Nchi hii haitawaliki tena! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi hii haitawaliki tena!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tikerra, Mar 30, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tanzania iko njia panda.

  Rais hana mamlaka tena,analosema linaonekana kama takatataka. Aliodhani watamsaidia, sasa wamemgeuke kabisa, wako kinyume naye.

  Ni hali tete isiyo ya kawaida, hali ya hatari. Ni wazi sasa kuna pande mbili zinazopingana, yaani serikali mbili. Mafahali wawili wanapigana na katika hali hii zitakazoumia ni nyasi, yaani wananchi. Ni mzimu gani umeikumba nchi yetu jamani?

  Kikwete nakuuliza wewe, hivi umeshindwa kabisa kupata suluhisho la kudumu la matatizo tunayokabiliana nayo hivi sasa? Hivi unataka tuanze kuchinjana kama kuku?

  Kwa mtazamo wangu ni kwamba hata kama unayo mikakati ya kumaliza matatizo yanayolikumba taifa letu hivi sasa, speed yako ni ndogo mno. Tutakuwa tumeshamalizana hata kabla mipango yako haijafanikiwa.

  Naomba ukimbie badala ya kutembea.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  na badala ya kuyashughulikia matatizo hayo ameamua kuanza kujiandaa kwa ajili ya kurudi tena 2010! Si kesha sema miaka hii miwili iliyobaki hatasafiri sana nje ili ajiandae kwa kampeni za uchaguzi za 2010?
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tanzania inatawalika ila JK amekosa ujasiri wa kuwashughulikia mafisadi kutokana na kujuana nao sasa kazi kwake 2010.
   
 4. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nchi inatawalika japo kuna baadhi ya watu wanaopenda nchi isitawalike kwaajili ya maslahi yao. Wengi wetu hatujui maana ya nchi kutotawalika na athari yake.
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  tatizo ni yeye mwenyewe, huwezi kuwa baba wa familia kisha unataka amri, principles na kanuni za kuendeshea familia yako utungiwe au kuletewa na baba mwingine.
   
 6. k

  kohena Member

  #6
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anasema anafuata utawala wa sheria sababu waliokaribu yake ndio wanavuruga hii Nchi kwa tamaa zao.
   
 7. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Si wanasema ni demokrasia. Kwamba unakuwa Raisi kwa sababu watu wametaka uwe Raisi. Unatawala kwa principles na kanuni walizoziweka waliokuweka. Unatoa amri kwa kuzingatia misingi ya priciples na kanuni za waliokuweka bila kusahau utashi wao. Wanasema kwamba Raisi pamoja na mamlaka yake yote ni mtu mdogo sana kwa wananchi. Mimi naona Raisi katika nchi ya kidemokrasia hana sifa ya baba wa familia.
   
 8. K

  Ki tochi Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  washikaji kwa hiyo hata u serious unapungua. tunakoelekea si kuzuri ila wananchi wenyewe tuwape support wale wanaojitahidi kuleta mabadiliko.
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Watz tutaacha lini kulalamika?.....kwa nini hatuamui kundamana saaizi ili kumng'o kikwete kwa kuwadanganya watz huku akiwakumbatia mafisaidi na yeye na ccm wakineemeka na ufisadi unaofanywa kwa pomoja na lowasa na rostamu na kikwete?...............kweli tz ni nchi ya siasa...watu tunaongea zaidi kuliko kutenda........kwa hali ilivyo ingekuwa nchi za wenzetu mtu km rostamu na familia yae angekuwa ameshachinjwa zamani tungekuwa tunajadili mambo mengine.......hapa kwetu rasi ndiyo mshirika mkuu wa mafisadi?!?!?!?!?!?!?!?!/.................kamwe hatutakuja kufika...tuchukue hatua kwani wengine wanafanyaje na sisi tunashindwa nini...........
   
 10. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  This is already a failed state. Sasa watachukua resources zetu kwa kujinoma. Lakini Watanzania tulikuwa na uwezo wote wa kuzuia hali hii ila tumepoteza chances zote. It's now too late.

  Tusubiri kiama chetu!
   
 11. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kauli kama hizi za kichochezi haziendani na malengo na sera za jamii forum. Kwa kauli yako sijui unawataka wananchi wamchinje Rostaum na familia yake? Alafu kosa hilo zito la Rostam lisilokuwa na suluhu zaidi ya kumchinja yeye na familia yake hulitaji. Mimi naona mhariri hupaswi kuruhusu posts kama hizi ambazo kwa maoni yangu zina kauli za kijinai.

  Ambacho msemaji angefanya kama anaamini yuko sahihi ni yeye mwenyewe kuandamana na walio nyuma yake kwenda huko Ikulu bila kujali nini itakuwa hatima yake kuliko kusema tu na kuwapotosha wananchi.
   
 12. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi kwa maoni yangu hatujawaha too late kutatuwa matatizo yetu wala dola haijashindwa. Dola ina mihimili mitatu likiwemo Bunge. Kwa bahati nzuri Bunge la safari hii lina mchanganyiko wa damu changa na pevu na lina uwakilishi nafuu wa vyama vya upinzani. Bunge lina mamlka makubwa ya kuweza kuikosoa na kuielekeza serikali. Tulitumie Bunge letu kurekebisha kasoro.

  Alafu, tunao mtaji wa katiba mpya ambao una baraka kutoka serikali na vyama vyote vya siasa. Matatizo tuliyonayo, kwa mujibu wa wataalamu wetu, yanachangiwa pia na mapungufu ya kikatiba na sheria. Tutumie nafasi hii kushawishi mabadiliko bora ya katiba yanayoweza kuzaa suluhisho la kudumu na kuleta muafaka mpya wa namna ya kutawalana.

  Matatizo ya ufisadi hatupaswi kuyakuza wala kuyadogosha. Ufisadi ni tatizo kubwa katika nchi nyingi za Afrika na hasa zile zile zilizo katika njia ya kwenda ubepari. Tatizo ni kwamba tuliingia ubepari bila kujiandaa. Tutumie nafasi hii ya katiba mpya kuleta mabadiliko ya kudumu
   
 13. m

  mzee wa inshu Member

  #13
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  No!, suluhu la kweli sio kuchinjana bali ni kujipanga namna ya kukuza demokrasia na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili wapate upeo wa kuchanganua mbichi na mbivu na pia kushinikiza mchakato utakaopelekea wananchi kupitia wawakilishi kuwa na mamlaka ya kuwawajibisha watawala wao pindi wanapokiuka maadili ya uongozi kwa vitendo vinavo dumaza uchumi wa taifa na kuzidi kuwadidimiza wananchi katika umasikini.

  Lengo liwe kuwapata viongozi wenye uchungu wa kweli na nchi yao bila kujali itikadi, dini, rangi wala kabila.


  Elimu ya uraia na subira ni bora zaidi kuliko mapanga katik kuleta mabadiliko ya kweli na maendeleo ya taifa.

  Sio kweli kwamba tumekosa suluhisho kiasi kwamba sasa tuanze kumwagana damu wenyewe kwa wenyewe. Tukifanya hivo tutajitumbukiza katika shimo ambalo itakuwa vigumu sana kwetu kutoka na kurejea katika hali ya utulivu waawali.

  MUNGU BARIKI TANZANIA NA WATU WAKE!
   
 14. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  .


  Sikia, wale waliomsaidia amewageuka na anaenda kinyume nao, so wameamua kukaa pembeni na kufanya mambo yao (hana ubavu wa kuwazuia). huyu ndo Jk usiyemjua.
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Unatamani istawalike lakini you are wrong..

  Matatizo yapo ndio maisha bila matatizo yatakuwa meaningless..

  Serikali zote za kidemokrasia kuna principles zake za kuendesha mambo...(consesus)

  Tulia subiri 2015 chagua unayemtaka..shiriki katika kumiliki uchumi wetu kwa vitendo, pambana na wahujumu kwa nguvu zako zote..
   
 16. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi sioni kama suala ni kuwageuka aliowasaidi. Lililojitokeza ndazi ya CCM ni mageuzi ambayo yalikuwa na nia nzuri japo yalifanyika haraka bila maandalizi. Sheria ya Garama ya Uchaguzi na msisitizo wake katika chama kuliwafanya baadhi ya wale waliokuwa wamejiandaa kama kawaida ya zamani kushindwa bila kutarajia. Hiyo iliwafanya baadhi yao kuimba kiCCM na kucheza kichochezi huku wakijifanya ni wasaidizi wa wapinzani.
   
 17. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #17
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Jana mheshimiwa kiongozi wa upinzani Bungeni Mbowe (MB) ameweka wazi bungeni ukweli kwamba Raisi JK ni msikivu na muungwana. Alitilia nguvu kauli yake kwa kutolea mfano suala la Katiba mpya ambalo baada ya kusikia kilio kutoka kwa wananchi kupitia vyama vya kisiasa, taasisi za kiraia, taasisi za dini na wanataaluma akaamua kuridhia bila kinyongo kuwepo mchakato wa kaatiba mpya. Viongozi wenye hekima, busara na usikivu kama hawa ni wachache sana katika Afrika.

  Wananchi na hasa vijana tuache jaziba kushabikia nchi kutotawalika. Tuige busara za Mbowe, Shibuda, Prof Lipumba na Mrema ili tumsaidie Raisi atupitishe katika mabadiliko makubwa ya kikatiba na mfumo mzima wa utawala wa kidemokrasia kwa amani. Bahati ya kuwa na viongozi wasikivu kama hawa ni chache.
   
 18. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  siku nyingi sana nchi hii haitawaliki jamani
   
 19. Davesto

  Davesto JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 60
  **** dem all politicians mamao
   
 20. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  shibuda na mrema wana busara?mh!
   
Loading...