tisa desemba
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 434
- 115
WanaJF nisaidieni tafadhali:
- Hivi Canada, Australia na New zealand nd ni nchi huru?
- Kuna tofauti gani kati ya kupata uhuru na nchi kuwa jamhuri?
Hakuna kukusanyika kwan al-shababu wataujumu, na kova alisha sema hivyo sherekehen majumbani mwenu tuuu.
historia, nimesoma japo si sana inaonekana hukunielewa vizuri kwa vile post imekaakaa kaa shairi fulani hivi, laki my point is:
1. Tanganyika ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wakoloni
2. Tanzania ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wazalendo
3. mimi na wingine wenye umri usiofikia miaka 47, tumezaliwa Tanzania na sio Tanganyika
4. muungano ni kielelezo cha umoja wetu na licha ya mapungufu yake, ni bora kuliko kutengana
5. changamoto tuliyonayo ni kuondoa mapungufu yake, iwe ni kwa kuunda serikali moja, tatu au kubaki na mbili za sasa, vyovyote vile, muhimu tuondoe kero zinazohusiana na muungano
kilichotufanya tusindwe kuijenga Tanzania si muungano uliopo, bali masuala mengi tu tunayojadili hapa kila siku kama ufisadi nk. kwa hiyo hata tukiuvunja muungano, tutashindwa kuijenga Tanganyika pia kama hatutapambana na matatizo haya (ufisadi nk)
Nafikiri kwa wakati huu kama utanikazania niiitwe mtanganyika nitakukatalia mimi ni Mtanzania, so baki na uzanzibar wako sisi tutaendelea na utanzania wetu usitutie ujinga. hamkawii kubadilika mara mtakapoona mtanzania anaendelea mtaomba turudiane so mimi nilizaliwa wakati wa Tanzania na nitaendelea kuwa mtanzania,
mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa Tanganyika,
maana ya neno Tanganyika, siijui,
Tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui
nilizaliwa Tanzania,
nilizaliwa Afrika
nilizaliwa duniani
nlizaliwa na mwanadamu
kwa hiyoÿ
mimi ni mtanzania
mimi ni mwafrika
mimi ni mdunia
mimi ni mwanadamu
maana ya Tanzania, najua
maana ya Afrika, najua
maana ya Dunia, najua
maana ya mwandamu, najua
nawauliza wazanzibari,
nini maana ya Zanzibari,
nani aliipa jina Zanzibari,
kwa nini wajivunie uzanzibari?
kwa nini wasijivunie utanzania?
Usidharau watu simply kwa kuwa wana mtizamo tofauti na wa kwako! Washabiki wa u-Tanganyika bahati mbaya sana haelezi faida zitakazopatikana mara baada ya kuanzisha Serikali tatu! Je, ufisadi utatoweka? Je, umaskini utaondoka? Je, vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 5 vitapungua? Kama hakuna majibu, basi sioni haja ya hiyo Serikali ya Tanganika ambayo nahisi itaongeza matatizo badala ya kupunguza!
mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa Tanganyika,
maana ya neno Tanganyika, siijui,
Tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui
nilizaliwa Tanzania,
nilizaliwa Afrika
nilizaliwa duniani
nlizaliwa na mwanadamu
kwa hiyo;
mimi ni mtanzania
mimi ni mwafrika
mimi ni mdunia
mimi ni mwanadamu
maana ya Tanzania, najua
maana ya Afrika, najua
maana ya Dunia, najua
maana ya mwandamu, najua
nawauliza wazanzibari,
nini maana ya Zanzibari,
nani aliipa jina Zanzibari,
kwa nini wajivunie uzanzibari?
kwa nini wasijivunie utanzania?
Tuko pamoja, lakini kuna wadanganyika, hawa ni nuksi.:juggle::juggle:Tanganyika ipo na kamwe hatuko tayari kuipoteza,Tanganyika bila zanziba inawezekana