jina ni jina tu, hata kesho likibadilika na kuwa JAMHURI YA SOKWENYIKA kwa mfano, it doesnt make any difference. mimi nilizaliwa Tanzania kwa maana ya the land of Tanzania. any time and under proper condition, the same land can be called any other name,
watu wa dunia ya leo wanatazama mbele sio nyuma.
watu wanajiuliza juu ya uraia wa nchi mbili au zaidi, sisi tunajiuliza uraia wa nusu nchi!
watu wanazungumza namna ya kuvutia uwekezaji wa kimataifa, uondoshwaji wa masharti ya visa, sisi tunazungumzia kichefuchefu cha neno "bara" kwenye utambulisho wetu, tunataka turejee kwenye nchi mbili na kurudisha masharti ya passport na visa
watu wanahangaika na mazungumzo ya ushirikiano/uundwaji wa shirikisho, soko la pamoja, ushirikiano katika masuala ya sayansi na tekinolojia, umoja wa forodha, sarafu moja nk sisi tunazungumza namna ya kuvunja muungano!.
jambo la msingi la kujiuliza ni je, tunapiga hatua kimaendeleo au tunarudi nyuma? tunakwammishwa na jina hili tanzania, au ni kitu gani kinatukwamisha tusiendelee kwa kasi tuliyotazamia? kama hatupati maendeleo tunayohitaji kwa kasi tunayotazamia, je, tatizo ni nini, ni jina la Tanzania?
tusijidanganye wapendwa. watoto na wajukuu zetu watatuthamini zaidi sisi na mchango wetu kama watakuta nyumba nzuri, barabara (na miundombinu mingine) nzuri, katiba nzuri, sheria nzuri, jamii iliyostawi vizuri, amani, maelewano mazuri ya kimataifa, maelewano mazuri ya kijamii nk hata kama tutakuwa bado tunabeba utambulisho wa "Tanzania". kinyume chake, hata tukirudia utambulisho wetu wa "Tanganyika" lakini tukakosa haya mambo niliyoyataja, watoto wetu watajuta kuzaliwa "Tanganyika".
tusipoteze dira ya maendeleo, tukageukia jina kama mwarobaini kwa kisingizio cha "jasiri haachi asili" ama uzalendo nk. tusipoangalia tutapoteza muda mwingi sana kwenye cheap politics za majina tukaacha kando masuala muhimu ya maendeleo na hakika tutachekwa na wenye akili