwa kwa watawala waliopatikana na hatia mahakamani, unataka kusema hawakuwa na hela?

Tukio moja, mawili au hata matatu, hayawezi kufanya ndiyo mfumo mzima wa mahakama za South Africa.

Mimi nimekaa miezi 4 Joburg, na mwaka mzima CapeTown, naweza kusema kuwa kuna uhalifu mwingi mitaani SA, hasa Joburg, lakini kwa upande wa mahakama, bado mahakama zao zipo much better, even 100 times, kuliko za kwetu.
 
CCM imeshindwa kabisa kuiweka nchi katika utawala mzuri. Siyo mimi ninayesema, bali data zinaongea:

Below are the 10 best governed countries in Africa according to World Economics:

Rank Country. Rank. Score:

1 Mauritius B. 69.3
2 Namibia B. 69.1
3 South Africa B. 65.5
4 Botswana B. 65.1
5 Ghana B. 61.7
6 Senegal C. 53.6
7 Malawi C. 52.9
8 Lesotho C. 52.3
9 Burkina Faso C. 51.8
10 Gambia C. 50.6

Mnaochangia msiropoke, zingatieni vigezo vilivyozingatiwa:

The cornerstone of effective governance globally lies in embracing principles such as transparency, accountability, inclusivity, and adherence to the rule of law.

Kwa vigezo hivyo, ndiyo unaweza kuelewa kwa nini Tanzania ambayo hata mahakama zake hazipo huru, haiwezi kuwa miongoni mwa nchi zinaxoongozwa vyema. Kukosekana kwa uhuru wa mahakama kwa Tanzania, ni jambo dhahiri, ndiyo maana hakuna mwekezaji yeyote mkubwa ambaye yupo Tanzania aliwahi kukubali mgogoro wowote baina yake na Serikali utatuliwe na mahakama za Tanzania.
Ningeshangaa kama Botswana na South Africa zisingekuwepo!
 
CCM imeshindwa kabisa kuiweka nchi katika utawala mzuri. Siyo mimi ninayesema, bali data zinaongea:

Below are the 10 best governed countries in Africa according to World Economics:

Rank Country. Rank. Score:

1 Mauritius B. 69.3
2 Namibia B. 69.1
3 South Africa B. 65.5
4 Botswana B. 65.1
5 Ghana B. 61.7
6 Senegal C. 53.6
7 Malawi C. 52.9
8 Lesotho C. 52.3
9 Burkina Faso C. 51.8
10 Gambia C. 50.6

Mnaochangia msiropoke, zingatieni vigezo vilivyozingatiwa:

The cornerstone of effective governance globally lies in embracing principles such as transparency, accountability, inclusivity, and adherence to the rule of law.

Kwa vigezo hivyo, ndiyo unaweza kuelewa kwa nini Tanzania ambayo hata mahakama zake hazipo huru, haiwezi kuwa miongoni mwa nchi zinaxoongozwa vyema. Kukosekana kwa uhuru wa mahakama kwa Tanzania, ni jambo dhahiri, ndiyo maana hakuna mwekezaji yeyote mkubwa ambaye yupo Tanzania aliwahi kukubali mgogoro wowote baina yake na Serikali utatuliwe na mahakama za Tanzania.

Tanzania inaponzwa na madeni aka Deni la Taifa
 
Back
Top Bottom