Nchi hii haitawaliki tena!

Ndg wajumbe nimetafakar kwa muda na nimejiuliza vitu vingi hasa kuanzia utawala wa Mh Mwinyi then Mh Mkapa na Mh Jakaya, hasa Mkapa na Jakaya.

Kiutawala Mwinyi alipiga hatua flan ingawa haikuwalidhisha baadh lakin kwa namna flan ilikuwa ni hatua, Mkapa akapiga hatua kadhaa ambazo ziliwafanya baadh ya watu wapendekeze katiba kubadilishwa ili aongezewa hata miaka mitano tu, lakin katiba ni katiba. Ingawa mwishon inasemekana alikwapua, ila kuna hatua ilionekana kiutawala.

Then akaingia Mh Jakaya kwa kura nying tena zilizovunja record, akionekana ni Rais kijana na mjanja wa mjin ambae angepiga hatua kubwa zaid hasa kwa vijana, lakin sina uhakika kama yale matumain ya wapiga kura 2005 kama bado yapo, na sidhan kama kuna mtu atapendekeza katiba imuongezee muda kama ilivyotokea kwa Mkapa.

Je, ni kwanini nchi imefikia hapa mara baada ya hatua zote hizo tena kwa huyu kiongoz aliyekuwa kwenye serikali zote mbil zilizomtangulia? Kwanini nchi imekuwa na sintofahamu nyingi kwa wakati mmoja na zisizo na majibu ya uhakika? Kwanini uaminifu baina yetu umepungua kwa kiasi kikubwa?

MIGOMO (Madaktari & walimu), RUSHWA (Mawaziri, Wabunge, wakurugenzi wa mashirika ya Uma, Mahakama/Polis n.k) MIGOGORO (Malawi na ziwa Nyasa, Meli ya IRAN na bendera ya TZ, haki na huduma za raia) MAJANGA (Meli kuzama znz, ajal barabaran, Dr Ulimboka na kuhusishwa kwa serikali) na mengineyo hasa kuanzia 2010.

Siupingi utawala wa Jakaya lakini nia yangu ni kujua kwanini hayo yametokea katika utawala huu kwa kiasi kikubwa kuliko tawala zilizopita? Ni wap utawala huu ulijikwaa? Au ni baada ya Lowassa na Richmond?

Je, ni kweli hapa tulipo sasa nchi haitawaliki, yani ipo kiholela tu, viongozi hawaaminiki na hawasikilizwi.?
 
Pia Rais wangu kuongoza nchi kishikaji. Akisahau uwongoz ni dhamana kubwa na hana ubia na mtu. Ukiacha katiba,
 
We cant blame anyone but the Government with leaders who are there to make friends with the rich inside and outside the country. The leaders who are easily blinded by outside investors with cheap contracts over precious wealth of our country and the leaders who despise the need and cry of normal Tanzanians.

Utajiri wetu unatugombanisha, Wazungu wanaumezea mate halafu sisi tunachekelea na kuwakaribisha bila tahadhali makini.

Wananchi wanajaribu kupaza sauti kwamba viongozi waache mambo hayo, badala yake wanapuuzwa kwa nguvu za dola na kubezwa eti hawajui maana ya maendeleo.

Sio kwamba Nchi haitawaliki, Wananchi wamechoka sana na Maisha haya na hatuoni dira kwa viongozi wetu.

Sasa hivi ni kama vile ViongoZi wanakamilisha tu vipindi vyao vya uongozi, hakuna anayetaka kuwa HERO wa nchi hii...na anayetaka kujaribu, badala ya kutiwa moyo na kupewa support, anabezwa kwamba ANATAFUTA UMAARUFU.

IPO SIKU KWELI NCHI INAWEZA ISITAWALIKE..GOD FORBID!!!
 
"Nchi hii haitawaliki tena"ni maneno yaliyo tamkwa mzee Ndesamburo mbunge na kada wa chadema mwaka jana baada ya serekali kubaka democrasia mkoani arusha kwa kuua raia ktk maandamano ya amani kupinga ubakaji wa demokrasia ulifanywa na CCM ikishirikiana na serekali yake, ktk mkutano wa kulaaani tendo hilo Ndesamburo alisema kama serekali imeanza kubaka demokrasia na kuua wananchi wake kwa kutumia polisi basi nchi hii haitawaliki tena.....

Tangu mwaka 2010 nchi yetu imekua ikiandamwa na majanga ya kushangaza ambayo mimi binafsi naona kama ni lahana inayotokana na viongozi ambao wameingia madarakani kwa njia chafu kama rushwa na kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu,watu hawa sio chaguo la wananchi na na wamekua wakilahaniwa na wananchi matokeo yake lahana hizi zinaanza kuonekana wazi kwa matukio yanayoendelea hasa kutokana na kugawa wananchi kutokana na hoja dhaifu,kama udini,ukabila,ukanda na upendeleo ambazo tunaanza kuona matokeo yake:-

1. Udini sasa wazi tunaanza kuona waisilamu wakigomea mipango ya serekali kama sensa na matokeo ya kidato cha nne yaliyotolwa na baraza la mitihani.haya yanatokana na hoja za kidini ambazo wahasisi ni ccm ambazo zinaelekea kutugawa watanzania katika makundi,mfano cuf ilishambuliwa kwa hoja ya udini kuwa ni waislamuna sasa chadema nao wanasingiziwa ni wadini wakati chama kina wafuasi wa dini zote wapagani,waslam na wakristo.

2. Muendelezo wa mauaji kwa chama pinzani cha chadema,mauji yanafanywa makusudi sasa ili kuzima na kutisha harakati za mabadiliko ambapo wamekua wakizima mikutano ya chadema tu,wakiacha matamasha ya fiesta yakiendelea wakati huu wa sensa ni jambo ambalo naona hakuna atakaea vumilia kuicha nchi itawalike kwa kundamimiza baadha ya wananchi katika nchi yao..

3.ubaguzi wa vipato baina ya wanasiasa na watumishi wa kawida.kama wakulima na wafanyakazi ambapo tayari kuna kila dalili ya wanyonywa kushindw kuvulia kundi la wanasiasa na viongozi wandamizi wajuu wa serekali wakipangia na kujilipa mishahara mikubwa na posho nono wakati wateleza sera na mipango kama madaktari na walimu wakigandamizwa nalo linaifanya nchi hii isitawalike siku za usoni...

4. Migomo ya wafanyakazi kama madaktari na walimu inayodumaza maendeleo ya wananchi kwasababu ya kuwalipa maslai duni watumishi hawa muhimu wa serekali,ambao kwasasa serekali inadhani imewadhibiti kwa kukimbilia mahakamani badala ya kutekeleza bado yanafukuta chini kwa chini tusubiri mlipuko wake tena na kila dalili zipo kweli nchi siku za mbele kwa haya haitatawalika kama alivyosema ndesamburo....

5. Dhuluma na unovu unaofanywa na wenye fedha wakishirikiana kudhurumu ardhi za wanyonge na bomoa bomoa isizofuata haki za binadamu ktk makazi ya wananchi migogoro hii nayo siku za mbele itafanya nchi isitawalike kiraisi kama alivyosema ndesapesa......

6. Ubaguzi katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu vyuo vikuu ni janga siku za mbele kwani maskini waanbaghuliwa ktk elimu kwa kutumia bodi ya mikopo kitu ambacho siku kitakusanya hasira za wanyonge against wanyanyasaji wao ambao ni serekali na bodi yake ya mikopo itokanayo na kodi zao sioni amani ktk ili......

7. Wazee na pensheni na dhuluma zinazofanywa na mifuko ya ifadhi ya jamii,manyanyaso ktk malipo na hata kudhurummiwa kabisa ambako serekali inakufumbia macho kwa kuwa tu watendaji wake ndio wahusika wakuu hemu ona wazee wa eas sfrica wanavyoangaika kuipata haki yao...kataika alichokisema ndesamburo lizima kiendelee tokea...

8. Wimbi la vijana kukosa ajira na hama hama ya kutoka vijijini kuja mjini ili kwa siku za mbele na hata sasa linaifanya nchi isitawalike kwa uraisi...jamani yapo mengi mno, ambayo tunayaona yanafanya nchi isitulie, ndio maana nchi haipunziki na matukio mfanao, umetoka mgomo wa madaktari umefuata mgomo wa walimu umetoka mgomo wa walimu umefuata mgomo waislamu kugomea sensa, umetoka mgomo wa waislamu na sensa yamefuta mauji ya raia morogoro na mauaji ya mwandishi wa habari iringa na sasa kinachofuata ni mgomo waandishi wa habari dhidi ya serekali na polisi,

Kama wananchi tumechoka kusikia habari mbaya za matukio ya ajabu ajabu wakati wenzetu wakiangaika kuvumbua technolojia mbalimbali sisi tupo busy na majanga na kubuni majanga kama mgawo wa umeme,na mauaji ya raia,haya ni matokeo ya kuingia madarakani viongozi ambao hawajali wananchi waliopata uongozi kwa njia sio halali mafano umejidhihirisha ktk uchaguzi wa igunga na sumbawanga mjini....

Kamwe watu hawa tusitegemeee watuletee maendeleo zaidi tutaendelea kusikia majanga kila kukicha wakati wenzetu wakiwa bize kuvumbua maendeleo kwa staili hii nchi hii haitatawalika kwa raha kama alivyowai kusema filimon ndesamburo......ni yangu maoni na machungu juu ya serekali na inakoipeleka. Asante.

Nomba kuwakisilisha wanajamvi..........

Tafadhari mods wa jf, naomba mulinde uhuru wa mawazo ya watu kwani na nyinyi siku hizi mnabomoa uhuru wanajf kwa kutupia kapuni haja na michango ya wanajanvi wanaotoa uzi kama huu wa kuikosoa sirikali
 
Ndesamburo alilia jukwaani huku akisema yeye alishiriki kutafuta uhuru wa nchi hii lakini hakupigwa mabomu na wazungu leo hii anapigwa mabomu na vikaragosi vya kikwete, ilivuta hisia sana mpaka vijana walikuwa tayari kwa lolote....
 
Si walisema nchi haita tawalika, analeta hadithi gani tena.

wewe gambba sio yaani ukimpiga chura teke umempunguzia safari,mnazani mnawapiga chadema mkidhani wananchi tuta nyamaza kwa wizi na ujambazi wenu,mwambie baba na mwekiti wako kikwete mwisho wake na cccm yake 2015.......mtake msitake,rais wetu Dr.slaa lazima tumweke madarakani hamtaiba tena kura.mtaficha wapi sura zenu?mafisadi na watoto wa mafisadi kama wewe?f** you
 
wewe umempitisha Slaa kuwa mgombea bila hata kuchaguliwa. Au ndio usultani wa CDM huu? Halafu wewe umweke Slaa madarakani kwani umekua Rostam Azizi?
 
Ndesamburo alilia jukwaani huku akisema yeye alishiriki kutafuta uhuru wa nchi hii lakini hakupigwa mabomu na wazungu leo hii anapigwa mabomu na vikaragosi vya kikwete, ilivuta hisia sana mpaka vijana walikuwa tayari kwa lolote....

Huyu bora apumzike na siasa sasa, asije kufia kwenye jukwaa
 
Ndesamburo alilia jukwaani huku akisema yeye alishiriki kutafuta uhuru wa nchi hii lakini hakupigwa mabomu na wazungu leo hii anapigwa mabomu na vikaragosi vya kikwete, ilivuta hisia sana mpaka vijana walikuwa tayari kwa lolote....
Ndiyo hao waliomteka Ulimboka na kuendeleza mauaji kwenye mikutano ya chadema. VIKARAGOSI VYA KIKWETE.
 
wewe umempitisha Slaa kuwa mgombea bila hata kuchaguliwa. Au ndio usultani wa CDM huu? Halafu wewe umweke Slaa madarakani kwani umekua Rostam Azizi?

wewe njaa yako mbya sana,hivi haujui kuwa SLAA ndio rais wa nchi hii na ccm mnatekeleza ilani ya cdm...mlivyo wajinga katiba haikuwa katika ilan yenu leo mnatekeleza ilani ya chadema,dhaifu anajua dhairi kuwa slaa ndie rais wa nchi subiri dawa yenu inachemka 2015 mtajificha wapi kwa haya mnayotufanyia leo?ilo ndio swali langu
 
Rais wa ngarenaro.
 
wewe umempitisha Slaa kuwa mgombea bila hata kuchaguliwa. Au ndio usultani wa CDM huu? Halafu wewe umweke Slaa madarakani kwani umekua Rostam Azizi?

wewe gamba,nimesema tumuweke sio nimuweke ona jinsi vichwa vyenu vilikuwa vigumu hata kinasomeka na kuonekana mnapindisha rudia tena kusoma DR.SLAA TUTAMUWEKA MADARAKANI 2015 KAMA TULIVYOFANYA 2010,,kuchakachua itakua ngumu mno...........maana patachimbika
 
wewe njaa yako mbya sana,hivi haujui kuwa SLAA ndio rais wa nchi hii na ccm mnatekeleza ilani ya cdm...mlivyo wajinga katiba haikuwa katika ilan yenu leo mnatekeleza ilani ya chadema,dhaifu anajua dhairi kuwa slaa ndie rais wa nchi subiri dawa yenu inachemka 2015 mtajificha wapi kwa haya mnayotufanyia leo?ilo ndio swali langu

Kweli mtu anaweza kuota hata bila kulala nimeamini'slaa rais wa wapi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom