Wewe pia hujui. Mabeberu kwanza hutafuta sababu, kisha huitumia sababu hiyo kufikia lengo. Ni kweli, Libya kulikuwa na maisha mazuri kwa vigezo vya kukamilisha matakwa ya binadamu ya mwili: chakula, makazi, umeme, nyumba.....ila hakukuwa na yale ya kukamilisha matakwa ya binadamu ya kiroho/kifikra: uhuru wa kusema, kupinga, kuafiki, kujumuika.......
Binadamu si kama mnyama anayetosheka tu kwa lile la kwanza. Huenda akavumilia ikiwa hilo la kwanza halipo hadi hapo litakapopatikana, ataanza kuomba hili la kiroho na kifikra. Lakini aghalabu, kukosekana kwa la kwanza huwa pia ni sababu ya kuomba hili la pili kwa haraka, maana linapokosekana la kwanza huwa pia kuna dhuluma na ujeuri wa kuzuia hili la pili! Na ukifika wakati huo hata umpe binadamu mikate kumi ya bure kila siku, hilo halitamtosha. Mifano mizuri iko kutoka Iran ( hii hata Mabeberu hawakujiingiza, watu wenyewe tu). Na....natabiri hayo hayo yatatokea Saudi Arabia, Ethiopiana Tanzania ( kama hatutageuza mkondo. Wenzetu Ethiopia wameanza). Hii ni "sunna" ya binadamu!