Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

Attachments

  • BSSP-Child-Labour-04.jpg
    BSSP-Child-Labour-04.jpg
    200.3 KB · Views: 103
Nchi haina furaha kwa sababu kila mmoja anajua uchaguzi umeibiwa kwa mara ya kwanza tangu Uhuru hao
CCM wameshindwa uchaguzi maana watanzania wanajua uchaguzi huu aliyeshinda ni UKAWA na hao CCM wamegeuza matokeo
 
Daaagh yaani kama nimesapu vile ninavyo jisikia au kama naumwa maana sielewi kama naota ama watanzania wamethibitisha urofa wao au tumeibiwa maana...
 
Acheni kujifariji. Magufuli hahitaji tabasamu wala kelele za mtu. Anasema yeye ni kazi tu. Wengi hawana furaha kwa sababu walidanganyika na nyomi. Wakasahau nyomi sio kura. Sasa rais keshapatikana wala hahitaji tabasamu lako. Anataka ufanye kazi tu.
Yule aliyepita alisema Ari mpya,nguvu mpya, kasi mpya" kasi mpya kama ya roketi, bla bla, Maisha bora kwa kila mdanganyika anaondoka kila mdanganyika yuko hoi bin taabani isipokuwa wale waliopata mgao wa EPA, DOWANS na ESCROW anakuja huyu mwenye jina, naomba nisilitaje hapa,ni ile kitu wanatumia walevi au wananing'iniza kwa mlango anasema "hapa kazi tu"

Wadanganyika wako hoi bin taabani hata hiyo nguvu ya kufanyia kazi hawana. Kwa hiyo "hapa kazi tu,Kwanza ajenge nyumba mpya za serikali. Halafu akamalizane na bbc, wanamhitaji kwa mahojiano.

Tuache utani wajameni, NEC ni janga lingine kwa wadanganyika.

Ngoja Rahisi aanze kufunga kambi, kupima barabara za vumbi atakazojenga , msisahau kuwa mkulu mpya anahitaji wakalimani atakapoapishwa , viongozi wa nchi za nje wamealikwa kuja kushuhudia madudu ya NEC au vipi?

Namtakieni wadanganyika nyote, wapumbavu na malofa miaka zingine 5 za umasikini, ujinga na maradhi, maisha bora na hapakazi tu.
 
Mafisadi mjiandae.

Unamaanisha Ridhiwani Kikwete na....any way tusitaje majina kwanza, unamaanisha Escrow, Twiga kapanda ndege, Uchaguzi 2015 pesa imetumika lakini kumbe mshindi alishachaguliwa, Mabehewa mabovu, Safari hewa za nje, Mishahara hewa Hazina, Ruzuku ya siri kwa CCM, Fungu moto la JWTZ na TISS, ..tuendelee ama tusiendelee!!!!???

Au watoto wa maskini watakaokosa elimu na kufanyishwa 'child labor' ndio mafisadi?

Kuna mzee kwenye taasisi fulani ana mke na watoto lakini bosi wake anamla nyuma eti kisa asipoteze ajira, nahisi kama nimekufananisha!
 
Daaagh yaani kama nimesapu vile ninavyo jisikia au kama naumwa maana sielewi kama naota ama watanzania wamethibitisha urofa wao au tumeibiwa maana...
Mmepigwa bao la mkono badugu. Kwa maneno mengine "ukibaka" umefanyika ili kuleta domokrasi.
Mlitegemea nini lakini?
Mlitegemea NEC tume isiyo huru, tume iliyoteuliwa na mwenyekiti wa CCM itangaze mgombea wa CCM ameshindwa huku CCM na NEC zinajua kuwa NEC ikishatangaza mshindi mchezo umekwisha.

Sasa uguzeni maumivu kwa miaka zingine 5.
Kama mnataka goli la mkono lisifungwe tena, kuanzia kesho mpange mkakati wa kupata Katiba mpya itokanayo na matakwa(maoni) ya wadanganyika(wananchi) na Tume huru ya uchaguzi.

Mkikosa hizo kitu mbili hata baada ya miaka 5, mkienda kwa uchaguzi, Mwenyekiti wa NEC anawasuburi awadunge sindano zingine kali zaidi mpaka mutie akili.
 
hahahahaha!!!! ndimu jamani rambeni ndimu labda mtapata furaha.... yaani nimefurahi kweli lowassa fisadi kukosa urais...

hivi mlidhani tutamwachia nchi mtu kama lowassa....?
 
Yaani adi natamani ningekuwa kwenye kitutuli nikiona unaweka tiki kwa rangi ya majani nakutia bonge la kofi kuanzia wew adi kitutuli mnaenda chini alafu nawaambia walio kwenye msitari mwingine aje afanye upumbavu aone .... Maana watu wengi wana kufa kisa hakuna huduma bora za afya alaf wew unayeweka tiki una ndugu na jamaa zako kibao wako mtaani hawana ajira na ata ada ni shiiida alafu ulikuwa mmoja wa watu uliye lalamika kuhusu Escro, Epa na mengi neyo then leo unafanya upumbavu na ulofa nakwambia ilo kofi lingekupa akili na ulofa na upumbavu wako ungekutoka... Embu ninyamaze nisije kulia bure
 
Acheni kujifariji. Magufuli hahitaji tabasamu wala kelele za mtu. Anasema yeye ni kazi tu. Wengi hawana furaha kwa sababu walidanganyika na nyomi. Wakasahau nyomi sio kura. Sasa rais keshapatikana wala hahitaji tabasamu lako. Anataka ufanye kazi tu.

Hebu waambie ukweli
 
Nilifikiri labda mimi ndio naona vibaya,kiukweli maeneo mengi ysmepoa.sana!
 
utoto mwingine raha sana

furaha itoke wapi wavivu, wezi, waliofoji vyeti mashaka matupu kaja jamaa kuwaadabisha

mlitaka apite goi goi mshangilie kula raha wakat hamfanyi kazi

Wape wape vidonge vyao wakimeza wakitema shauri yao
 
Sema sina furaha. Mimi sijalala na wenzangu leo tumekesha kusherehekea ushindi wa tingatinga.
 
Kwa sisi wenye imani Fulani huwa tunasema wananchi wakilaani nchi yao hata aje nani nchi haitakuwa na maendeleo kwa magufuli hata afanye vipi nchi haiwezi songa maana tumeshailaani mpaka tuje kuitengua hio laana
Na hip laana itaondoka tu pale tutakapo kuwa na imani na mtu atakayetuongoza nb "haki huinua taifa Bali dhambi ni aibu ya watu wote "
 
Huu ni ukweli usio pingika. Watanzania wana sononeka sana kama walivyo sononeka kipindi cha Kifo cha Mwalimu Nyerere. Huwezi kuamini kuna Baadhi ya watu wamesema ni bora wakachoma vitambulisho vyao vya kupiga kura kwani hawajaona faida yoyote waliyo ipata baada ya kupoteza muda na mali zao wakijua wana kwenda kumchagua mtu wampendaye. Hii ni LAANA na Tusifanye Mchezo watanzania yatatukuta mambo makubwa sana. Manunguniko na kukata tamaa kwa watanzania Mungu atakuja kutenda miujiza yake.
 
mtoa mada upo sahihi kabisa. ...taft ambazo zimewahi fanywa hapo juzi kati zinaonesha tzn ni nchi ya 113 ambayo watu wake hawana furaha....nahis tuna amani ya nje lkn ndani ya mioyo ya watu hakuna amani

mtu anayependa majungu hawezi kuwa na furahan, Majungu yote UKAWA
 
Back
Top Bottom