Hivi kuna mtu anawaelewa wanasiasa wa hii nchi kweli?

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,296
3,967
Wakati wa Prof Muhongo,wakipigia upatu mradi wa gesi ya mtwara,akisaidiwa na wanasiasa wa vyama vyote mfano akina Zitto,waliahidi kuwa huu mradi ukianza hakutakuwa na mgawo wa umeme tena.

Na gharama za umeme zitashuka sana.

Miaka michache baadae,ni kama nchi ndiyo imepata Uhuru.Mgao sasa ni zaidi ya wastani wa saa 72 kwa wiki.

Mh Magufuli alipoingia,alifikia kuwatuhumu baadhi ya wanasiasa waliotumika kuhujumu suala la umeme,hadi kuamua kuyafungulia maji mabwawa ili maji yapungue wakate umeme.Kusema kweli kwa miaka yake mitano,hakukuwa na shida ya umeme kabisa.

Mara tu Magufuli alipoondoka,wajuaji walianza kukata umeme hovyo hovyo wakimlaumu eti alikuwa hafanyi service ya mitambo.Wao wakaanza service tukiwa gizani.Tukapewa muda wa service na ahadi kuwa umeme hautakatika hovyo tena baada ya service hiyo.Muda ukaisha,matatizo ndiyo yakaongezeka.

Tukaambiwa mabwawa hayana maji.Mungu si Athuman,mvua zilianza kunyesha tena sana,tatizo halikuisha.Tukaambiwa mvua hazinyeshi kwenye mabwawa.Hata hivyo naamini Mungu alichukizwa na akaamua kuleta mvua za mafuriko kila mahala.Bado tatizo halikuisha.

Ndipo Rais akaja mbele ya umma na kuahidi tatizo hili litaisha baada ya miezi sita.Nakumbuka ilikuwa mwezi wa nane ama wa tisa mwaka jana.

Leo miezi sita inaisha hakuna hata dalili ya tatizo kuisha badala yake hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha.

Katika hali ya kusikitisha kabisa,nimesoma taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari kuwa,bunge limewapa serikali hadi mwezi Juni, tatizo la umeme Liishe eti kwa kuwa serikali waliahidi litaisha mwezi Juni!

Hivi watanzania ni mimi huenda sikumuelewa mama alivyoahidi kuwa litaisha baada ya miezi sita na kumbe alisema litaisha mwezi wa sita!

Kama kuna mtu anawaelewa wanasiasa,anisaidie kuelewa maana ninajikuta nikiamini hawa jamaa huenda wana unasaba na shetani kabisa.Ni vigumu kuwaelewa.Wanatumia kanuni ya ku confuse watu hususan tunaotawaliwa.
 
Mimi nawaelewa,
1. Upinzani na watawala wote lao ni moja

2. Hawajawahi kuwa na utofauti/kutofautiana na kama ikitokea ujue ni ishu za Personal

3. Ukiona kiongozi yeyote wa upinzani mkali kuliko kawaida, huyu hajawahi kuwekwa ama kushirikishwa kwenye mambo kadhaa ya kisiasa ya pande mbili, yupo yupo haelewi nn kinaendelea ndani

4. Wanasiasa wote ni marafiki (wanaitilafiana katika Personal issues, na hasa kama maslahi yako biased)

5. Mwisho kabisa siasa ni kama movies za hollywood (binadamu anatoa spider webs mkononi)

Ushauri pambana kutengeneza maisha yako... Sababu wanasiasa wanapambana kutengeneza maisha yao
 
Wakati wa Prof Muhongo,wakipigia upatu mradi wa gesi ya mtwara,akisaidiwa na wanasiasa wa vyama vyote mfano akina Zitto,waliahidi kuwa huu mradi ukianza .
Tanzania tupo pazuri sana kisiasa na kwakweli tunaelekea pazuri sana...

Msioelewa siasa ya TZ, tutakwenda nanyi taratibu, pole pole na kwakweli tutavuka salama sote 🐒

muhimu sana muwe na subra, na mara zote muwe wastahimilivu na wenye bidii katika kufanya kazi na daima msikate tamaa hata kidogo...

R I P Laigwanan comrade ENL
 
Wakati wa Prof Muhongo,wakipigia upatu mradi wa gesi ya mtwara,akisaidiwa na wanasiasa wa vyama vyote mfano akina Zitto,waliahidi kuwa huu mradi ukianza hakutakuwa na mgawo wa umeme tena.
Na gharama za umeme zitashuka sana.
Miaka michache baadae,ni kama nchi ndiyo imepata Uhuru.Mgao sasa ni zaidi ya wastani wa saa 72 kwa wiki.

Mh Magufuli alipoingia,alifikia kuwatuhumu baadhi ya wanasiasa waliotumika kuhujumu suala la umeme,hadi kuamua kuyafungulia maji mabwawa ili maji yapungue wakate umeme.Kusema kweli kwa miaka yake mitano,hakukuwa na shida ya umeme kabisa.

Mara tu Magufuli alipoondoka,wajuaji walianza kukata umeme hovyo hovyo wakimlaumu eti alikuwa hafanyi service ya mitambo.Wao wakaanza service tukiwa gizani.Tukapewa muda wa service na ahadi kuwa umeme hautakatika hovyo tena baada ya service hiyo.Muda ukaisha,matatizo ndiyo yakaongezeka.

Tukaambiwa mabwawa hayana maji.Mungu si Athuman,mvua zilianza kunyesha tena sana,tatizo halikuisha.Tukaambiwa mvua hazinyeshi kwenye mabwawa.Hata hivyo naamini Mungu alichukizwa na akaamua kuleta mvua za mafuriko kila mahala.Bado tatizo halikuisha.

Ndipo Rais akaja mbele ya umma na kuahidi tatizo hili litaisha baada ya miezi sita.Nakumbuka ilikuwa mwezi wa nane ama wa tisa mwaka jana.
Leo miezi sita inaisha hakuna hata dalili ya tatizo kuisha badala yake hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha.

Katika hali ya kusikitisha kabisa,nimesoma taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari kuwa,bunge limewapa serikali hadi mwezi Juni, tatizo la umeme Liishe eti kwa kuwa serikali waliahidi litaisha mwezi Juni!

Hivi watanzania ni mimi huenda sikumuelewa mama alivyoahidi kuwa litaisha baada ya miezi sita na kumbe alisema litaisha mwezi wa sita!!!

Kama kuna mtu anawaelewa wanasiasa,anisaidie kuelewa maana ninajikuta nikiamini hawa jamaa huenda wana unasaba na shetani kabisa.Ni vigumu kuwaelewa.Wanatumia kanuni ya ku confuse watu hususan tunaotawaliwa.
Wanasiasa wa nchi hii kwa 80% ni wapumbavu kwa sababu wanatoka kwenye jamii ambayo 80% yake imejaa wapumbavu.
 
Hii ndo Tanzania huku Tanesco wanasema mabwawa hayana maji ya kutosha ndo maana Kuna mgao,kule sukari imepanda bei kisa viwanda havizalishi kwa sababu ya miwa imesombwa na mafuriko.
Bado hujasema 😂 😂 😂 , na utasema 😂😂, yaani mpaka useeme 😂
 
Wakati wa Prof Muhongo,wakipigia upatu mradi wa gesi ya mtwara,akisaidiwa na wanasiasa wa vyama vyote mfano akina Zitto,waliahidi kuwa huu mradi ukianza hakutakuwa na mgawo wa umeme tena.
Na gharama za umeme zitashuka sana.
Miaka michache baadae,ni kama nchi ndiyo imepata Uhuru.Mgao sasa ni zaidi ya wastani wa saa 72 kwa wiki.

Mh Magufuli alipoingia,alifikia kuwatuhumu baadhi ya wanasiasa waliotumika kuhujumu suala la umeme,hadi kuamua kuyafungulia maji mabwawa ili maji yapungue wakate umeme.Kusema kweli kwa miaka yake mitano,hakukuwa na shida ya umeme kabisa.

Mara tu Magufuli alipoondoka,wajuaji walianza kukata umeme hovyo hovyo wakimlaumu eti alikuwa hafanyi service ya mitambo.Wao wakaanza service tukiwa gizani.Tukapewa muda wa service na ahadi kuwa umeme hautakatika hovyo tena baada ya service hiyo.Muda ukaisha,matatizo ndiyo yakaongezeka.

Tukaambiwa mabwawa hayana maji.Mungu si Athuman,mvua zilianza kunyesha tena sana,tatizo halikuisha.Tukaambiwa mvua hazinyeshi kwenye mabwawa.Hata hivyo naamini Mungu alichukizwa na akaamua kuleta mvua za mafuriko kila mahala.Bado tatizo halikuisha.

Ndipo Rais akaja mbele ya umma na kuahidi tatizo hili litaisha baada ya miezi sita.Nakumbuka ilikuwa mwezi wa nane ama wa tisa mwaka jana.
Leo miezi sita inaisha hakuna hata dalili ya tatizo kuisha badala yake hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha.

Katika hali ya kusikitisha kabisa,nimesoma taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari kuwa,bunge limewapa serikali hadi mwezi Juni, tatizo la umeme Liishe eti kwa kuwa serikali waliahidi litaisha mwezi Juni!

Hivi watanzania ni mimi huenda sikumuelewa mama alivyoahidi kuwa litaisha baada ya miezi sita na kumbe alisema litaisha mwezi wa sita!!!

Kama kuna mtu anawaelewa wanasiasa,anisaidie kuelewa maana ninajikuta nikiamini hawa jamaa huenda wana unasaba na shetani kabisa.Ni vigumu kuwaelewa.Wanatumia kanuni ya ku confuse watu hususan tunaotawaliwa.
Sio wanasiasa, ni CCM ndugu.

CCM ndiyo kiini cha kila uovu, umasikini, ujinga, magonjwa na kutoendelea kwa ujumla.
 
Mzee wa msoga kama kawa yake walijiuzia vile vitalu vya gas kwa 'wakoloni" tena kwa bei ya maparachichi!
Tena kwa hati ya dharura iliyopitishwa na wabunge wa CCM kwa "kitu kdg"
 
Back
Top Bottom