Nchi imegeuka ya wacheza kamari!

Kuna mambo ukiyacheki unabaki kuumia na kukasirika tu. Just imagine mnyama wa taifa ni twiga, timu ya taifa twiga na ndo tupo tupo tu kama twiga, favorite ya vijana wengi ni kamari na ulevi tena vinahimizwa mpaka kwenye television ya taifa halafu Kila wakisimama jukwaani utasikia vijana acheni kuwaza shortcut jitumeni na mjiajiri ndipo mfanikiwe, alama za taifa mwenge ni alama kubwa sana miongoni mwao- kila mwaka kukimbizana na mimoshi ya moto matokeo yake unasababisha ngono tu na ukimwi

Huzuni zaidi ni kwamba hao TBL, TCC, na hao wa kamari ndio wanaoingizia serikali pato kubwa
 
Wapendwa binafsi nmekua nikichukizwa na kufadhaishwa sana kwa jinsi vitendo vya kamari na bahati nasibu zilivyoshamiri kwenye jamii yetu, nmekua nikijiuliza maswali kadhaa kama taifa tunaelekea wapi ,upi mstakabali wa vijana wetu na ubunifu kwa ujumla ili kuboresha ustawi wetu kama taifa.

Vyombo vya habari navyo vimekua mstari wa mbele kuanzisha michezo yao ya kubahatisha ilihali wanajua wazi njia hiyo inawatajirisha na kuzidi kumdhoofisha mtanzania mnyonge.

Chukulia mfano bahati nasibu ya mtu kupokea laki 5 kwa kutuma shs 1000 kwenda namba ya kampuni, kama watz mil1 wakituma hiyo elfu1 manake wasimanizi wanapokea bil1 alafu wanatoa laki5 kwa mshindi, hii kitu haikubaliki na inazidisha umaskini kweny jamii yetu, naomba kama taifa tujiunge na kupinga michezo hii inayozidi kuangamiza taifa letu.

Nawasilisha
Economic crisis! Ilishawahi kutokea miaka ya 1933s nchini ufaransa, wahuni wakahamia USA, Ndiyo ikawa home gambling, miji mikubwa kama Las Vegas, New York City and Hong Kong,ndiko ulikoanzia ule mchezo maarufu Deci, pyramid scheme system Nchi inapita Wakati mgumu kidogo
 
Back
Top Bottom