Nchi hii viongozi wa dini wamezidi unafiki
Ndugu, waombe radhi viongozi wa dini kwa kuanza na kashfa dhidi yao. Si kila kitu ni siasa.
pamoja na kuhubiri neno la Mungu wanapaswa kukemea maovu
Kazi yao ni kuhubiri neno la Mungu na kuwaasa wanadamu waachane na uovu kwa kuhofia hukumu ijayo (msingi wa imani)
hasa pale viongozi wanapokiuka misingi ya nchi kwa kuvunja katiba na sheria za nchi wanapaswa kukemewa
Viongozi wa dini hawaapi kuilinda katiba ya nchi, bali kweli ya neno la Mungu. Wao hutoa kemeo la ujumla kwa uovu unaoenderlea katika jamii, mfano rushwa na ufisadi. Lakini kumbuka kazi yao ya msingi ni kuwahubiria waumini wao ubaya wa utenda dhambi na hukumu yake wakati wa kiama.
viongozi wa dini wanaona jinsi viongozi wa vyama vya siasa wanavyogandamizwa na serikali wao wapo kimya
Kitendo cha viongozi wa dini kuingia katika haya moja kwa moja ni kuchagua pande. Kumbuka wakati Gwajima anamuunga mkono Lowassa, wengine wa imani yake walikuwa upande wa Magufuli. Unapata picha? Msitake kugeuza nyumba za ibada kuwa uwanja wa siasa. Vinginevyo viongozi hawa watapoteza credibility na hakuna atakaye wasiiliza
siku yakitokea machafuko wao huwa wa kwanza kukimbilia kuliombea amani taifa, huu ni unafiki
Sio unafiki, ndio sehemu ya jukumu lao. Hawalindi amani kwa kuhubiri siasa madhabahuni, bali kwa kumuomba wanayemwamini kwamba anaweza yote ailinde amani yetu.
hao mnaowafuata yaani Yesu na mtume Muhammad hawakuwa waoga kiasi hicho walikemea serikali zao bila unafiki wowote hali iliyopelekea hata kuingia matatizoni.
Kama hujui Yesu Kristu mwenyewe hakuwahi kuingia matatani ni serikali ya wakati wake, bali VIONGOZI WA DINI ama MAFARISAYO. Kumbuka Pilato alijaribu hata kumwachia huru Yesu Kristu!!
Alilipa kodi na kuamuru ya kaisari tumpe kaisari na ya Mungu tumpe Mungu.
Wewe unataka ya kaisari tumpe Mungu na ya Mungu tumpe kaisari!!
Ni unafiki kuombea taifa amani ili hali misingi ya amani inapovunjwa wapo kimya.[/QUOTE]
Misingi ya amani inapovunjwa, ndipo wenye haki wanamlilia Mungu ageuze mioyo ya watawala ili amani irejee.
Hii ni pamoja na kikundi cha wahuni kinapoamua kushambulia misingi ya amani kwa kujipa majukumu ya polisi, ilhali wahusika wapo. Hapa lazima wapige magoti kuombea amani!!