Nchi hii tuna viongozi wa dini wanafiki sana

Waache viongozi wetu,mnaenda kanisani/mskitini mnaonywa hamuonyeki!!! Wao wanatoa mafundisho katika nyumba za ibada hawapendi kumwandama mtu like personal...kama mu wapenzi Wa Mungu basi mfuate mafundisho sio kulazimisha watu wadini kuingilia siasa zenu
Maneno kuntu...viongozi wa dini sio walioagiza ukawa kumpokea mzee mamvi ambapo wananchi walikasirika na kuwanyima kula. Hapo viongozi wa dini wanaingiaje katika hilo?
 
JAmani haya sasa ni maajabu kabisa kuchanganya mabombo,

Kwani huyo kiongozi wa dini anamwamba mungu gani, maana haya anayoyafanya Dr. Pombe ni ya huyo huyo Mungu sasa sema unajichanganya tu.

Hao wanasiasa unaowasema juzi tu walikuwa wanatwambia kuwa nchi imeoza.
Tena walisema nchi hii inaitaji rais DIKTETA.
Hao hao wakaendelea kusema TANZANIA iaitaji rais atakayekuwa nafanya maamuzi ya matamko yake.
Alafu hao unaotaka watetewe alisema anatakiwa rais mkali

SAsa sikia hadi tunafika 1992 tulikuwa na viwanda/mashirika ya umma 425 ndani ya chama kimoja, sasa tulipoingia ktk mfumo wa vyama vingi CCM nayo ikaacha ujenzi wa viwanda na hata kuua vile vilivyokuwepo hili nao wafanye siasa kama wenzao.
Sasa Magufuli amekuja na kuanza kurudisha nchi ktk misingi yake wewe unasema wanaonewa.
Sisi WA TANZANIA TUNATAKA MAENDELEO NA SI SIASA.

Mh. rais Kaza buti Hao viongozi wa dini watakao jitokeza ni wale wenye maslai binafsi. Tupa kule.
Maneno kuntu..kula like
 
Maneno kuntu sana! Unafiki unalitafuna Taifa hili.
Nilikuwa mtumishi wa kanisa lako Bwana atasema sikujui , Nilikuwa nikitoa zaka nyingi kanisani atasema sikujui , Nilikuwa nikiponya watu na kunena kwa lugha atasema sikujui , ondokeni mkachomwe moto na shetani ×2 huu wimbo umebeba ujumbe kuntu.
 
Nchi hii viongozi wa dini wamezidi unafiki, pamoja na kuhubiri neno la Mungu wanapaswa kukemea maovu hasa pale viongozi wanapokiuka misingi ya nchi kwa kuvunja katiba na sheria za nchi wanapaswa kukemewa, viongozi wa dini wanaona jinsi viongozi wa vyama vya siasa wanavyogandamizwa na serikali wao wapo kimya, siku yakitokea machafuko wao huwa wa kwanza kukimbilia kuliombea amani taifa, huu ni unafiki, hao mnaowafuata yaani Yesu na mtume Muhammad hawakuwa waoga kiasi hicho walikemea serikali zao bila unafiki wowote hali iliyopelekea hata kuingia matatizoni.

Ni unafiki kuombea taifa amani ili hali misingi ya amani inapovunjwa wapo kimya.
Kitu kingine ni kwamba, ukiwa mhubiri wa dini ukiwapongeza viongozi wa serikali kanisani/msikitini kuwa wanafanya vizuri katika eneo fulani na hivyo tuwape ushirikiano, hakuna anayelalamika kuwa "unachanganya dini na siasa". Lakini, ukiwa mhubiri ukiwakosowa viongozi wa serikali na kuwaomba wananchi wawajibishe ili wazidi kuboresha utendaji wao utalalamikiwa na kuundiwa mizengwe kuwa "unachanganya dini na siasa". Sababu yake ni nini na viongozi wa dini wanapaswa wafanye nini - kukaa kimya kama wanaona kuna haja ya kusema kuhusu jambo fulani wanaloona haliendi au kusema na kuanza kutupiwa lawama kila kona?
 
Katika Biblia kuna kitabu kimoja kinaitwa Wafalme,Kitabu hiki kinayo mengi sana ya kujifunza.Kinazungumza habari za Wafalme ambao walikuwa viongozi wa Taifa teule la Mungu.Miongoni mwao ni Mfalme Manase,Manase alilelewa vema sana na baba yake ambaye pia alikuwa ni Mfalme kabla ya Manase. Wakati huo baba yake alikuwa na rafiki yake ambaye pia alikuwa nabii wa Mungu ambaye aliitwa Nabii Isaya. Isaya alikuwa mtumishi wa Mungu ambaye alimtumia kuonya Wafalme na watu wa Taifa la Mungu.Manase akiwa Mdogo sana baba yake alimchukua na kuketi naye mahali pake ili ajifunze namna ya kutawala kwa haki mara baada ya baba yake.Baada ya muda baba yake Manase alilala mauti hivyo Manase akawa mfalme kamili akiwa peke yake. Manase akaanza kukengeuka akafanya machukizo mbele za Mungu.
Nabii Isaya bila kuogopa akaenda kwa Mfalme Manase na kumueleza kinagaubaga kuwa ametenda machukizo mbele za Mungu. Mfalme Manase akaamuru Nabii Isaya auwawe kwa kupasuliwa na Msumeno.Lakini tunamuona Mfalme alichukuliwa utumwani kwa aibu.
Mada yangu imejikita zaidi kwa Nabii Isaya,yeye alikuwa mtumishi wa Mungu tena hasiye a unafiki alimmfuata Manase Ikulu na kumuonya, Je leo hii wako wapi kina Nabii Isaya miongoni mwa watumishi wa Mungu waliopo?Mbona leo kina Manase kila wakifika katika nyumba za Ibada kina Isaya wa Leo ndiyo wa kwanza kuwatukuza.Je kina Isaya hawaoni vilio hivi vilivyozagaa miongoni mwa wananchi?.Nini kinasababisha viongozi wa dini wasifanye wajibu wao bila kupepesa macho na wala bila kuhofia usalama wao kama Nabii Isaya?.
 
Hawa wa leo njaa kali na Unafki juu. Wanahaidiwa kujengewa mahekalu watasema nini ??!!
 
Nchi nzima ilikuwa dini moja ya kiyahudi hivyo kiongozi wa kidini alikuwa kama viongozxi wa kidini wa nchi za kiislamu ambako kiongozi wa kidini anakuwa na nguvu kubwa na sauti kubwa usilinganishe na Tanzania nchi isiyokuwa na dini.
 
Nchi hii viongozi wa dini wamezidi unafiki, pamoja na kuhubiri neno la Mungu wanapaswa kukemea maovu hasa pale viongozi wanapokiuka misingi ya nchi kwa kuvunja katiba na sheria za nchi wanapaswa kukemewa, viongozi wa dini wanaona jinsi viongozi wa vyama vya siasa wanavyogandamizwa na serikali wao wapo kimya, siku yakitokea machafuko wao huwa wa kwanza kukimbilia kuliombea amani taifa, huu ni unafiki, hao mnaowafuata yaani Yesu na mtume Muhammad hawakuwa waoga kiasi hicho walikemea serikali zao bila unafiki wowote hali iliyopelekea hata kuingia matatizoni.

Ni unafiki kuombea taifa amani ili hali misingi ya amani inapovunjwa wapo kimya.
ukuta uliwapa deni, walijiiingiza kuisaidia serikali kuitega ukawa km haikutaka amani,wakapewa jukumu waliloomba la kuongea za serikali. ETI WAONGEE NA BOSS WAO ,MWAJIRI WAO?Mrejesho hadi kiama au Yesu arudi.Sasa waje kuwaambia wananchi hadharani kwamba CCM sio sikivu.Umbea wao sasa umewashika.
 
Nchi hii viongozi wa dini wamezidi unafiki, pamoja na kuhubiri neno la Mungu wanapaswa kukemea maovu hasa pale viongozi wanapokiuka misingi ya nchi kwa kuvunja katiba na sheria za nchi wanapaswa kukemewa, viongozi wa dini wanaona jinsi viongozi wa vyama vya siasa wanavyogandamizwa na serikali wao wapo kimya, siku yakitokea machafuko wao huwa wa kwanza kukimbilia kuliombea amani taifa, huu ni unafiki, hao mnaowafuata yaani Yesu na mtume Muhammad hawakuwa waoga kiasi hicho walikemea serikali zao bila unafiki wowote hali iliyopelekea hata kuingia matatizoni.

Ni unafiki kuombea taifa amani ili hali misingi ya amani inapovunjwa wapo kimya.
Ume hit the point ila subiri WAFIA CHAMA WAJE HAPA
 
Kwa nchi za wenzetu zilizoendelea China,Japan,Germany,UK,USA,Russia,Korea kusini nk sijawahi kusikia eti kuna kuna waraka wa maaskofu au wa mashekhe.Wenzetu huu upuuzi hawauendekezi na ndio maana wanapiga hatua na wanazidi kuwa wamoja.Hivi hawa viongozi wa dini mfano KKKT,CATHOLIC,MORAVIAN ,WAISLAM na WASABATO hivi kila mmoja akitoa waraka au vison yake alafu wote wakatofautiana hamuoni kama watawagawa watanzania,haya maswala ya dini ya ishie huko ktk familia zenu kwani tukiwaendekeza watatugawa hawa watu wa dini na cha ajabu sisi Wafrika tulio kumbatia dini tunazidi kuwa masikini kuliko wenzetu wasiokuwa na muda na hizi dini,sometime tujitafakari kama Waafrika.
 
Back
Top Bottom