Nchi inaliwa na mchwa, wananchi tusipoweka mguu chini wanasiasa wataifanya nchi kuwa kama Congo

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
4,430
4,222
Katika interview aliyofanyiwa Bwana Kigwangala ameonyesha wasiwasi wa kuwa wanasiasa wenzake katika chama chake wanafanya kufuru ya wizi wa mali za umma kununua majumba katika maeneo yasiyofikirika mtumishi wa umma kumiliki majengo kama Mikocheni, Dubai, Afrika ya kusini nk. Huyu Mh. amewahi kuwa waziri na anaweza kupata taarifa ambazo sisi watu wa kawaida si rahisi kuzipata.

Mheshimiwa Balozi pole pole katika interview na mwandishi wa habari nguli huyo huyo wa the Chanzo alionyesha wasi wasi kuwa wahuni wametapakaa katika serikali hii ya awamu ya sita na kuonyesha wasi wasi kuwa huenda hawa wahuni walioaminiwa na mama Samia wakatufikisha ndiko siko kama Taifa.

Katika report ya CAG ambae ndie instrument ya Taifa, report yake kila mmoja anajua kuwa ilijaa uchafu mwingi sana ambao unatia kinyaa kwa mzarendo yeyote wa taifa hili na ni bahati mbaya sana kuwa hakuna hatua madhubuti kulinusuru Taifa letu na uhuni huu wa kutapanya mali za umma.

Kwa sasa hivi ni dhahri kuwa kila kona watu wanalia na sidhani kuwa kuna anaesikia kilio chao. na kwa mantiki hiyo ni lazima tujiulize mbali na CAG ambaye ndo angalau anafanya kazi yake instruments zifuatazo zina kazi zipi kwa sasa.

1. Tume ya maadili
2. Jeshi la polisi
3. Usalama wa Taifa
4.Takukuru
5. Waandishi wa habari

Ni kwa masikitiko makubwa kuwa nchi yetu kwa sasa wananchi wake tumekuwa wajinga wa kupindikia habari zetu ni yanga na simba na wanasiasa wamechukua hiyo opportunity and its real sad.Haya mambo hayahitaji research kwani kwenye issue ya bandari, uporaji wa rasilimali unaoendelea na jinsi kwenye system wanavyolindana tunayo hali mbaya.

Suala la ulinzi wa rasilimali zetu tujikabidhi sisi wananchi na tusipuuze habari, kila anaepata habari ya wizi tuweke hadharani bila hiana maana sioni hizi tool nilizotaja hapo juu zikifanya kazi inavyotakiwa. hata kutoka nje ya nyumba ukapiga mayowe tu inatosha kwani ki ukweli hali si shwari.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom